PierreLiquid
JF-Expert Member
- Oct 16, 2019
- 596
- 2,280
Habari,
Kwa majina naitwa Peter Bernad, miezi kadhaa niliwahi kutoa tangazo la kuomba nafasi angalau ya kuonyesha njaa yangu ya kujituma ili kutimiza mafanikio yangu kimaisha. Uzi wangu uliwagusa wengi, na nashukuru wengi wenu mlikuja DM kwa lengo la kutimiza hitaji langu la nafasi ya ajira.
Asanteni, ila cha kunisikitisha hakuna aliefanikisha kutimiza ahadi aliyonipa japo zilikuwa ni za kutia matumaini. Wengi niliwakumbusha Ila ilikuwa ni kama kero kwa wengi wenu. Kusaidia ni moyo ndugu zangu maandiko yanasema hakuna Jambo baya kama kuweka nadhiri ya ahadi kwa muhitaji, mnyonge au fukara bila kuitimiza maana machozi ya huyu mtu atamlilia Mungu akiamini yeye ndie sababu ya kushindwa kumfanyia wepesi kwenye hitaji lake.
Mungu hatopendezwa, Ila yote kwa yote nashukuru Mimi bado ni muhanga wa ajira nafanya biashara ndogo ndogo ambazo zinakizi kiwango kidogo cha kusongesha maisha yangu. Mimi Nina elimu ya stashahada ya ugavi na uchukuzi na uzoefu mkubwa wa masuala ya mikopo kama loan officer kwenye Microfinance.
Kama una moyo unaweza kunipa nafasi ili kutimiza malengo yako na ya kwangu. Sifa yangu kubwa ni uchapaji kazi bila kukata tamaa pale napopata nafasi. Asanteni na Mungu awabariki.
Napatikana Kinondoni Dar es Salaam