Natafuta vifaa vya Muziki, Ukiguswa tafadhali!!

benwise

Member
Oct 24, 2015
98
71
Salamu wakuu,mimi ni kijana wa kiume(21)ninaishi mkoani Iringa.namshukuru MUNGU amenijaalia kipaji cha mziki na mpaka hapa nilipo naweza kutumia vyombo vya mziki (kinanda na magitaa aina zote)na pia nina uwezo wa kuandaa muziki kwa program za kompyuta(fl studio,cubase na adobe audition).Ndoto zangu ni kufungua studio yangu ya kurekodi muziki japo kuwa nimefanikiwa kwa kiasi kidogo sana kununua vifaa vichache .kilichonileta kwenu nikuomba kwa yeyote atakayeguswa kunichangia ili nikamilishe,kwa sababu vifaa ni bei ghali na kwa sasa sina uwezo wa kumudu kununua vyote.Lakini naomba nisihisiwe na utapeli wowote ule kwani nipo serius nahitaji msaada wa hali na mali.Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa wote watakaonisaidia
namba yangu ni-0673501746
_________________
Jamani wakuu kutokana na mahitaji niliyonayo na jinsi nilivyokwama nipo tayari hata kufanya kazi kwa mtu yeyote ili nifanikishe malengo hayo.hivyo kama una kazi na unaitaji wa kuifanya mimi nipo tayari kuifanya.
 
Japo Si rahisi, ila Ni vizuri ungeorodhesha vifaa ulivyonavyo, Na vile unavyohitaji msaadaa, pamoja Na gharama zake......ningekushauri Tu ukomae mwenyewe, Ni ngumu kupata msaada hapa kwa shida yako, kichange ununue kifaa kimoja baada ya kingine, ukiwa Na Mixer ndogo inaweza kuwa 500,000 mpaka 700,000, Mic ya ukweli 500,000 mpaka 1,000,000, Monitor Speaker 1,500,000, Na vifaa vichache vingine, Maproducer wengi wanaomiliki studio Leo walinunua kifaa kimoja kimoja, kupata mtu hapa jf akupe lets 3,000,000 Ni ngumu! Pambana mwenyewe mkuu! Bado mdogo baada ya miaka 5 ukiwa Na Malengo utakua Na studio iliyokamilika!
 
Mkuu unaonekana una uzoefu na haya mambo. Kwa wastani studio nzuri inahitaji vyombo vipi na vipi na roughly vinaweza kugharimu shilingi ngapi?
 
Mixer, Mic yenye uwezo, Monitor Speaker, Kinanda, Computer yenye uwezo, Vocal room imbayo iko Na sound proof, Gitaa kwa ajiri ya kuingiza live, Na vitu vingine vichache, kuhusu bei inategemea, nikupe mfano, mixer ya njia 8 lets say inauzwa 1 mil. Na mixer ya njia 50 lets say inauzwa 10 millions, zote zinafanya kazi Ile Ile, tofauti Ni kwamba kwenye mixer ya njia 50 utaweza kuingiza vyombo live kwa wakati mmoja, Utaingiza Kick live, Snare, Gitaa zote, Drums, Na vikorokoro vingi vya kwenye beat Na vocal juu, kila kitu kitaingia kwenye njia yake, hivyo hata kwenye Mixing hautasumbuka, tofauti Na Ile ndogo ambapo baadhi ya vitu itabidi uingize pamoja kwenye njia mmoja....kwa maelezo hayo nadhani utanielewa nikisema kwa 10. Millions, unafungua studio, pia kwa 50 Millions unafungua studio Na hata 200 millions unafungua studio!
 
Hivi misaada ya hivi huwa ipo?

Ushauri wangu mie (endapo hautapewa msaada hapa), tafuta ajira. Utaitumia kama colateral kukopa pesa na kufungua hiyo studio. Utaanza kisimamia huku unamtumikia mwajiri na kulipa mkopo bank. Mkopo ukiisha utaendelea na studio yako.
 
Pole kama nitakukwaza. Nina hasira zangu hapa nina ndugu ana miaka 10 sasa anaomba msaada wa kutimiza ndoto yake. Ila hataki kuajiriwa. Angenisikiliza ushauri huu wa kuanza kidogo kidogo angekuwa mbali sana sasa hivi. Bado anaomba hadi leo
 
Tunao wa hivo. Ndugu lawama hao
 
Mixer, Mic yenye uwezo, Monitor Speaker, Kinanda, Computer yenye uwezo, Vocal room imbayo iko Na sound proof, Gitaa kwa ajiri ya kuingiza live, Na vitu vingine vichache, kuhusu bei inategemea, nikupe mfano, mixer ya njia 8 lets say inauzwa 1 mil. Na mixer ya njia 50 lets say inauzwa 10 millions, zote zinafanya kazi Ile Ile, tofauti Ni kwamba kwenye mixer ya njia 50 utaweza kuingiza vyombo live kwa wakati mmoja, Utaingiza Kick live, Snare, Gitaa zote, Drums, Na vikorokoro vingi vya kwenye beat Na vocal juu, kila kitu kitaingia kwenye njia yake, hivyo hata kwenye Mixing hautasumbuka, tofauti Na Ile ndogo ambapo baadhi ya vitu itabidi uingize pamoja kwenye njia mmoja....kwa maelezo hayo nadhani utanielewa nikisema kwa 10. Millions, unafungua studio, pia kwa 50 Millions unafungua studio Na hata 200 millions unafungua studio!
Ahsante mkuu. Nimekupata kwani umetoa maelezo mazuri. Swali la nyongeza. Kwa nini gitaa tu na si vyombo vingine kama drums, synthesizer au cymbals ndiyo unanunua separately ili kuingiza sauti yake live kwenye mixer wakati kwenye keyboard iliyopo kunapatikana sauti ya kila chombo ikiwemo na hiyo ya gitaa? Kununua gitaa wakati keyboard inaweza kutoa sauti zote si kutaongeza gharama?
 
Hivi misaada ya hivi huwa ipo?

Ushauri wangu mie (endapo hautapewa msaada hapa), tafuta ajira. Utaitumia kama colateral kukopa pesa na kufungua hiyo studio. Utaanza kisimamia huku unamtumikia mwajiri na kulipa mkopo bank. Mkopo ukiisha utaendelea na studio yako.
nakushukuru kwa ushauri wako
 
Japo Si rahisi, ila Ni vizuri ungeorodhesha vifaa ulivyonavyo, Na vile unavyohitaji msaadaa, pamoja Na gharama zake......ningekushauri Tu ukomae mwenyewe, Ni ngumu kupata msaada hapa kwa shida yako, kichange ununue kifaa kimoja baada ya kingine, ukiwa Na Mixer ndogo inaweza kuwa 500,000 mpaka 700,000, Mic ya ukweli 500,000 mpaka 1,000,000, Monitor Speaker 1,500,000, Na vifaa vichache vingine, Maproducer wengi wanaomiliki studio Leo walinunua kifaa kimoja kimoja, kupata mtu hapa jf akupe lets 3,000,000 Ni ngumu! Pambana mwenyewe mkuu! Bado mdogo baada ya miaka 5 ukiwa Na Malengo utakua Na studio iliyokamilika!
Ungekuwa mchango wa harusi ungepata,lakini mchango wa kujitafutia maendeleo kaka funga buti mwenyewe hakuna wa kukusaidia au jaribu kamuone,diwani /mbunge wako wana hela za kuwasaidia vijana huko wilayani
 
Ahsante mkuu. Nimekupata kwani umetoa maelezo mazuri. Swali la nyongeza. Kwa nini gitaa tu na si vyombo vingine kama drums, synthesizer au cymbals ndiyo unanunua separately ili kuingiza sauti yake live kwenye mixer wakati kwenye keyboard iliyopo kunapatikana sauti ya kila chombo ikiwemo na hiyo ya gitaa? Kununua gitaa wakati keyboard inaweza kutoa sauti zote si kutaongeza gharama?
Kwenye utengenezaji wa beat, hasa Bongo fleva, kila Producer Ana style yake ya utengenezaji beat, Ukiacha kick, snare n.k, Keyboard, Gitaa, Marimba, Zeze n.k ndo vyombo vinavyotengeneza Melody katika beat kutokana Na key producer au artist watayoamua kutumia, vyombo vyote vinapatikana kwenye Keyboard but Ni artificial, Ni mtaalam WA Muziki Tu ndo anaweza kusema Hili Gitaa Ni live au sio, live Gitaa Lina sound great, Na utofauti unaonekana, pia Ni rahisi kupata Melody mzuri Kama utatumia Gitaa au Keyboard, Gitaa Ni muhimu zaidi kuliko Drums hasa studio za Kibongo fleva sababu beat za bongo fleva au Hip hop, Ni Mara chache zinakua Na drums, nyingi zinakua Na Gitaa hasa beat za kuimba, Producer anaweza tengeneza beat mwaka mzima bila kutumia Drums labda kwa radha kidogo ila hawezi kupitisha siku 2 bila kuingiza radha ya Gitaa kwenye Beat, Kama sijakosea beat ya Nyimbo ya Chid ya Dar es salaam Stand, in radha ya Hindi, Ni drums peke yake zimeleta radha Ile, but may be Ni asilimia 10 Tu ya beat za Chid zina Drums, 50% au 60% zina gitaa ndani!
 
Ahsante ndugu kwa maelezo yako ya kitaalamu.
 
Karibu Sana Mkuu! Kwa kuongezea Tu now days Wasanii Na Producers wanataka vitu vingi viingizwe live, Ili hata msanii akienda fanya live show, Bendi itayopiga nyimbo live, Na Nyimbo original visitofautiane, zamani Producer waliweka vitu kibao kwenye beat ambavyo Ni artificial ikapelekea shida kwa Bendi inayopiga live nyimbo ya msanii, Kama utakumbuka Mara nyingi tulisikia Live show ya msanii, but nyimbo original Na live tofauti, Ni tofauti Na America, ambapo wasanii Kama Kanye anapotaka radha ya mdundo wa ngoma ya kiafrica kwenye beat yake, Yuko tayari kulipa pesa nyingi kumtoa mpiga ngoma West Africa mpaka America, kwa ajiri ya kuingiza Tu radha ya ngoma, Na itaingizwa live, but now days Na sisi tunajaribu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom