Hivi mitandao yetu ya kibongo inatoa speed gani ya mwisho kwa downloading?
Ntakupa analysis ya haraka haraka ila kabla ya kuendelea mbele ni vema kujua baadhi ya maneno ya speed zitumikazo na Telecom companies
1.
LTE A.K.A 4G
2.
HSPA,HSPA+,DC-HSPA+
Twende mitandao ya bongo
1.
SMILE TANZANIA
Hawa nafikiri hamna ubishi kila mtu anawajua kwamba ni LTE na speed yao japo hawaiweka wazi ila Modem zao ni 100Mbps japo 4G inaweza fika hadi 150Mbps
2.
AIRTEL TANZANIA
Airtel wamekua wakinadi 3.75G Speed na wengi tumekua tukiwadharau ila ukweli ni kwamba kwa hapa Dar hamna mtu GSM network inaweza wafika hawa jamaa kwa sasa hapa Bongo maana wanadai wanayo minara 400 ya 3.75g
Na kama inavyoonekana kwenye picha hapa chini wanayo DC-HSPA+ ambayo ni 42Mbps
Na hii imetapaaka karibu Dar nzima hawajabagua maeneo
3.
Vodacom Tanzania
Hawa walinadi kwamba watatuletea LTE na
WiMAX lakini tumesubiri mpaka matumbo yameuma...
Kwa maeneo nako ishi na maeneo kama matatu nilipowajaribu Vodacom nimegundua bado sana kumfika Airtel maana kati ya hayo maeno niliyoyajaribu hamna hata sehemu wamesoma DC-HSPA+ wameishia tu HSPA+
4.
MIC TANZANIA
Hawa Tigo wana mbwembe nyingi ila mtandao wao kimeo sana achilia mbali kwamba mwaka jana walitangaza wana 4G yenye max speed ya 42Mbps katika maeneo ya UDSM,UDOM,MAKUMBUSHO na MASAKI lakini sijaona kitu labda watu wanaoishi hayo maeneo watwambie
Mimi ninakoishi wanayo HSPA+
5.
ZANZIBAR TELECOMMUNICATION(ZanTel)
Hawa wako kote kote CDMA na GSM Technology ila sijaona kipya sana sana katika huduma za huu mtandao
Sometime napata HSPA+ someties HSPA
6.SMART/BOL
Mpaka sasa hawa jamaa kwa hapa DAR hamna kitu ni full 2G japo wamewapa shavu watu wa mkoani na sisi wa Dar wametuaidi 4G