Natafuta shule nzuri Arusha au Moshi

Natafuta shule nzuri Arusha au Moshi

sambeke

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2014
Posts
713
Reaction score
651
Wanajamvi, naombeni mnisaidie,

Mtoto wangu wa kike anamaliza darasa la saba mwaka huu. Nisaidieni kupata shule bora. Iwe Arusha au Moshi:

1. Iwe shule yenye kuzingatia maadili
2. Inayofanya vizuri ki academic
3. Ikiwa ya mchepuo wa sayansi ni bora zaidi
4. Napendelea zaidi shule za Catholic.
 
Mpeleke Precious Blood iko maeneo ya Arumeru. Shule hii ni ya Masista wa Kikatoliki na kwa kweli inafundisha maadili mazuri. Performance ya shule hii mwaka 2013 wa nne kitaifa, 2014 wa nane kitaifa. Mpeleke hapo na hutajuta.
 
shule za masista ni nzuri sana kuanzia secondary ila kwa shule za msingi siyo wazuri sana ni wakali sana kwa watoto
 
shule za masista ni nzuri sana kuanzia secondary ila kwa shule za msingi siyo wazuri sana ni wakali sana kwa watoto

Yaaa ukali unapitiliza hadi watoto wanawaogopa sana, wanakuwa na hofu muda wote
 
Ungetaja na level kama ni advance au ordinary labda ungepata msaada vzuri zaid
 
mlete mkuu day secondary shule ni ya kutwa na bweni.ipo wilaya ya rombo mabweni yanamilikiwa na parokia ya mtakatifu sesilia mkuu!!!mimi nimeanzia hapo o level na sasa nipo hapo advance.shule ni ya serikali
 
Kwa moshi mpeleke visitation girls ama kibosho girls ama weruweru ni ya serikali ipo chini ya masista kama kafaulia kata muhamishie hii shule inafanya vizuri na ina mazingira mazuri, st.Mary goreth ni nzuri ila naona kuna wahindi wengi hivyo inaweza kuwa kuna ubaguzi ili sina uhakika
 
Naamini hata mkuu wa shule hawezi kujitokeza hadharani kuinadi. Btw, hawafundishi kwenda "Kenya"??


mlete mkuu day secondary shule ni ya kutwa na bweni.ipo wilaya ya rombo mabweni yanamilikiwa na parokia ya mtakatifu sesilia mkuu!!!mimi nimeanzia hapo o level na sasa nipo hapo advance.shule ni ya serikali
 
Kwa vile ipo rombo Guus??????huku ni kenya full mtandao ni safaricom radio ni za kenya tu!!!!!tuna use kenya shillings
 
Last edited by a moderator:
KAFA.cOm unadhani hata nilikuwa najua kuwa wilaya ya rombo ipo kenya, mimi nilikuwa natiririka tu!!

Ila toa huo mkono katika shavu, unatuhudhinisha na wengine huku.
 
Last edited by a moderator:
Nashukuru sana jamani wote kwa ushauri wenu
 
Hakikisha amepata alama A nikuunganishe na MaryGoerth hapa Moshi hakika utakuwa umemtengenezea maisha!
 
Back
Top Bottom