Natafuta kazi yoyote au Kibarua

Natafuta kazi yoyote au Kibarua

mtoto mdogo sana

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2020
Posts
476
Reaction score
1,449
Habari zenu Wakubwa;

Naamini hamjambo. Mimi pia.
Mimi ni kijana wa kiume mwenye miaka 24.
Natafuta kazi ama shughuli yoyote halali inayoweza kuniingizia kiasi chochote cha pesa. Kwa wakati hui sina maamuzi ya kuchagua wala utashi wa kuweka masharti juu ya aina au kiwango cha ugumu wa kazi. Pia niko tayari kufanya kazi Dar au mkoa wowote Tanzania na nje ya nchi.

Kiufupi:
- Ninajua kusoma na kuandika vizuri lugha ya kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha
- Ninajua vema kutumia kompyuta hasa program za kiofisi (word, powerpoint, exel n.k) na program za Graphic designing (photoshop, - - - -Illustrator) na nyingine za msingi zinazohusika na Internet.
- Nina afya nzuri inayoniruhusu kufanya shughuli ngumu.
- Pia nina cheti cha mafunzo ya JKT mujibu wa sheria.
- Nina uzoefu wa muda mrefu wa kusajili laini za mitandao yote na huduma za kifedha za mitandao ya simu,
- Nina uwezo wa kufundisha vizuri masomo ya lugha (Linguistics, Kiswahili) na Fasihi (Literature) pamoja na mengine ya sanaa. (NIMESOMEA, NGAZI YA SHAHADA YA KWANZA)
- Nina uzoefu kidogo kwnenye kurekebisha simu za mikononi.

Niko Dar es salaam. Na niko tayari kwa mchongo wa kazi yoyote halali ninayoweza kuimudu kati ya nilizozitaja au hata ambazo sijazitaja.

Kwangu, uaminifu ndio jambo la kwanza. Niko tayari kuweka dhamana ya utambulisho halisi wa Serikali za mitaa ninakoishi, Kitambulisho changu cha NIDA au hata cheti cha elimu za sekondari.

Natanguliza shukrani kwa yeyote atakayeguswa kunisaidia.
 
Ingia mtaan ongea na dereva bajaji yoyote akufundishe kuendesha ukijifunza nenda kakate licence ukipata licence jichanganye kwenye vijiwe vya bajaji au rud tena humu kunawa2 wanabajaj watakupa mishe
 
Ingia mtaan ongea na dereva bajaji yoyote akufundishe kuendesha ukijifunza nenda kakate licence ukipata licence jichanganye kwenye vijiwe vya bajaji au rud tena humu kunawa2 wanabajaj watakupa mishe

Asante sana kwa ushauri wako mkuu. Nitaufuata ushauri wako.
Nashukuru tena kwa kuchukua muda wako kunipa wazo bora.
 
Kila rakheri mkuu, umejielezea vizuri

Hello potential employers, please pitieni huku tumsaidie kijana.

Nashukuru kwa Kongole, pia kwa wito uliohitimisha nao.
Wewe pia iwapo unamfaham mtu anayeweza kunipa kibarua usisite kunikutanisha nae. Natanguliza shukrani
 
Kuna kitu ndani yako.Mungu atakuonesha namna.Nitakuombea na pia nitakutafuta kukiwa na FURSA.MUNGU AKUPE BARAKA TELE

Nimeguswa sana na kufurahishwa na mtazmo wako juu yangu. Ama kwa hakika umeniaminisha nimezidi kujenga kujiamini kupitia wewe. Nashukuru kwa Baraka zako na ahadi pia. Ubarikiwe sana ndugu yangu.
 
Kazi ipo ila si DAR. Nitag- pm

Habari.
Nashukuru sana.
Kama nilivyokwisha kueleza awali, sichagui sehemu ninayohitaji kufanya kazi.
Nakufuata PM unisaidie tafadhali.
Aidha natanguliza shukrani zangu za dhati.
 
Njoo Tabata relini, tembea kama unakuja chuo cha ualimu saint mary, kabla hujafika chuoni kuna stoo kubwa sana ina madirisha mengi ya aluminium.

Hapo Ndio kwa SHAYO. Njoo ubahatishe vibarua vya kumwaga zege au kushusha kontena za saint Anna.

uwe mvumilivu maana vibarua sio given hapo.

au,

kajiunge na ulinzi pale garda world
 
njoo tabata relini, tembea kama unakuja chuo cha ualimu saint mary, kabla hujafika chuoni kuna stoo kubwa sana ina madirisha mengi ya aluminium...

Asante Mkuu.
Nitakuja bila shaka jumatatu, Mungu akinijalia uhai na afya.

Kuhusu Ulinzi nilipeleka barua G4S walinambia huwa wana-recruit watu kulingana na order walizonazo. Kwa hiyo niko pending.
Nitajaribisha lakini kwenda hapo Gardaworld pia nipeleke barua
 
Back
Top Bottom