Natafuta mume tuoane

Mwanamke hawezi kuoa bali huokewa. Sasa huko kuoa unakosema ina maana yeye mwanaume akimaliza kukuoa na wewe unamwoa??
Kama ulienda shule basi rudi tena ukarisiti!!!

Inaelekea ulizungusha kama Bashite. Hata kiswahili tu kinakushinda!!
 
Hongera kwa kutafuta Mme wa kukuoa. Ila Binafsi na swali... Yule alie zaaa nae huyo mtoto mmeshindana nn mpaka asikuoe yeye!
 
Salama wakuu wa love connect.

Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 37, nina mtoto mmoja wa mwaka mmoja, baba yake tuliachana ila hatukuwahi kuishi pamoja, nimeajiriwa serikalini, nina elimu ya masters.

Umbo langu ni mnene kiasi, maji ya kunde, dini mkristo mkatoliki, ninaishi dar.

Natafuta mume wa kufunga nae ndoa na kumaliza nae muda wa kuishi duaniani; awe mwenye umri kuanzia miaka 37, Mwenye elimu kuanzia chuo kikuu, asiwe mnene, rangi yoyote, mwajiriwa ama mtafutaji, anayejua umuhimu wa maisha na ndoa, mwenye kumpenda mke na atakayemkubali na kumpenda mwanangu, awe mkristo wa dhehebu lolote isipokuwa msabato.

Nitampenda kwa moyo wangu wote na kuwa mwaminifu kwake.

Kwa anayekubali vigezo anakaribishwa PM tafadhali.
daaah nina 36 net. plz nisubiri mwaka mmoja miaka itimie vigezi vingine ninavyo umri tu ndy bado mwaka mmoja
 
Miaka 37 mmmmh utazaa watoto wangapi kabla uzazi haujaisha? Mmmh nasita kukuoa aisee.....
 
Samehe ujinga wangu, lakini miaka 37 single mother, kuolewa kazi ipo. Labda upate baba aliyetalikiwa au kufiwa na mke, maana ni kweli wapo, lakini nitakushauri sana chukua muda wa kutosha kutafakari watu hao wana changamoto zao. Kitu pekee kinachoshinda yote haya ni upendo. Nakutakia heri.
 
Nawaambia kuna changamoto zaidi kuishi na mwanamke mwenye mtoto wa mwanaume mwingine. Tena kasema mtoto ni mdogo, mwaka mmoja! Hii mada naweza kuandikia hata insha ya kurasa 100!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom