Natafuta rafiki wa kawaida wa kike

Natafuta rafiki wa kawaida wa kike

nyakanazi

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2013
Posts
307
Reaction score
397
Nahitaji rafiki wa kike kwa urafiki wa kawaida tu. Madhumuni hasa ni kuchat juu ya mambo mbalimbali ya maisha kwa ujumla (opportunities, professional, biashara, kilimo hususan cha biashara, ushauri juu ya mambo mbalimbali). Ningependa mtu nisiyefahamiana naye ambaye naweza kuwa free kumweleza chochote kile na tukashauriana juu ya chochote kile bila woga.

Sifa: Awe mwanamke mwenye upeo wa juu sana wa kuelewa mambo, awe ana uwezo wa kufanya critical analysis ya mambo mchanganyiko na akaja na ushauri wa kiutafiti. Sipendi nitaje elimu, maana elimu zenyewe siku hizi si kipimo cha uelewa wa mtu.

Karibu, kama uko serious, wewe ni twangie kwa siri kwakuwa hayo si ya kuweka hadharani.

Sifa zangu: Intelligent and analytical gentleman

Karibu.
 
Duh... Mie upeo wangu mdogooo, ngoja nikusabahi tu. Hujambo nyakanazi?
 
Last edited by a moderator:
una mke? kuwa na urafiki na wewe, ni sawa na kuwa consultancy je utanilipa?
 
du nyakanazi! sasa kama ni rafiki tu mbona wachambua sana? uko pande zipi kozi kqmq uko songea mimi bk ni mipango gani itaendelea nitumie pm
 
Hilo ndio tatizo kubwa sana la sisi Watanzania kwamba wengi wetu tunashindwa kujiuza na kujua thamani yetu na matokeo yake watu wengi wanashindwa kupita kwenye usaili makini wa kazi kwakuwa hatujijui thamani yetu ni nini. Unaulizwa kwanini unadhani tukuchukue wewe na asiwe mwingine, unabaki unagwayagwaya tu, wapaswa ujinadi kuwa wewe ni competent na unauwezo kuliko wengine kwakuwa na sifa A,B, C......
Si kwamba najisifia ila ninajijua kuwa ni mbora kiasi gani, kwani nafanyakazi na watu waina mbalimbali kielimu, kitaifa, kwahiyo unaweza ukaona nafasi yako ipo wapi ukijima na waliokuzunguka, uwezo wako ni upi kiufanisi wa kazi, uchangiaji wa mawazo muhimu katika changamoto kubwa za kikazi na kimaisha. Vilevile unapata feedback kutoka kwa watu wanaokuzunguka kuwa wewe ni mtu wa aina gani, haiwezekani kila mtu aseme wewe ni mtu wa aina fulani halafu ikawa uongo. Sisi Watanzania tuwe na ujasiri wa kuweza kujiona ni competent people na tunaweza na kushindana na yeyote yule pahala popote pale na kwa lolote lile hasa inapokuwa suala linalohusiana na field yako. Kwa hiyo mimi najijua vizuri sana kuliko mtu mwingine yeyote yule. Tuwe nauwezo wa kufanya self-crtical analysis na evaluation ya kila kitu tunachofanya katika maisha ili tuwe na uwezo wa kujirekebisha na kuwa bora zaidi hata kama tunafanya vizuri katika nyanja fulani kwani "No matter how good you are, still there is a room for improvement.
Nadhani mmenielewa vizuri tu, si kwa nia ya kujisifu bali kueleza ukweli kuwa mimi najielewa kuwa ni nani, na amini nakwambia hii imeleta mafanikio makubwa sana katika maisha, so anza kujielewa nafasi yako wewe ni nani. Na ndo maana katika Business management and analysis kuna vitu kama SWOT Analysis, Balanced scorecards, Benchmarking etc hizo strategic tools zinazoweza kuisaidia kampuni kujua nafasi yake katika biashara ya ushindani na kujua nafasi ya makampuni yaliyomo katika the same industry ili iweze kuchagua strategy zilizosahihi zitakazowezesha kampuni hiyo ku outperform kampuni zingine. Kwahiyo hii inaweza kuwa translated kwa mtu binasfi, usipojijua wewe ni nani, strong point na weak points zako ni zipi huwezi kupiga hatua kwenye maisha. Ndo maana nasema nataka mahusiano na mtu aliye na uwezo wa kuyaelewa haya mambo ili tunapoongea tunaongea lugha tunayoelewana. Asante sana
 
Asante, sichambui sana. Najaribu kutafuta mtu tunayeweza tukawa na upeo huu mdogo unaofanana wa kuelewa mambo. Unajua humu kuna watu wa aina nyingi, sasa si rahisi kushirikiana na kila mtu mwenye upeo fulani ndo maana ni muhimu kufanya mchujo wa chenga na mchele. Ni kwa nia nzuri tu na si ya kubagua.
 
Ndio yaleyale ni nayoyasema kuwa upeo wa kuelewa mambo ni kitu muhimu. Kuwa na mke au mume hakukufanyi wewe usiwe na mashirikiano ya kawaida na ya faida katika maisha na mtu wa jinsia tofauti. Pesa ni matokea ya kazi na si kazi matokeo ya pesa. Una uhakika gani kama mimi nitafaidika zaidi na mahusiano haya na wala isiwe wewe. Kwenye jamii forum kuna watu wa aina mbalimbali na wakati mwingine ninaimani tunapata nafasi ya kuwasiliana na watu ambao katika hali ya kawaida ya kuonana uso kwa uso tusingeweza kupata nafasi hiyo kulingana na tofauti zetu mbalimbali za kinyazifa, mali, elimu, jinsia etc. Kwahiyo nafasi zinapotokea tue na positive attittude ya kutaka kujifunza na kuelewa zaidi rather than challenging unnessarily. Jaribu, hulipii kitu, ukiona hakuna mwelekeo unajitoa taratibu tena bila kuoga kama inabidi.
 
Umepiga msumali kwenye kidonda. Kama hujijui wewe mwenyewe kuwa unauelewa gani ni tatizo kubwa sana. Unapaswa ujijue wewe unauelewa kiasi gani na uwe tayari ku autheticate uelewa wako kwa yeyote yule. Napenda kuongea ninapokutana na mgeni bila kujali ni nani. Nilikuwa safarini kweye KQ (Dar-Nairobi-Entebbe). Nilipata bahati ya kukaa kitu kimoja na dada mmoja Mkenya. Katika kujitambulisha akaniambia yeye ni the Head of Customer Service ya Kampuni moja huko Nairobi na kwa muda huo alikuwa Uganda kwa miezi sita wakufungua matawi na ulikuwa mwezi wake wa mwisho kabla hajaenda Dar TZ kufungua matawi yao pia. Kwabahati nzuri tumekuwa tukiwasiliana, niliporudi TZ aliniambia amepata tabu sana kuwafanyia usali vijana wa Kitanzania waliomaliza degree kwakuwa hawakuwa na uwezo kabisa wa kujieleza na kujinadi hasa kwa lugha ya Kiingereza ambayo ni muhimu kwao kama Customer Service department ambayo inahusika na watu wa Mataifa mbalimbali. Ilibidi awaruhusu wajieleze Kiswahili, lakini lazima tukubali kwamba sisi hata kwakiswahili inakuwa taabu kujieleza kinagaubaga hasa kwa wasomi wa siku hizi, ukiangalia watu wanavyojieleza kwenye TV unatingisha kichwa. Nini tatizo letu. Wakati umefika, tujijue sisi ni kina na nani na ni upi upeo wetu katika kuelewa mambo na hasa yanayohusu fani zetu za kazi. Nimepata bahati ya kushiriki kuwasaili watu magraduates, ni aibu, inasikitisha........
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom