Natafuta mashine ya kupukuchua mahindi

Natafuta mashine ya kupukuchua mahindi

manking

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2014
Posts
1,306
Reaction score
316
Wakuu habari,

Naombeni msaada wa kupata mashine ya kupukuchua mahindi kuna aina mbili nimeziona watu wanatumia.

1. Zipo zinazotumia engine ya petrol.

(2) Pia kunazile zinazotumia engine za diesel.

Nahitaji kujua bei zake na zinapatikana wapi hapa Tanzania.

Natanguliza shukrani kwa mwenye kufahamu.
 
ubungo millennium park, opposite na ubungo plaza. kuna wachina wanazo, ndogo kabisa ya petrol nafikiri laki nane, ila ya 2m ni nzuri ni diesel.
 
ubungo millennium park, opposite na ubungo plaza. kuna wachina wanazo, ndogo kabisa ya petrol nafikiri laki nane, ila ya 2m ni nzuri ni diesel.

Asante sana mkuu nitafika hapo.
 
Nikikumbuka kesho nitaangalia kumbukumbu zangu nikupe contact za wauzaji. Nilikutana nazo nane nane Kanda ya kaskszini mwaka huu, ndogo kabisa ilikuwa inauzwa laki tatu na nusu, yenye uwezo wa kupukuchua kilo 500 kwa siku.
 
Waone poly machinery co. Ltd, wapo ubungo millennium business park, wanazo mashine aina mbali mbali IPO inayopukuchua kilo 500 kwa saa, kg 1500 kwa saa na kg3000 - 5000 kwa saa. Hiyo ya kilo 500 kwa saa, msimu wa 88 walikuwa wanauza laki tatu na nusu. Simu zao 0654 333331, 0656 088888. All the best.
 
Wakuu wenye mrejesho kuhusu hizi mashine
Mi nataka nijaribu hii biashara kwa kuanzia na mashine ya kg 1500 kwa saa,

Vitu navyopenda kujua ni pamoja na utumiaji wa mafuta,lita ngapi kwa gunia ngapi, je haziharibiki haraka? maana vitu vya kichina vina changamoto flani hivi.
 
Nenda saba saba kama uko dar zipo nyingi sanaa..
 
Saba saba nimeiona kwa poly machinery pekee ndo wenye nazo, kama kuna penginepo nielekezwe jaman. Pia pale kila kitu kizuri siwezi kuielewa pale pale, uzoefu tafadhalini wakuu
 
Back
Top Bottom