Natafuta mchumba wa kiume, awe anaishi London

Zanzibar2014

JF-Expert Member
Nov 13, 2022
743
591
Mimi ni wanamke ninae penda kuwa
na amani na furaha wakati wote.

Natafuta mume, niliwahi kuolewa lakini hatukupata watoto, mimi sina watoto na ambae pia hana watoto, ili tupate watoto wetu pamoja.

Mimi silewi wala sivuti sigara n.k na
najitahidi kuwa kwenye misingi ya dini.
Na nahitaji mume ambae yuko kwenye
misingi ya dini pia havuti sigara, halewi n.k

Naipenda kazi yangu na nahitaji mume wangu mtarajiwa anaefanya kazi au biashara.
Elimu kamaliza college (huko mnaita
fomu 6) sio lazima kamaliza chuo kuwa
hata mimi pia sikumaliza lakini nitajiendeleza.

Naishi London, natoka Zanzibar, nafanya kazi ya ofisini, nina miaka 41, nahitaji mume wangu mtarajiwa kuanzi miaka 41 mwisho 50, muislamu hana mke/wake, anaishi London na sio mji mwengine wa UK, mimi ni 5'2" awe kuanzia 5’8”, rangi kama yangu kwenye picha yangu ya Avatar, vile vile Mzanzibari mwezangu. Ahsanteni saaana 🙏🙏

Tafadhali kama huna vigezo vyote nisamehe kuwa sitoweza kujibu, na kama huna uhakika tafadhali uliza kabla ya kunihukumu au kutumia lugha mbaya.

Tafadhali nisiombwe namba wala picha zaidi ya hiyo kwenye avatar yangu, tukubaliane kwanza mengine yatafuata inshaaalah kwa uwezo wake M/Mungu.
 
Mimi ni mwanamke ninaependa kuwa na amani na furaha wakati wote.

Natafuta mchumba atakaekuwa pia anataka kuwa kwenye ndoa.

Mimi sina watoto ambae pia hana watoto.

Najitahidi kuwa kwenye misingi ya dini na ambae pia yuko kwenye misingi ya dini.

Naipenda kazi yangu na nahitaji mume wangu mtarajiwa pia awe anafanya kazi.

Naishi London, natoka Zanzibar, nafanya kazi ya ofisini, tunahusika na uhasibu, nina miaka 41, nahitaji mume wangu mtarajiwa awe na miaka kuanzia 41, muislamu na awe anaishi London pia.
 
Shida ya wanawake wa sasa wanatafuta mfanyakazi au mfanyabiashara kwenye ndoa. Badala ya kutafuta mume ndiyo maana hamuolewi.

Hata akikuoa siku akifukuzwa kazi au biashara zikiyumba utamkimbia. Mnatanguliza masilahi mbele kuliko utu.
Kumbuka ndoa ni maisha halisi.

Kuna kufukuzwa kazi, biashara kuyumba au kuugua. Utaweza kuvumilia hayo ikiwa uliingia kwenye ndoa kwasababu mumeo ni muajiriwa, amejiajiri au mfanyabiashara?

Maneno ya busara yamenukuliwa kutoka Kwa Wong Fei
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom