Kauli ya Rais Magufuli ya 'Watu Kuishi kama mashetani' inahalalisha maovu

tajirijasiri

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,864
3,851
"Kuna watu walikuwa wanaishi kama malaika, ni lazima tuwashushe waishi kama mashetani"
Rais John Pombe Joseph Magufuli, Machi 2016.

F1CAE0AA-8DC8-4F58-A08F-2A5CAABAF478.jpeg


Wote tunajua kuwa kuishi kama malaika ni kuishi maisha mazuri, tulivu yenye amani, furaha, raha na bila dhambi yaani utakatifu wa kimungu. Na kuishi kama shetani ni kuishi ndani ya shida, maovu na dhambi za kila aina kama uongo, wizi, uzinzi, tamaa, utapeli, ufisadi, rushwa, dhiki, magonjwa, mabalaa na kila aina ya mabaya.

Unapokuwa kiongozi, hasa kiongozi mkuu wa nchi inakubidi uchunge sana kauli zako, kwani zinaweza kupoteza maana halisi na kuleta mkanganyiko.
 
Umeamua kutoa kijisehemu iko cha maneno ili mradi ueleweke, ungeeleweka zaid kama ungeleta speech nzima. Hukumwelewa ndo maana ktk speech nzima ulisikia iyo kauli tu
Kwa vyovyote vile iwavyo, hiyo kauli haikupaswa kuwa kama mfano kwa kile alichokikusudia kukisema. Malaika hawezi kufananishwa na wabadhilifu, wala rushwa na wapokea mishahara hewa. Malaika ni uwasilisho wa kiroho unaojengeka kama alama ya utakatifu, matendo mema, maisha safi yasiyo na dhambi.

Kuishi kama shetani unakufahamu. Shetani ndio baba wa mabaya yooote ya ulimwengu huu.

Hapo Mkuu alibugi na haipaswi tukamuacha akapotea.

Tunamheshimu na tunathamini vita yake juu ya rushwa na ufisadi. Ila hana budi kuchunga kauli zake.
 
Kwan mlikuwa hamjui kuwa mnaishi maisha ya kishetani? Rais yupo sawa kabisa na hana nia ya kuwafanya watu waishi kama malaika ila wote tuishi kama mashetani!
 
Unachambua vifungu vya maneno Kama unasoma bible
Akutakiae mema atakukosoa unapotoka nje ya mstari, lakini asiyekutakia mema atakuacha uendelee kupotoka.
Huu mfano wa Mkuu haukuwa sahihi japo alikuwa na nia njema.
Usipochunga kauli unaweza kufuta maana halisi iliyokusudiwa.
 
Kiukweli washauri wamwambie apunguze kucheza na jukwaaa.lasivyo itamponzaaa
Wanamwogopa kumwambia ukweli ili wasije 'wakatumbuliwa'. Kwa hivyo wataendelea kumpigia makofi hata akitoka uchi alimradi watoto wapate mkate. Ndio maana haja ya kupata katiba ya wananchi iko pale pale ili kuondoa umungu-mtu!
 
"Kuna watu wanaishi kama malaika, ni lazima tuwashushe waishi kama shetani" Rais John Pombe Joseph Magufuli, Machi 2016.

Wote tunajua kuwa kuishi kama malaika ni kuishi maisha mazuri, tulivu yenye amani, furaha, raha na bila dhambi yaani utakatifu wa kimungu. Na kuishi kama shetani ni kuishi ndani ya shida, maovu na dhambi za kila aina kama uongo, wizi, uzinzi, tamaa, utapeli, ufisadi, rushwa, dhiki, magonjwa, mabalaa na kila aina ya mabaya.

Unapokuwa kiongozi, hasa kiongozi mkuu wa nchi inakubidi uchunge sana kauli zako, kwani zinaweza kupoteza maana halisi na kuleta mkanganyiko.

Mizuka baba mizukaaa!! Jana hafahamu dhana ya Urais bado...
 
Uruga ruga utamponza,tatizo la watu wengi walio zaliwa na kukulia bara na kuishi uko muda mrefu ni kushindwa kujua na kuimudu kazi nzima ya kucheza na maneno!jk alikuwa kilaza,ila alijua kucheza na maneno!magufuli anaitaji trimming ya hali ya juu,na sipati picha hapo ameenda kuhutubia U.N,na ile lafudhi yake,halafu autoe mfano kama huo...dah,sijui watz tuta ziweka wapi sura zetu
 
Back
Top Bottom