Natafuta msichana mkweli tuwe wachumba

Mr Kind

Senior Member
Mar 4, 2017
178
308
Natumai mko poa wanajukwaa hili.
Najitokeza kwenu leo kwa lengo moja tu la kutafuta mschana ambaye yuko tayari tuwe wachumba na hatimaye tufikie lengo la kuanzisha na kujenga familia.

Nahitaji mschana mwenye umri kuanzia miaka 20 hadi 28 aliye tayari kuolewa, anayeishi Morogoro itakuwa nzuri zaidi kurahisisha mawasiliano. Kwa aliye nje ya Morogoro awe tayari kusafiri.
(Vigezo vingine tutajuana vizuri baada ya kukutana face to face)

Mimi ni kijana mwenye miaka 30, kwa sasa naishi Morogoro mjini, ni mwajiliwa, Mkristo wa dhehebu la Catholic, urefu wangu ni wa wastani, si mweusi wala mweupe (katikati) na niko kawaida.

Muhimu : Wapenzi hukutana popote, mtaani, kijijini, kwenye vyombo vya usafiri, mashuleni /vyuoni, ofisini, nyumba za ibada, na hata kwenye jukwaa kama hili.

Familia bora na yenye amani haijengwi katika misingi ya mahali mlipokutania mwanzo! Kuna walio kutania kwenye nyumba za ibada leo familia zao hazina amani, Kuna walio oana kwa kigezo cha ukaribu wa familia zao lakini leo nao hawana amani, lakini wapo waliojuana kupitia majukwaa kama haya au vilabu vya mziki na hata baa na wamejenga familia bora na wanaishi kwa amani tele!

Ubora wa familia hutokana na maelewano mazuri kati ya wanaoamua kuianzisha bila kujali wamekutana sehemu gani

Mschana aliye tayari, karibu inbox /Pm. Tafadhali, usiweke namba ya simu hapa kwenye public kuepuka usumbufu.

Karibu sana!
 
Back
Top Bottom