Natafuta nafasi ya kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natafuta nafasi ya kazi

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by nkisumuno, Jul 15, 2012.

 1. n

  nkisumuno JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa mwenye taarifa ya shirika lolote linalolipa mshahara mzuri au kampuni Mimi nina taaluma mbili 1. ni mwalimu kada niliitumikia kwa muda mrefu na naendelea kufundisha shule za msingi. 2. Mimi ni Counselor nina shahada ya unasihi (Bachelor of couselling). Baada ya kumaliza masomo yangu ya shahada niliomba kubadilishiwa cheo lakini kutokana na ukiritimba wa nchi yetu nikaambiwa shahada yangu haitambulikani licha ya umuhimu wa taaluma hiyo kama nitakavyoeleza umuhimu wake hapa chini. Baada ya hapo nikaomba likizo bila malipo ili nifanye kazi na Kituo cha Afya kama mratibu wa UKIMWI nikakataliwa. Hata hivyo nikaamua kufanya kazi kwa mkataba wa mwaka mmoja kwa muda fulani mwisho wa juma na kila baada ya kazi. Baadaye ya mkataba kwisha niliamua kuachana kutokana na kipato walichokuwa wananilipa. Katika Tanzania nimegundua kuwa ili upate kazi lazima uwe na mtu wa kukupigia debe bila kujali uwezo ulionao. Aidha uwezo wa viongozi wetu ni mdogo kutokana na sifa wanazoajiriwa kutokana na kufahamiana na nani baadala ya kuajiriwa kwa kuwa unajua nini. Nilipowambia nimemaliza shahada yangu nilijibiwa kuwa shahada yangu haitambulikani bila kuuliza nilichosoma kina faida gani katika jamii. UFUATAO NI UMUHIMU WA UNASIHI (COUNSELLING) 1.Ni muhimu katika kutoa elimu ya malezi bora, Tuna mafisadi wengi kwa vile tu wana matatizo ya kisaikolojia kwa vile tu waliikosewa kulelewa kisaikolojia na kujikuta hawajiamini. kwa vile hawajiamini wanafikiri wakiwa na mali basi wataheshimika, wataonekana, kwa ufupi wanatafuta kujulikana na kulindwa na mali. Na ili mtoto ajiamini anatakiwa apate malezi bora kwa kufuata kanuni bora za kimalezi kisaikolojia akiwa na umri wa miaka 0-5 kisha miaka 5-12 Akikosewa hapo basi mtoto huyo hataweza kujiami. Na mtoto anayekosa kujiamini basi ataweza kushiriki katika matendo ya ulevi, umalaya na mambo mengi maovu akiongozwa na wale wenye tabia mbaya kwa kupelekeshwa. Kwa hiyo tabia mbaya kama kuvuta bangi, kuiba, rushwa n k ni matokeo ya jamii kuiga kwa vile tu hawajiamini. Muhimu hapa ni kuwapa nafasi wataalamu watoe elimu jinsi ya kulea watoto ili waweze kujiamini na kuwa na jamii bora. Leo hii waafrika wengi hawajiamini kwa vile tu Wazungu waliwaharibu waafrika wajione hawafai. Ni viongozi wachache katika Afrika wanaoweza kuamini kuwa maendeleo ya waafrika wanaweza kuleta maendeleo yao pasipokutegemea wazungu. Unasihi kwa ngazi ya shule utasaidia wale wanafunzi wasiojiamini waweze kujiamini pale wataalamu wa kisaikolojia (wanasihi ) watakaporejesha kujiamini kwa kuwajenga kisaikolojia waliopoteza kujiamini. Kuwasaidia wale waliopoteza wapendwa wao na kuathirika kisaikolojia, wanaoumwa magonjwa yanayosababisha wanyanyapaliwe. Familia wapate elimu kuhusu umuhimu wa kuvumiliana katika ndoa ili kulinda madhara yatakayowapata watoto endapo wataachana Kutoa elimu kuhusiana na matatizo ya kisaikolojia kama vile athari za msongo wa mawazo nakadhalika. msongo wa mawazo una madhra makubwa katika kila sekta, mfano daktari mwenye msongo wa mawazo anaweza kumpa dozi isiyostahili mgonjwa na kusababisha madhara zaidi ikiwa ni pamoja na vifo. mwalimu anaweza kufundisha au akawa mkali kwa mwanafunzi kwa vile tu anamsongo wa mawazo, Anayefanya viwandani au kushughulika na mashine anaweza kuharibu vifaa au kuweza kupata ajali kwa kujikata na mashine kwa vile tu anamsongo wa mawazo. Hivyo ni vema ofisi ziwe na wanasihi kwa kila sekta ili watu wapate nafasi ya kupata msaada wa kisaikolojia ili kupunguza msongo wa mawazo. Zifuatazo ni baadhi ya dalili za msongo wa mawazo 1.kula sana au kupoteza hamu ya kula 2.kukosa usingizi au kulala usingizi sana 3.kupenda vitu vitamu kama vile pipi, biskuti, soda 4.kunywa pombe sana 5. Kupoteza hamu ya tendo la ndoa au hamu ya tendo la ndoa kuzidi 6. Kupoteza hamu ya kuwasiliana na ndugu au marafi (Kuwachukia) 7. Kujiskia mchovu bila sababu za msingi Hizo ni baadhi tu ya dalili za msongo wa mawazo Ili kupunguza msongo wa mawazo (stress) fanya yafuatayo 1. Fanya mazoezi ya viungo kama kukimbia, kuendesha baiskeli nk 2. Punguza vyakula vya mafuta, kula mboga na matunda kwa wingi 3. Jithidi kuwa jirani na mtu unayempenda au kundi la watu baadala ya kuwa peke yako 4. kama kuna mnasihi jirani unayemfahamu mwombe ushauri 5. Fanya kitu unachokipenda kama vile kuangalia mpira, tv nk 6. Punguza kufanya kazi, uwe na muda wa kupumzika Nimejaribu kuonyesha kwa ufupi umuhimu wa Unasihi katika jamii ya kitanzania Nawasilisha .
   
