Natafuta mtu wakunipa hifadhi ya Siku 3 Mtwara

Vijana mnaochipukia aisee mna mambo ya ajabu Sana. Yaani mtu ukutane nae tu JF ukalale kwake, seriously?
Acha hizo mkuu watu wamepokelewa na watu hata hawajuani na wakakaa nao mpaka mambo yakakaa sawa hakuna tozo wala nn?. Angekuwa anakuja mtaa niliopo ningemsaidia mpaka hela ya kula kwenye usaili wake
 
Pengine hujawahi kupitia changamoto mkuu

Ungekuwa ni jinsia ile ya upande wa pili, nina uhakika wadau wangepigana vikumbo humu kukupa hifadhi! Hakuna namna. Ikitokea ukapata wa kukupa hifadhi ni jambo la kumshukuru Mungu.

Ukikosa, wewe nenda tu mpaka eneo la tukio, na akili itapatikana huko huko. Unaweza ukakuta kuna mtu mwingine atakayefanyiwa hiyo interview naye akawa na shida kama yako,hivyo mkajikuta mnachukua chumba kimoja na mambo yakaenda vizuri tu kwenye bajeti zenu.
 
Gharama ni za kawaida kulingana na sehemu zipo Hadi guest za buku Sita Ila huko kunguni ni kawaida
Standard ni elf 30 Hadi 50 kwa Lodge
Kama una nguvu karibu Naf Beach Hotel hapo kulala si chini ya laki moja
 
Mtwara guest zipo bei tofauti kuanzia elf8 unapata sehemu nzuri ya kulala, mm naish mtwara but now nipo nje ya mtwara kwa siku 4, gheto nimefunga
 
Omba mchango wa Lodge utakua salama zaidi. Tunapenda kijana uwe salama na upate kazi ya kusoma MITA ila usijirahisi kulala kwa mtu usiyemjua Zama hizi za Magonjwa mengi
 
Hello wana Jamvi nilikuwa naomba hifadhi ya kulala Hapo Mtwara kwa muda wa siku tatu, Ninakuja huko kwa ajili ya interview Vitu kama chakula ntajitegemea au kama patakuwa na utaratibu wa kupika pia ntachangia. Nina documents zote ambazo zitakutoa shaka kabisa na ukao wangu hapo kwako wasiwasi ni akili hivyo nitajitahdi kukuonesha proof zote kuwa mimi mgeni salama.

Interview inafanyikia Bandari sekondari na Employer ni TANESCO , Sijawahi kufika Mtwara naomba pia anayejua gharama za Guest hapo zikoje anijuze ili option namba moja iki fail ni opt hio ya pili.

Asanteni sana.

Jinsia yangu ni ya kiume.

Age 25
Wasomi wetu bana wa siku hizi,yaani umekosa hadi shilingi elfu kumi ya kulipia guest then unataka kufikia kwa mtu wa jamii forum?kwa akili hizi nakushauri hata kwenye hiyo interview usiende maana una vyeti tu Ila kichwani upo mweupe
 
Nipo Mtwara Nina mwezi sasa, nilikuwa mgeni Kama wewe, usihofu, Ukifika shuka pale stendi mpya panaitwa mkanaledi.
Mimi naishi Shaghani ni karibu na stendi hiyo nitakupa hifadhi Nimepangishiwa nyumba nzima na ofisi utakula utalala dada wa kazi yupo. Unaweza kunipm.
Aisee. Nikija mkuu nita ku pm. Mchakato majimboni utakapoanza. Naomba nafasi ibakie mkuu. Mambo ya kufikia Naf apartment ni ya kwepe. Prokal nyingi.
 
Aisee. Nikija mkuu nita ku pm. Mchakato majimboni utakapoanza. Naomba nafasi ibakie mkuu. Mambo ya kufikia Naf apartment ni ya kwepe. Prokal nyingi.
Wewe Kama unafanya seminar pale NAF hotel Ina maana unakula perdiem Nzuri, Sasa na huyu bwana mdogo ndiyo anaanza maisha. Mbona unajishusha Mkuu?
 
Hello wana Jamvi nilikuwa naomba hifadhi ya kulala Hapo Mtwara kwa muda wa siku tatu, Ninakuja huko kwa ajili ya interview Vitu kama chakula ntajitegemea au kama patakuwa na utaratibu wa kupika pia ntachangia. Nina documents zote ambazo zitakutoa shaka kabisa na ukao wangu hapo kwako wasiwasi ni akili hivyo nitajitahdi kukuonesha proof zote kuwa mimi mgeni salama.

Interview inafanyikia Bandari sekondari na Employer ni TANESCO , Sijawahi kufika Mtwara naomba pia anayejua gharama za Guest hapo zikoje anijuze ili option namba moja iki fail ni opt hio ya pili.

Asanteni sana.

Jinsia yangu ni ya kiume.

Age 25
Option nyingine tofauti ambayo pia itaondoa hizo doubts ni kuomba angalau mwenye nacho amchangie ili apate kiasi cha yeye kuweza kwenda kulala guest na kupata mahitaji ya msingi ili akamilishe hiyo interview.
Na kulala guest pia kutaweza kumpa muda mzuri wa maandalizi kwani atakuwa huru kuliko ugenini

Ova.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi mtwara hakuna stand ya mabasi?
Jamaa anahitaji kulala, siyo kusafiri. Stand ya mabasi ya nini? Unataka akalale stand ya mabasi?
Msaidieni sambamba na ombi lake kama mnaweza. Vinginvyo mwelekezeni guest house/ lodge za bei nafuu.
 
nenda Masandube pale utapata hifadhi saaafi hadi unamaliza shughuli zako Ntwara
 
Pamoja sana mzee,all the best.He is a good person so dont worry.I know him nje ya JF.Uandae tu buku la bodaboda from hiyo mitaa ya Ligula hosp mpaka Bandari.Muda wakurudi unaweza piga ado ado ili uuone mji.

Sent from my Infinix X623 using JamiiForums mobile app
Nashukuru sana mkuu na Nimeshawasiliana nae mchana ivo mambo yako sawa

undugu kufaana na sio kufanana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom