Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,559
- 41,077
Kauli ya Rais kuhusiana na umuhimu wa katiba, imethibitisha yafuatayo:
1) Rais wetu hajui maana wala kuelewa uzito wa Katiba ya Nchi
2) Rais wetu haelewi kuwa kinachowekwa kwenye kitabu kinachoitwa katiba ni maamuzi ya Wananchi wa nchi husika juu ya utawala wa nchi. Hivyo kitabu hicho hakipewi heshima kwa sababu ni kitabu bali kwa sababu ni rejea ya yale wananchi waliyoyaamua kuhusiana na utawala wa nchi kuanzia taratibu za kuwapata watawala wa wa nchi, bamna muundo wa utawala unavyotakiwa kuwa, namna ya upatikanaji wa sheria, n.k.
3) Rais wetu hajui kuwa bila katiba, hata yeye binafsi, hana tofauti na Khadija Kopa au karani wa kiwanda cha konyagi.
4) Rais hajui kuwa bila katiba, yeye siyo Rais wala siyo kiongozi yeyote. Bila katiba hana uwezo wa kumpa madaraka mtu yeyote.
Naamini mtu anayetakiwa kupewa shule ya nguvu kuhusiana na katiba ni Rais wetu.
Bahati nzuri au mbaya nchi yetu inavumilia kila aina ya uozo. Ingekuwa ni nchi ambazo wananchi wake hawavumilii uozo wa aina yoyote, ofisi ya Rais ingekuwa katika wakati mgumu sana baada ya Rais kutoa kauli inayoashiria kuwa katiba aliyoapa kuulinda si chochote na si lolote, ni kitabu tu kama cha Abunuwasi. Na fikra hizi ndizo zinazowafanya watawala wetu kutoheshimu katiba. Wakati kiuhalisia Rais kutoheshimu katiba ni uhaini dhidi ya umma.
Rais kama hajui uzito wa katiba, kwa kweli ni hatari kubwa sana. Wahusiaka wampeleke darasani Rais wetu haraka sana ili asiendelee kutamka mambo ya ajabu yanayofisha Taifa na nafasi yake.