Kuna kitabu kimoja chenyewe jina lake silijui lakini muhusika alikuwa anajina la kibantu,na alipokuwa anasoma akajibadilisha jina na kulikatisha jina lake na kujiita BANTA GONTUMBA,alipoanza kazi alijihusisha kimapenzi na mdada wa kihindi,ambapo uhusiano huo ulipelekea kifo chake,na hadithi yetu inapoanza inaanzia maiti Yake iliporudishwa kijijini,halafu ndio ikaja histori huyo.
Kitabu chengine ni UTUBORA MKULIMA,hicho ni cha Shaaba Robert.
Vitabu vingine ni mizimu ya kale.kingine kinaitwa KIMADA,hiki simjui mtunzi wala story yake nilikuwa sijakimaliza,ila kinahusu kuna jamaa alikuwa anaishi na msichana (hawara).
Yule msichana akaja kufa sasa wazazi wake wakagoma kuzika maiti yake.Wakawa wanataka mtoto wao akiwa hai.
Mwanamke aliyebisha hodi jioni.
Mafiga matatu.
Kuna jamaa alioa kumbe alishapata story kuhusu mkewe tangu akiwa mchanga sasa yule mwanamke akawa anaaga kwenda kwao kumbe hafiki anaishia kwa hawara.Sasa akaja kufiwa na mama yake mzazi na jamaa akaletewa taarifa kutoka ukweni akaamua kwenda kuzika bila kumsubiri mkewe kwani alikuwa kaaga ameenda kwao.
Ni vitabu vizuri vya kizamani ambavyo vina mafundisho na pia vinasisimua.Naomba mwenye kujua au kufahamu wapi nitavipata.Mwanamke alobisha hodi jioni na mafiga matatu mtunzi wake ni mmoja na nahisi anatokea Zanzibar kama nitakuwa nimechanganya mwenye kujua anaweza kunisahihisha.
Shukran Wakuu