 2. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  andika vizuri kwa paragraf ili uleweke
   
 3. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Good fellow counsellor,nimegraduate 2008 hadi leo sijaajiriwa na mtu, if at all you want to make use of your career as a counsellor fungua office yako binafsi anza kupiga kazi,otherwise ni ngumu kupata firm au company itakayokuajiri,bado ni watu wachache wanaotambua umuhimu wa counselling bongo hii!
   
 4. m

  muhinda JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2012
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 337
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Nashauri utafute partners nfungue office. Hii huduma ni adimu sana hapa Tanzania
  trust me kuna watu wengi wana matatizo lakini hamna pa kwenda kupata iyo counselling (especially kwenye malezi ya watoto na ndoa).
  you will make good money
  all the best
   
 5. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kama huko alikoomba wampe nafasi ya kazi kulingana na elimu yake alijieleza kama alivo andika hapa, huenda ndo sababu akaambiwa kuwa shahada yake haitambuliki. ukasuku kwenye kujieleza haulipi. Rudia tena kupanga maelezo yako.
   
 6. n

  nkisumuno JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa mwenye taarifa ya shirika lolote linalolipa mshahara mzuri au kampuni Mimi nina taaluma mbili 1. Ni mwalimu kada niliitumikia kwa muda mrefu na naendelea kufundisha shule za msingi. 2. Mimi ni Counselor nina shahada ya unasihi (Bachelor of couselling). Baada ya kumaliza masomo yangu ya shahada niliomba kubadilishiwa cheo lakini kutokana na ukiritimba wa nchi yetu nikaambiwa shahada yangu haitambulikani licha ya umuhimu wa taaluma hiyo kama nitakavyoeleza umuhimu wake hapa chini. Baada ya hapo nikaomba likizo bila malipo ili nifanye kazi na Kituo cha Afya kama mratibu wa UKIMWI nikakataliwa likizo. Hata hivyo nikaamua kufanya kazi kwa mkataba wa mwaka mmoja kwa muda fulani mwisho wa juma na kila baada ya kazi. Baadaye ya mkataba kwisha niliamua kuachana kutokana na kipato walichokuwa wananilipa. Katika Tanzania nimegundua kuwa ili upate kazi lazima uwe na mtu wa kukupigia debe bila kujali uwezo ulionao. Aidha uwezo wa viongozi wetu ni mdogo kutokana na sifa wanazoajiriwa kutokana na kufahamiana na nani baadala ya kuajiriwa kwa kuwa unajua nini. Nilipowambia nimemaliza shahada yangu nilijibiwa kuwa shahada yangu haitambulikani bila kuuliza nilichosoma kina faida gani katika jamii. UFUATAO NI BAADHI YA UMUHIMU WA UNASIHI (COUNSELLING) . Ni muhimu katika kutoa elimu ya malezi bora, Tuna mafisadi wengi kwa vile tu wana matatizo ya kisaikolojia kwa vile tu waliikosewa kulelewa kisaikolojia na kujikuta hawajiamini. kwa vile hawajiamini wanafikiri wakiwa na mali basi wataheshimika, wataonekana, kwa ufupi wanatafuta kujulikana na kulindwa na mali. Na ili mtoto ajiamini anatakiwa apate malezi bora kwa kufuata kanuni bora za kimalezi kisaikolojia akiwa na umri wa miaka 0-5 kisha miaka 5-12 Akikosewa hapo basi mtoto huyo hataweza kujiami. Na mtoto anayekosa kujiamini basi ataweza kushiriki katika matendo ya ulevi, umalaya na mambo mengi maovu akiongozwa na wale wenye tabia mbaya kwa kupelekeshwa. Kwa hiyo tabia mbaya kama kuvuta bangi, kuiba, rushwa n k ni matokeo ya jamii kuiga kwa vile tu hawajiamini. Muhimu hapa ni kuwapa nafasi wataalamu watoe elimu jinsi ya kulea watoto ili waweze kujiamini na kuwa na jamii bora. Leo hii waafrika wengi hawajiamini kwa vile tu Wazungu waliwaharibu waafrika wajione hawafai. Ni viongozi wachache katika Afrika wanaoweza kuamini kuwa maendeleo ya waafrika wanaweza kuleta maendeleo yao pasipokutegemea wazungu. Unasihi