Natafuta mwanaume wa kuzaa nae

Natafuta mwanaume wa kuzaa nae

Ushauri wa bure,
Kama unalea mwenyewe mtoto then ongeza vigezo, lengo upate mtoto mwenye afya, inteligent, good speaker na good behaviour.
Hii itakusaidia katika maliza ya mtoto wako na future yake inaweza kuwa bright kwa kuzingatia selection ya baba utakayepata.
Huko mamtoni watu wananunua sperm za macelebrity, maprofessor, maCEO, n.k
If your capable follow this root and you'll thank me later.
 
Marejesho hadi mda huu ana watoto wawili na mimba nyingine ina miezi miwili😂😂😂
 
Yaan sasa hivi utakua na watoto wengi sana kwa hizo kilometres ulizotembea naona huko kutakua na mfululizo wa mapacha mwendo wa gusa achia twende kwao
 
Natafuta mwanaume wa kuzaa nae ila kuoana hapana, awe tayari kupima HIV!

Nikizaa nitalea mwenyewe, na yeye atabaki kuwa baba mtoto na mzazi mwenzangu ila ngono baada ya kuzaa hapana.

Awe sura nzuri, mrefu.
Wanawake wa aina hii (PILIPILI) unaweza ukafikiri hawapo! Ila kiukweli wapo kwenye jamii yetu. Na mara nyingi mpaka wanafikia hatua hii, sababu zifuatazo husababisha;

1. Ubinafsi uliopitiliza (egoism). Mara nyingi wanawake wa aina hii hujali zaidi hisia zao kuliko za watu wengine. Hujiangalia wao zaidi wenyewe na si mtu mwingine.

2. Huwa ni viumbe wenye dharau na kiburi kilichopitiliza. Wakati mwingine unaweza ukamkuta mwanamke wa aina hii hana mbele wala nyuma, ila kwa sababu tu ya kusifiwa kuwa na uzuri wa sura au umbo; dharau na kiburi humjaa na hivyo kutamani maisha ya peke yake/maisha ya uhuru/maisha ya kujiachia. Nwanamke mwenye dharau na kiburi hawezi kuishi maisha ya ndoa, na yanayomtaka kumtii mwanaume.

3. Ukosefu wa makuzi ya malezi ya wazazi wote wawili (baba na mama), au athari za kisaikolojia alizozipata utotoni kwa kukosa malezi ya wazazi wake wawili, na hivyo kulelewa na mama pekee. Wanawake wa aina hii kamwe hawawezi kuona faida ya kuishi maisha ya ndoa, au ya familia. Kwa sababu yeye kama yeye hajawahi kuyafurahia kupitia wazazi wake.

4. Tamaa iliyopitiliza. Wanawake wa aina hii hupenda kuishi maisha ya uhuru kwa sababu siku zote huwa na ndoto za kuwa na mahusiano na wanaume matajiri wa kuwatimizia mahitaji yao.

5. Utandawazi. Mara nyingi wanawake wa aina hii, hushinda kwenye mitandao na hivyo kujikuta wanajifunza tamaduni mpya na ambazo hazijazoeleka kwenye jamii yetu.

NB: Wanawake wa aina hii mara nyingi huangukia kwenye mahusiano mabaya, na yanayo waathiri wao wenyewe kisaikolojia na kimwili, lakini pia mahusiano hayo huwaathiri pia watoto wao kwa namna moja au nyingine. Maana yake na watoto nao watarithi tabia zile zile za kutothamini maisha ya familia.

Ushauri kwa wanawake wote;
1. Jitahidi kutambua thamani ya kuwa na familia hapa duniani.
2. Punguzeni ubinafsi, kiburi, dharau, na kujidanganya. Kuweni wanyenyekevu, kwa sababu maisha ya familia ni bora sana kuliko maisha ya usingle mother.
3. Punguzeni tamaa na kupenda kushawishiwa kirahisi na maisha ya kwenye mitandao. Ridhikeni na kile kidogo mnachopata kutoka kwa waume zenu.
4. Jengeni maisha yenu tofauti kabisa na yale ya wazazi wenu. Yaani kama ulikosa malezi ya wazazi wako wote wawili kwa sababu ya ubinafsi wao, kamwe usikubali na watoto wako nao waishi maisha ya aina hiyo hiyo.

Mwisho kabisaaa, wanaume tufahamu siyo kila mwanamke ni wa kuoa. Wengine ndiyo kama hawa! Wanawake wa aina hii hata uwafanyie nini, watakuumiza tu. Kwa sababu lengo lao kuu ni kutaka kuishi maisha ya uhuru, na kujiachia. Wanawake wa aina hii ni vyema wakaachwa waishi maisha yao waliyo jichagulia. Ukilazimisha umuoe/uwe naye kwenye mahusiano, aisee hakuna rangi ya maumivu ya mapenzi ataacha kukuonesha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom