CHE GUEVARA-II
JF-Expert Member
- Jun 17, 2010
- 571
- 157
nyau wangu ana vitoto tele njoo uvichukue maana nawaza pa kuvipeleka aiseeh
mkuu upo wapi kama upo dar mm nikuletee free kabisa. garama mpaka za kufika kwako juu yangu mkuu.
Huyu atazaa siku si nyingi nitakupatia wote kama utakua bado hujapata.
nyau wangu ana vitoto tele njoo uvichukue maana nawaza pa kuvipeleka aiseeh
mkuu upo wapi kama upo dar mm nikuletee free kabisa. garama mpaka za kufika kwako juu yangu mkuu.
Kuna nyau anasumbua sana hapa sijui nikukamatie!
Habari zenu wadau?
Naomba msaada.
Natafuta paka (domestic cats) wawili - dume na jike.
Wasio na mabaka kama ya chui.
Wenye mabaka kama ya chui wana asili ya kuwa deviant (paka mwitu)- huwa na tabia ya kukamata vifaranga na hata kuku.
Nawahitaji sana, panya wananisumbua.
Sipendi kutumia sumu au mitego - ni kinyume na taratibu za mazingira, pia hazimalizi tatizo - hupunguza tatizo tu.
Njia sahihi ni kufanya mazingira yasiwe rafiki kwa panya (i.e kutoacha mabaki ya vyakula hovyo au kutohifadhi vibaya vyakula) na biological control (kwa kutumia paka).
Natanguliza shukrani.
Mara unafuta PAKA,
Mara unatoa mongozo wa njia sahihi za kudhibiti PANYA,
Muda sio mrefu utaanza kutafuta MBWA na baadaye utatafuta PANYA.
Mimi nikushauri: Paka sio mnyama wa kufuga ikiwa huna hela kama wengi wetu tunavyodhani. Leo hii wewe unatafuta JIKE na DUME, style anayokujanayo mtu anayetaka kufuga ng'ombe au mbuzi akiwa na lengo wazaliane na kuongzeka. Je, hiyo ndio nia yako?
Ikiwa huna hela za kuwafunga kizazi hao PAKA wako, basi naomba uwe na huruma kwa jirani zako. Nyau anazaa mara 2 kwa mwaka na huzaa watoto kadhaa, cha kuzingtia ni kwamba, hutakuwa na wa kumuuzia.Jirani yangu alipoanza na nyau mmoja JIKE, hakuyazingatia haya. Tena yeye hakuwa na super strategy kama wewe uliyeamua kutafuta DUME na JIKE sasa hajuti peke yake, bali mtaa mzima tunajuta.
Sumu ya PANYA ipo hadi ya 500.
Nenda pale open university of Tz kinondoni biafra, kuna nyau wengi sana. Yaani wametapakaa kila kona. Idadi ya pusi pale inalingana ya wanafunzi.