kwa ngazi ya shule utasaidia wale wanafunzi wasiojiamini waweze kujiamini pale wataalamu wa kisaikolojia (wanasihi ) watakaporejesha kujiamini kwa kuwajenga kisaikolojia waliopoteza kujiamini. Kuwasaidia wale waliopoteza wapendwa wao na kuathirika kisaikolojia, wanaoumwa magonjwa yanayosababisha wanyanyapaliwe. Familia wapate elimu kuhusu umuhimu wa kuvumiliana katika ndoa ili kulinda madhara yatakayowapata watoto endapo wataachana Kutoa elimu kuhusiana na matatizo ya kisaikolojia kama vile athari za msongo wa mawazo nakadhalika. Msongo wa mawazo una madhara makubwa katika kila sekta, mfano daktari mwenye msongo wa mawazo anaweza kumpa dozi isiyostahili mgonjwa na kusababisha madhara zaidi ikiwa ni pamoja na vifo. mwalimu anaweza kufundisha au akawa mkali kwa mwanafunzi kwa vile tu anamsongo wa mawazo. Anayefanya viwandani au kushughulika na mashine anaweza kuharibu vifaa au kuweza kupata ajali kwa kujikata na mashine kwa vile tu anamsongo wa mawazo. Hivyo ni vema ofisi ziwe na wanasihi kwa kila sekta ili watu wapate nafasi ya kupata msaada wa kisaikolojia ili kupunguza msongo wa mawazo. Zifuatazo ni baadhi ya dalili za msongo wa mawazo 1.kula sana au kupoteza hamu ya kula 2.kukosa usingizi au kulala usingizi sana 3.kupenda vitu vitamu kama vile pipi, biskuti, soda 4.kunywa pombe sana 5. Kupoteza hamu ya tendo la ndoa au hamu ya tendo la ndoa kuzidi 6. Kupoteza hamu ya kuwasiliana na ndugu au marafi (Kuwachukia) 7. Kujiskia mchovu bila sababu za msingi Hizo ni baadhi tu ya dalili za msongo wa mawazo. Ili kupunguza msongo wa mawazo (stress) fanya yafuatayo 1. Fanya mazoezi ya viungo kama kukimbia, kuendesha baiskeli nk 2. Punguza vyakula vya mafuta, kula mboga na matunda kwa wingi 3. Jithidi kuwa jirani na mtu unayempenda au kundi la watu baadala ya kuwa peke yako 4. kama kuna mnasihi jirani unayemfahamu mwombe ushauri 5. Fanya kitu unachokipenda kama vile kuangalia mpira, tv nk 6. Punguza kufanya kazi, uwe na muda wa kupumzika Nimejaribu kuonyesha kwa ufupi umuhimu wa Unasihi katika jamii ya kitanzania Nashukuru kwa ushauri ila ndugu yangu King jaribu kuwa na lugha nzuri, kwani kutoa hukumu kwa kosa moja ambalo hujui limetokana na nini si busara. Si kweli kwamba wewe uko perfect wakati wote nilidhani nimeweka vema post kumbe sijaweka aya. Sorry kwa usumbufu wanajamvi.
   
 7. Sema Chilo

  Sema Chilo JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 324
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  cheki ajira ktk website ya UNDP kuna ajira ya conc
   
 8. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,224
  Trophy Points: 280
  Dia 'kansela'
  hata paragraph hakuna......   
 9. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ....and your point is?
   
 10. c

  cielo Senior Member

  #10
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 2, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  dont be discouraged, one day God wil remember u
   
 11. Kilahunja

  Kilahunja JF-Expert Member

  #11
  Jul 17, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 1,497
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kama counceling yenyewe iko namna hii, unaongea mfululizo bila kumpumzika mpaka matee...ndo maana ukaambiwa hutambulika, weka koma, alama za mkato, aya n.k sio unaandika tu kama bata.
   
 12. S

  Stoudemire JF-Expert Member

  #12
  Jul 17, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 840
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Jifunze kwanza matumizi sahihi ya computer. Hivyo ulivyoandika kama unatuma application kwa barua pepe hawakupi kazi bandugu. Edit kwanza maandishi yako tukuone kweli unastahili ajira.
   
Loading...