Natafuta mtaalam wa kunisaidia kupata ajira na kuniondolea gundu

mimi mtakatifu

JF-Expert Member
Oct 11, 2019
207
482
Kama heading inavyojieleza bado naangaika kusaka ajira. Kuna siku niweka uzi nikaukimbia watu wana maneno makali sana unaweza jiona hufai tena.

Sijachanganyikiwa kama wengine wanavyoamini mimi nipo timamu kabisa.

Kuna wakati nilizunguka uko kwa wataalam sikufanikiwa sababu naona ilikuwa uwezo wao nikakata tamaa ila nimeamua nirudi tena sina options.

Najua kuna watu wamevuka stage ya utoto wanayaelewa vizuri maisha na watanielewa kinachonisumbua

Natafuta mtaalam wa jadi mzuri ataeweza nisaidia kupata kazi na kuniondolea gundu.

Maana kwa sasa kila nachojaribu kufanya kinaishia kuharibika naomba kazi miaka 3+ natoswa siku hizi sipati hata simu ya interview nna mwaka sasa.

Ningefurahi zaidi angekuwa Dar maana pia nauli ya kwenda mbali na DSM ni changamoto kwangu ila kama anakuwa mbali sio mbaya nitapambana nimfate.

Nasubiri msaada PM.

Mtaonitukana nimewasamehe in advance.
 
Mkuu pole sana na masahibu yote unayopitia. Sijui kama utaupenda ushauri wangu, ila acha nikuambie kitu.

Waganga utapoteza pesa, kuendelea kujiwekea nuksi. Nachokushauri kwa Imani yako, mrudie Mungu omba toba/msamaha kwa kuamini binadamu, ndiye anayeweza kukutatulia shida zako.

Baada ya hapo mwamini yeye, kama ameweza kukuumba hashindwi jambo dogo kama kukupatia kazi na kutoa hiyo mikosi unayohisi.

Hayo ni mapito na majaribu ya dunia, kila mtu anapitia kwa aina yake. Mwisho wa siku Imani yako itakuokoa.
 
*Kuna kitu nitakutumia pm ufanye, utaleta mrejesho...
Ushauri wako ni mzuri sana dada ila umeutoa kipindi kibaya mno hapa nilipo ni kama homeless nahitaji kula kuwa na sehemu yaekulala na mahitaji mengine ya lazima mimi naweza vumilia ila hivi vitu vimeshindwa kunivumilia. Napoelekea nitaokota makopo
 
Mkuu pole sana na masahibu yote unayopitia. Sijui kama utaupenda ushauri wangu, ila acha nikuambie kitu.
Waganga utapoteza pesa, kuendelea kujiwekea nuksi. Nachokushauri kwa Imani yako, mrudie Mungu omba toba/msamaha kwa kuamini binadamu, ndiye anayeweza kukutatulia shida zako.

Baada ya hapo mwamini yeye, kama ameweza kukuumba hashindwi jambo dogo kama kukupatia kazi na kutoa hiyo mikosi unayohisi.
Hayo ni mapito na majaribu ya dunia, kila mtu anapitia kwa aina yake. Mwisho wa siku Imani yako itakuokoa.

*Kuna kitu nitakutumia pm ufanye, utaleta mrejesho...
Msizungumzie vitu msivyo na uhakika navyo.Kama unamshauri mshauri, Waganga wapo na wanasaidia kama akimpata wa kweli.Yeye mpaka katafuta mganga si kichaa kama alivyosema.Hata wachungaji wapigaji wapo pia.Kuna wakati muwe mnatoa ushauri kwa mujibu wa uhitaji wa mtu.Mtu kitu kama hukijui si wakiacha tu.
 
Bora umenisaidia mkuu. Unakuta huyo mtu hajawai hata kulala njaa ila anahisi anaelewa vizuri mapito yako.
 
Unajua watu wanalazisha uwaze wanavyotaka wao, mganga hawi mchawi au kudhuru mtu.Na kila mahali pana watu wema na wabaya hata katika familia zetu.Sasa waganga wachache waharibifu waharibu fani nzima ya uganga?Si sawa hii.Uganga ulikuwepo upo na utaendelea kuwepo.UGANGA SI TUNGULI PEKE YAKE.
 
Back
Top Bottom