Umekuwa mzungu wa kuoa mwanamke aliyekuzidi umri?
Yaani unapenda u-ben10 kwenye maisha halisi ya ndoa?
Mzidi umri mkeo kuanzia miaka10 hadi ishirini, hapo maisha yenu yataenda pamoja hadi uzeeni.
Unapooa mwanamke anakuzidi, let say miaka3 ama zaidi, kama bandiko lako, inamaana mtakapofikisha miaka20 ya ndoa, mkeo atakuwa tayari alishaingia kwenye "menopause" na atakuwa 'hakuhitaji' tena.
Sasa kwa umri wako huo wa miaka 45 damu bado inachemka utaingia mtaani kusaka 'jiko'?
Tunavyoshauri kumzidi miaka mingi mkeo, ili atakapofikia kuchoka kibaiolojia, nawe utakuwa tayari kambabu ulishapinda mgongo, unatembelea mkongojo'uko na hautaki tena "mambo'ayo", mnabaki tu kumalizia maisha yenu kirafiki bila mgogoro.