Natafuta mganga wa jadi

Natafuta mganga wa jadi

posho

Member
Joined
Mar 15, 2014
Posts
9
Reaction score
4
Sabalkheri Mabibi na Mabwana wa Jamiiforums.
Nimekuwa msomaji wa tovuti hii kwa kiasi cha muda na sasa nimeonelea vyema kujiunga nanyi.
Natafuta mganga mzuri wa jadi awezae kazi na sio mwenye maneno matupu, najua humu wapo watu kadha wa kadha waliowahi pata mitihani ya maisha na kwenda kuongea na mizimu na kupata ufumbuzi wa jambo husika.
Mimi ni mjasiriamali na napatikana morogoro na kusafiri naweza.
Kwa yoyote alie na mawasiliano na mganga mzuri tafadhali nitumie mawasiliano yake kwa PM. ukinisaidia na nikapata ufumbuzi nitakupatia zawadi.
Ni hayo tu kwa leo.
 
nenda magogoni (white house) utawakuta mpaka wa Nigeria
 
omba tu kwa mungu wako kaka utashinda
 
Unaamini Mwanadamu ndo anaweza kukusaidia kuliko Mungu wako....!
 
hiyo salamu tu aliyoanza nayo kwenye post ake nshajua dini yake huwa wanaamini sn hizo mambo watu wa dini hiyo kuliko hata kufanya kazi.Ukikwama kabisa mtafte MZIZI MKAVU manake ye anajua tiba ya kila tatizo
 
unaweza kufikia Roho ya mtu aliyekufa, Roho ya kiumbe mbinguni kuzimu kwa kupitia Mganga "mwanadamu". Tukienda huko tunaamini mwisho na si njia.
 
MUNGU ndie kila kitu ndie aliyekuumba , anawaangazia jua wabaya na wema anawapa usingizi maskini na tajiri ,ametupa usiku na mchana kwa weupe na weusi mtegemee mungu ukiomba kwa imani utapata unachotaka.
 
amtegemeaye mwanadamu amelaaniwa mwamini Mungu tu hata ungenda Nigeria utafanikiwa kwa mda kidogo halafu majanga bure Mungu ndo kila kitu
 
hiyo salamu tu aliyoanza nayo kwenye post ake nshajua dini yake huwa wanaamini sn hizo mambo watu wa dini hiyo kuliko hata kufanya kazi.Ukikwama kabisa mtafte MZIZI MKAVU manake ye anajua tiba ya kila tatizo

na waganga anaowaulizia woote ni wa mrengo huo.
 
Tembea along Morogoro road utakuta vibao vingi sana
 
Kila mtu ana haki ya kuamini kile ambacho anaona sahihi kwake...who are you to judge him? Nyie ni wasafi kiasi gani hadi mhukumu mapema hivi?

Mungu ametoa vipawa kwa watu wake ili watibie wwnzao kupitia mitishamba n.k ndugu ameona atapata msaada huko then mwacheni akapate salama yake. Kwani inaaminika imani yako tu ndo itakuponya, hivyo imani yako iko kwa sangoma. Mwacheni aende.

Mungu akujalie upone kupitia tiba za asili ndugu.

Kila la kheri!!
 
1187261_159020260968517_1673611614_n.jpg
 
Yesu Kristo ndiye mgamga pekee wa ukweli, wengine wote waongo. Mtafute Yesu utapata jibu la matatizo yako
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Kila mtu ana haki ya kuamini kile ambacho anaona sahihi kwake...who are you to judge him? Nyie ni wasafi kiasi gani hadi mhukumu mapema hivi?

Mungu ametoa vipawa kwa watu wake ili watibie wwnzao kupitia mitishamba n.k ndugu ameona atapata msaada huko then mwacheni akapate salama yake. Kwani inaaminika imani yako tu ndo itakuponya, hivyo imani yako iko kwa sangoma. Mwacheni aende.

Mungu akujalie upone kupitia tiba za asili ndugu.

Kila la kheri!!

Asante kwa kunielewa ndugu.
 
Back
Top Bottom