Natafuta kazi za ndani(maid)

Natafuta kazi za ndani(maid)

Dada wewe unajitambua. Kuna kijana mmoja alipohitimu Shahada yake aliamua kuendesha boda boda. Watu walikuwa wanamcheka sana eti Msomi mzima unaendeshaje boda boda. Leo hii ninavyokwambia kapata kazi ni Bosi kwenye Shirika fulani la Kimataifa na yupo nje ya nchi. Jamaa zake waliokuwa wanamcheka bado wapo wanazurura na bahasha za khaki posta pale.
Kiukweli bahati nzuri tu mimi nina mfanyakazi ambaye yupo vizuri sana otherwise ungenifaa sana. Nakutakia kila la heri.

Ujumbe: Zama hizi sio za kuchagua kazi, hasa kwa wale wanaotoka shule sasa hivi. Wako watu hapa watakubeza wakati kwa siku hawaingizi hata 100.
Kila la heri
Kweli mkuu umeongea facts.
 
Mimi ni mwanamke mwenye umri usiopungua miaka25.Nimehitimu shahada ya sanaa ya Elimu Yaani "Bachelor of Arts with Education"

Nimekuja Hapa jamvini kuomba nafasi ya kuwa mfanyakazi wa Ndani anayekuja na kuondoka

Kazi kuu inayonifaa ni
a. Kulea watoto
Nina ujuzi wa kutosha kulea watoto kielimu...kimaadili na kimwili pia. Watoto wako watafurahi kushinda nami kipindi hiki cha likizo
b. Usafi
Kufua nguo Za watoto...kupiga Deki nk
Niko kama machine kwani nimekulia kwenye familia ya watu wengi

Kazi nisizoweza kufanya:

Kumpikia Mume wa mtu Kama nitapata kwenye familia ya Mke na Mume.. Hiyo ni kazi ya mke

Kufua nguo za mume wa mtu

Ikiwa nitapata mwajiri mume ama Mke Asiye na mwenza hizo kazi naweza kufanya!!

Ratiba
Nina uwezo wa kufika saa kumi na mbili asubuhi na kuanza taratibu za kazi mpka saa kumi na mbili jioni
.Kila siku kasoro jumapili na siku nitazokuwa naenda kwa interview.

Malipo:
Elfu hamsini kwa wiki.

Uaminifu
Asilimia Mia...
Mahali ninapoishi
Dar es salaam pembezoni kidogo na mji

Nb
Wengine mtanipa ushauri nianzishe tuition nishaanzisha
Imekufa Wazazi huku uswazi wagumu kutoa pesa na watoto hawapendi kusoma.
Mitumba viatu nimeuza yaani nimetembeza door to door... Mtaji umekufa.
Ahsanteni.
Aliye tayari anipm
NimekuPm hujibu..utachezea bahati
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom