Natafuta mtu wa Kuniloga.

Wakuu,

Nina miaka 4 sasa nafanya utafiti kuhusu kuwepo kwa uchawi sijapata kujiridhisha kihalisia kuwepo kwa ushirikina.
Uchawi ni nini katika utafiti wako/wenu? Ushirikina na uchawi ni kitu kimoja? Mazingaombwe ni nini? Hii ni muhimu sana kwa maana si rahisi kuweza kutafuta kitu ambacho hukifahamu.
 
me kuna siku nilikuwa kijiweni na wazee alafu nikaropoka me sirogeki! wale wazee wakaniuliza unasemaje kijana! nikajibu hapana natania tu!
 

Wamekudharau wala hawatakudhuru,ukitaka sema unataka kununua uchawi tena tangaza dau kubwa uone watakavyokuletea kila mmoja akijisifu wake ndiyo mkali tena watakujaribia kama siyo kwako kwa mwenzio unajua hii ni secret society fulani hivi sawa na freemason au haloween hawapendi kujionesha pasipo maslahi. hata biblia inatambua kuwa uchawi upo ila unadhbitiwa kwa jina la Yesu,wenzetu wengine kwao ni sehemu ya dini.unaweza kuletewa hata kwa njia ya meseji au hata kwa mawasiliano ya simu ila endelea na utafiti wako iko siku utauona
 
Kwa post hii,kweli umerogwa!
 
Mbona tayari usharogwa na aliyekuloga humjui,

Matokeo ya kulogwa huko ni haya unayoyaongea hapa na juzi ulisema tukukutanoshe na mwenye jamhuri kwakuwa unafanana nae tu, kibaya zaidi mchawi aliyekuloga kakupiga jabulani ya kutosha yani una miaka 28 na tayari una watoto 6, ukifika miaka 40 sijui utakuwa na sakosi ya aina gani.

Huo ndio uchawi, hakuna kingine
 
unaamini uwepo wa miujiza ,lakini huamini uwepo wa uchawi....majanga

unaamini mungu yuou na anabariki lakini huamini kama kuna uchawi ambaye huyo anayekubariki anatambua na kuukiri upo...majanga

Wakuu,

Nina miaka 4 sasa nafanya utafiti kuhusu kuwepo kwa uchawi sijapata kujiridhisha kihalisia kuwepo kwa ushirikina.
Kama kuna mtu amelogwa au anaweza kuniloga atoe fact hapa.
kazi ipo....
 

Naamini NGULI atakuja kukujibu ila naomba kuchangia tu kuwa huyo padri niliyemzungumzia hapo juu, alikwenda kwa waganga wengi(majina aliyataja) wengine unawafahamu. Hata yule mchawi alitaka kuomba kibari cha kuruka na ungo alionananaye, na kote alikokwenda, alikwenda eidha kama mteja wa uchawi au kama mgojwa lakini aliishia kusema yote ni sanaa na mazingaombwe.
 

Sikutemea hii judgement kutoka kwako. i thought your thinking capacity is beyond this.....
 
unaamini uwepo wa miujiza ,lakini huamini uwepo wa uchawi....majanga


unaamini mungu yuou na anabariki lakini huamini kama kuna uchawi ambaye huyo anayekubariki anatambua na kuukiri upo...majanga


kazi ipo....

Hapo kuna mchanganyiko. Naungana na wewe, ume-spot kitu cha msingi.
Ngoja tumsubiri NGULI mwenyewe.
 
Mi naona ungeanza kujitafiti kwamba kwa nini katika umri mdogo huo una watoto 6? Nadhani hapo ndo umelogwa kwa vile umeshindwa kujitambua.
 
Naomba unipe jina lako na la mama yako liwe kamili.
Halafu niambie unataka nikuroge uweje
1.Ufe kabisa?
2. Uwe kichaa?
3.Uwe fukara maisha yote?
4.Uwe shoga?
 
Sitosahau siku moja nikiwa mkoa flani ambao sitoweza kutaja jina nikiwa nimerudi toka kwenye mihangaiko yangu usiku nikalala usiku nilila na bukta ndani nikiwa na boxer nilistuka usiku wa saa tisa na kujikuta nipo uchi chini ya uvungu nilinyanyuka nakuangalia mlango umefungwa vilevile alafu bado unaniambia uchawi haupo hapana mkuu mimi nakataa.
 
Nitajitolea kufanya kazi yako; nitahitaji vitu vifuatavyo ili kufanikisha zoezi langu.

1. Nitahitaji kupata Tambiko (Zindiko) lako la ukoo, kama hulijui basi nitatumia utaratibu wa kukupisha huku kiganja chako
cha mkono wa kulia kikiwa kimekandamiza pembe la kiapo.

2. Nitahitaji kuchukua moja ya vifuatavyo: Unyayo, Unyewe wa utosini, kucha au kope

Hivi vitu ndiyo vinatakiwa kufanikisha zoezi la kukugeuza uwe ndondocha!!

Vitu vingine ambavyo wewe havikuhusu - nitahitaji kupata:

1. Sanda iliyotumika kumzikia mtoto mchanga.
2. Kipande cha mbao kilichongolewa kutoka kwenye kitanda kinachotumika kubebea maiti
3. Bundi mweusi - Hasa kama mizimu yako ni mikorofi kukuachia
4. Maji ya baharini kama utaamua kuishi baharini au maji ya mtoni kama pia utapenda kuishi huko - hapa ni chaguo lako

Note: Huu uchawi ni wa Bara (Ndagu)- Pwani wao wanatumia Majini.

Upo tayari.....
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…