Natafuta mwekezaji

kichichia

New Member
Oct 1, 2014
3
45
Habari,

Mimi ni kijana wa kitanzania, ninaishi DSM.. ninajishughulisha na kazi za usanidi wa mifumo ya kompyuta (computer programming).

Kampuni yangu mpya inaitwa sari technologies LTD.
Je, umeshawahi kusahau documents zako au mzigo wako wa muhimu sehemu..?

Je, umeshawahi kutaka kumtumia mtu mzigo ndani ya DSM kwa haraka na nafuu..?

Je, unafanya biashara zako mtandaoni, na unawaza ni namna gani utakuwa unafanya deliveries kwa wateja wako kwa haraka na nafuu..?

Je, umeshawahi kufanya manunuzi mtandaoni, na ukataka njia ya haraka ya wewe kupata bidhaa zako..?

Njia rahisi zilizopo ni kufanya mwenyewe au kutumia bodaboda ambazo ni gharama na pia sio salama, kwa baadhi ya mizigo kama simu na vyakula..

Tumetengeneza programu ya simu ambayo itawewezesha watu binafsi pamoja na wafanyabiashara kuweza kuagiza na kutuma mizigo kwa urahisi, nafuu na salama.

— watu hawahitaji tena kusuburi muda mrefu kutuma au kupokea mizigo, ndani ya lisaa limoja utapata mzigo wako
— ni nafuu sana, gharama zetu ni hadi sh 3000 kwa umbali mrefu
— ni rahisi hauhitaji kutembea wewe mwenyewe kufata au kutuma mzigo
— ni salama hauhitaji kutumia bodaboda wasio haminika

Mfumo huu unafanya kazi kama uber lakini ni kwaajili ya mizigo (parcels).
1. Login kwenye app
2. Request a delivery (kama vile unarequest a ride from uber)
3. Utaweka mahali ambapo mzigo ufuatwe (pick-up point) na namba za simu
4. Utaweka mahali mzigo unaenda (delivery point) na namba za simu
5. Mfumo utakuonyesha gharama za huduma
6. Halafu utatuma request yako

Natafuta mwekezaji atakae saidia kataka gharama za uendeshaji kampuni na masoko, kiwango cha kuwekeza na faida ni makubaliano

Tuwasiliane: +255 788 826982
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom