Natafuta mtu wakunipa hifadhi ya Siku 3 Mtwara

Kwa akili hizi tusitegemee vijana critical kwa Sasa. Kwa nn mnapenda mteremko? Msaada una gharama zake Mdogo wangu. 2004 NIliwahi kwenda interview Mtwara nikiwa na 50,000/= tu nikalala Guest 5,000/= . Japo Hapo Nina ndugu wengi tu

Muongo 2004 hela ya Mkapa ilikuwa na thamani kubwa sana na bado sehemu nyingi za miji ya Tanzania hakujakuwa na guest houses za ku-cost 5,000/= per day na kwa Mtwara na-assume ulilipa ukakaa zaidi ya week kwa hiyo hiyo 5,000/=,wewe mbona unapendaga kuwa muongo muongo sana?

Dar kipindi hiko ndo ujana wangu unachanganya guest nimeingia sana sijawahi kulipa zaidi ya 3,000/= tena nyumba classic hizo za uchochoroni zilikuwa 1,500/= au 2,000/= 5,000/= ilikuwa ni kwa hotel za Kariakoo ikizidi sana 6/7,000/= leo useme Mtwara guest 2004 zilikuwa 5K unadhani upo na wanao humu unawadanganya siyo?
 
Nipo Mtwara Nina mwezi sasa, nilikuwa mgeni Kama wewe, usihofu, Ukifika shuka pale stendi mpya panaitwa mkanaledi.
Mimi naishi Shaghani ni karibu na stendi hiyo nitakupa hifadhi Nimepangishiwa nyumba nzima na ofisi utakula utalala dada wa kazi yupo. Unaweza kunipm.
Shangani ni karibu na Mkanaledi mkuu? Wacha kupotosha watu.
 
Option nyingine tofauti ambayo pia itaondoa hizo doubts ni kuomba angalau mwenye nacho amchangie ili apate kiasi cha yeye kuweza kwenda kulala guest na kupata mahitaji ya msingi ili akamilishe hiyo interview.
Na kulala guest pia kutaweza kumpa muda mzuri wa maandalizi kwani atakuwa huru kuliko ugenini

Ova.....

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu nashukuru kwa hili wazo lako pia lakini nimeshapata mwenyeji wangu humu ivo Ntafikia kwake hakuna shida.
 
Hello wana Jamvi nilikuwa naomba hifadhi ya kulala Hapo Mtwara kwa muda wa siku tatu, Ninakuja huko kwa ajili ya interview Vitu kama chakula ntajitegemea au kama patakuwa na utaratibu wa kupika pia ntachangia. Nina documents zote ambazo zitakutoa shaka kabisa na ukao wangu hapo kwako wasiwasi ni akili hivyo nitajitahdi kukuonesha proof zote kuwa mimi mgeni salama.

Interview inafanyikia Bandari sekondari na Employer ni TANESCO , Sijawahi kufika Mtwara naomba pia anayejua gharama za Guest hapo zikoje anijuze ili option namba moja iki fail ni opt hio ya pili.

Asanteni sana.

Jinsia yangu ni ya kiume.

Age 25
Bei ni ndogo kuanzia 10000 hadi 25000 zipo
 
Vijana mnaochipukia aisee mna mambo ya ajabu Sana. Yaani mtu ukutane nae tu JF ukalale kwake, seriously?
Mkuu ujazunguka kutafuta life hii issu kwa kwetu ni jambo la kawaida mnapiga ghetho acheni uwoga mkaribisheni mwenetu kaja kujaribu alafu ukiona jambo uliwezi usipende kukatisha watu tamaa nina imani na watu wa kusini watamsaidia mdau!sio kama watu wa dar ukiwambi nakuja nataka ata member fulani tufanye biashara atakukimbia mkuu msipende kukatisha watu tamaa
 
Nipo Mtwara Nina mwezi sasa, nilikuwa mgeni Kama wewe, usihofu, Ukifika shuka pale stendi mpya panaitwa mkanaledi.
Mimi naishi Shaghani ni karibu na stendi hiyo nitakupa hifadhi Nimepangishiwa nyumba nzima na ofisi utakula utalala dada wa kazi yupo. Unaweza kunipm.
Nimekukubari mzee baba huo ndio ujasiri wa kiume tena mpambanaji sio hawa watoto wa mama wanabaki kumzihaki mtu!ujui mtu ana hali gani kipesa mpaka aombe msaada JF ina watu wengine wa ovyo sana
 
Jamaa anahitaji kulala, siyo kusafiri. Stand ya mabasi ya nini? Unataka akalale stand ya mabasi?
Msaidieni sambamba na ombi lake kama mnaweza. Vinginvyo mwelekezeni guest house/ lodge za bei nafuu.
Ameshapata,tunashukuru,,wazo langu kweli lilikuwa extrem,, desperate situation need desperate measure
 
Wakazi wa Mtwara chukueni tahadhari, ripotini mtu yeyote mnaye mtilia shaka, mtoa mada uje kuripoti polisi utapewa msaada. Ikitokea umepokea mhalifu utajuta kuzaliwa.
Ahsante
Badilisha pombe asee,hiyo imekushinda
 
Nipo Mtwara Nina mwezi sasa, nilikuwa mgeni Kama wewe, usihofu, Ukifika shuka pale stendi mpya panaitwa mkanaledi.
Mimi naishi Shaghani ni karibu na stendi hiyo nitakupa hifadhi Nimepangishiwa nyumba nzima na ofisi utakula utalala dada wa kazi yupo. Unaweza kunipm.
Shangani na mkanaledi ni mbali kiongozi japo panafikika kwa urahisi makadirio ni km 2 na kuendelea inategemea anapitia wapi mnarani, kupitia kwa jonee au bima au hata kule Paris au sasa steramarise. Umefanya utu kiongozi kheri iwe nawe
 
Kama wewe ni mgeni Mtwara hujui kinacho endelea, kaa kimya
Bouy ni kweli ila zile misheni za kapigado huko kwa mzee malando na mwanetu alieomba hifadhi sidhani kama zinauwiano, japo unaambiwa muone adui kabla hajakuona.
Yeye mwenyewe ameshasema kua atatoa ushahidi wa vielelezo ili aaminike. Janja nicheki pm nikuunge kwa mchungaji wa Kanisa langu pale koko beach ukaangushie.
 
Shangani na mkanaledi ni mbali kiongozi japo panafikika kwa urahisi makadirio ni km 2 na kuendelea inategemea anapitia wapi mnarani, kupitia kwa jonee au bima au hata kule Paris au sasa steramarise. Umefanya utu kiongozi kheri iwe nawe
Km 2 mbali we chalii acha uswahili basi au una junsia ke ila kama me km 2 nazani ni mwendo wa dk 20 kinyonge hapo
 
Km 2 mbali we chalii acha uswahili basi au una junsia ke ila kama me km 2 nazani ni mwendo wa dk 20 kinyonge hapo
Nimeweka makadirio kiongozi ila kipande cha mkanaledi shangani ni parefu na ikumbukwe shangani ziko mbili East na West . Asante kiongozi kwa maneno yako nimeyapenda wala hayaniumizi ila nikikuonesha uwezo wangu wa kutembea unaweza jiuliza mengi sana. Chezea zile route za mabio ya kujitegemea na mengine tuyaache tu. Ila umenijaza nyembe ungekua nakufahamu . Ningestaafishwa kesho wallah
 
Guest ni kuanzia 7k unalala zipo zimejazana tu.Kama unataka guest ukifika mtwara chukua bodaboda halafu muelekeze akupeleke guest za hiyo bei atakupeleka but muambie iwe maeneo ya town itakuwa rahisi kwenda hapo bandari secondary.Halafu chakula usihofu mtwara chakula bei chee buku unakula unashiba bajeti ikibana unakula hata mihogo

Sent from my Infinix X623 using JamiiForums mobile app
JERO anashiba Mtwara. Anaweza piga ming'oko na UPUPU.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom