Natafuta ukweli wa CCM niupate uongo wa Dk Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natafuta ukweli wa CCM niupate uongo wa Dk Slaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mnyamahodzo, Apr 21, 2009.

 1. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Ili niujue UONGO lazima niwe na UKWELI. Nitaendelea kuuamini uongo kuwa ndiyo ukweli hadi pale nitakapoujua UKWELI.Nikijua ukweli ukaniletea uongo ukisema huu ndiyo ukweli nitakwambia wewe ni MWONGO kwa kwa sababu kile UNACHOSEMA NI UONGO.
  Wakati sakata la wizi wa Benki Kuu linaanza kupigiwa kelele, viongozi wa vyama (CHADEMA,CUF,TLP na NCCR-Mageuzi) walitoa matamko yao kupinga wizi uliofanywa na CCM, kuiba fedha za umma na kuzitumia kwenye kampeni 2005. katika mkutanoi huo Dk Slaa ndiye aliyetamka wazi kuwa kiasi cha shilingi bilioni 10 [kupitia kampuni ya Deep Green] waliiba fedha toka Benki Kuu ili zitumiwe na CCM kwenye kampeni mwaka huo.Tundu Lissu pia alikuwepo wakati viongozi hao wakitoa tamko lao.
  Taarifa hizo zilipotolewa na vyombo vya habari vikiwemo gazeti la Mwananchi na ThisDay, Yusufu Makamba,Katibu mkuu wa CCM, alijibu mapigo.

  ""Katibu Mkuu wa Chama hicho, Yusuf Makamba aliliambia gazeti hili (Mwananchi) jana kuwa tuhuma kwamba CCM kiliiba fedha kwa ajili ya kufanikisha kampeni zake za uchaguzi hazina ukweli wowote.

  "Siwezi kutoa ufafanuzi juu ya madai ya uongo. Uongo haujibiki unakaliwa kimya," alisema Makamba.

  Alisema wapinzani waliotoa tuhuma hizo walipaswa kuzitoa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2010 ili jamii iweze kuwaunga mkono, badala ya kuzitoa sasa na kumaliza uongo wote uliotakiwa kutolewa wakati wa uchaguzi huo.

  "Uongo huo ungewasaidia kama wangetoa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2010, sasa wanapoumaliza leo watasema nini kipindi hicho kikifika?" alihoji

  Mbali na BoT na CCM, watuhumiwa wengine ambao umoja wa wapinzani umewahusisha na ufisadi huo mpya ni kampuni moja ya Afrika Kusini, Benki moja nchini na mawakili wawili wa kampuni moja ya uwakili nchini""

  Ikumbukwe kuwa kipindi hicho uchunguzi wa wizi wa fedha za EPA ulikuwa bado haujakamilika ile ripoti ya E&Young ilikuwa haijatolewa.

  Sasa mimi nina maswali kadhaa, kwa uchache;
  1. Dk Slaa alisema uongo,ili nijue kuwa alichosema ni uongo wafurukutwa na wakereketwa wa CCM niambieni ukweli ili nithibitishe Dk ni mwongo na nimwitwe hivyo.
  2. Kwa kuwa uongo haujibiki wanaCCM nipeni ukweli.
  3. Ili jamii ukiunge mkono kwa chama chochote ni vizuri kikitoa tuhuma za uongo, kama zile za "tumekamata visu na mapanga vyenye rangi ya chama chao,tunajua wanakusudia kumwaga damu" na "huyu si mtanzania safi wa kwasababu alikuwa mwanachama wa HIZBU"?
  4. Katika kampeni za uchaguzi Mkuu 2010, tutarajie vyama vya siasa ikiwemo CCM kusaidiwa na uongo ili vishinde?

  Natafakari, niko njia panda, nikitafuta ukweli.
   
 2. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Hivi CCM hadi sasa mnaamini uongo unasaidia kuwafanya mkubalike katika jamii?
  Umepita mwaka sasa toka nilipoandika post hii. ninyi wa CCM tuonyesheni uongo wa Dr Slaa.

  Natafakari bado!!
   
 3. U

  Uswe JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  hadi leo hawajajibu? teh teh teh!
   
 4. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #4
  Apr 23, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  Unadhani ni rahisi kujibu hoja kama hii!?..
   
 5. hKichaka

  hKichaka Senior Member

  #5
  Apr 23, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 199
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Chama makini kama CDM hawawezi kusema uongo.Angali tu hata wabunge wake ni moto wa kuotea mbali.Kila anaeongea ana point ya msingi, kwa sisi wasomi ukweli tunaujua .
   
 6. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Hapo kumbuka JINA LANGU... "UKWELI KITU GANI.." Maana yake ni hii,ukweli wa mkubwa kwa mtoto ni uongo na ukweli wa wa mtoto kwa mkubwa ni Uongo...sasa ukweli ni kitu gani? kuna baadhi ya watu wakiwemo wanaojiita WASOMI ndani ya CCM, tena wenye MVI hadi masikioni, utakuta wanaapa hadharani eti wapinzani ni waongo na sera/taarifa zao ( juu ya WIZI MKUBWA ) za ufisadi serikalini uliofanywa na CCM na uthibitisho upo....pia wapo watu wengine nikiwemo mimi tunajua na kuamini kuwa wizi na ufisadi mkubwa ulifanywa na unaendelea kufanywa na CCM... sasa hapo likija jicho la tatu, litahoji ukweli ni nn?
  Umenielewa kaka? hii kitu ni very contradicting despite yhe facts..
   
 7. Quinty

  Quinty JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 463
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hawa wamekosa cha kufanya...!
   
 8. S

  Simon B james Member

  #8
  Apr 23, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hebu fikiri. Kama kweli taarifa za Dk slaa zingekuwa za uongo sasa hvi Kiwete siangetumia madaraka kumswaga jela? Wangapi waliswagwa ndani kwa kosa hata la mke? Unamjua Babu sea? Nini kilicho mswaga ndani. Naomba nikutoe shaka Slaa ni mtafiti na msomi hawezi kukurupuka. Achana na degrii za kikwete za kupewa
   
 9. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #9
  Apr 24, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Wanafalsafa na wanasaikolojia tunaomba mtusaidie jambo hili {wakati tunasubiri majawabu toka kwa wakereketwa na wanachama wa CCM}; kati ya hoja yenye ukweli na hoja yenye uongo ni ipi iliyorahisi kuikanusha?
   
Loading...