Mkuu ukitaka mashamba au
shamba huko morogoro au sehemu ingine yoyote ya JMT isipokuwa unguja na
pemba inakubidi kwanza ubainishe eneo unalolitaka mfano kama ni morogoro
je ni kilosa? kilombero? ulanga? na baada ya hapo linalofuata ni wewe
kufunga safari hadi kwenye hilo eneo ulilolipenda, tatu unaenda kwa
ofisi za ardhi za wilaya, wao watakuambia sehemu yalipo hayo
mashamba/shamba, hatua ya nne ni kukutana na viongozi wa serkali za kata
na vijiji za maeneo hayo sasa serkali za vijiji wakikubaliana na wewe
wanahitisha mikutano mkuu na wanavijiji wanatoa mawazo na maoni yao,
wakikubalia basi umepata mashamba/shamba, lakini kwa ukweli siyo
mashamba wala shamba bali ni mapori ambayo mengine hayajawahi
kukanywagwa na mwanadamu tangu uumbaji, hivyo mwisho kabisa ni kazi
kwako kubadili pori kuwa shamba.
Gharama zitatofautiana kutoka eneo hadi eneo lakini kwa wastani
ukijumlisha huduma zote kuanzia usafiri, chakula, malazi, kulipia vikao
(sitting allowance) za serkali za kata/vijiji, kumtoa bwana ardhi
ofisini, gharama ya kununua ardhi (pori) na kulisafisha ili liwe shamba
ni 50,000.00 hadi 100,000.00 kwa hekari.