Natafuta kazi kwenye retail industry | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natafuta kazi kwenye retail industry

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by noella, Mar 28, 2011.

 1. n

  noella Senior Member

  #1
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  WanaJF Habari zenu,

  Nahitaji msaada wenu tafadhali.

  Mimi ni mama (single mum) wa watoto wawili, ninawasomesha na kuwatunza peke yangu. Sikubahatika kwenda shule kwahiyo sina elimu hata ya sekondari,niliishia form 2 kutokana na matatizo ya ulimwengu.

  Nilikuwa nafanya kazi kwenye duka fulani la nguo hapa mjini kwa bahati mbaya kutokana na ugumu wa maisha nikawa kwenye namba ya watu waliopunguzwa.

  kwa sasa natafuta kazi yoyote kwenye retail industry kwa maana nina uzoefu kwenye industry hiyo pekee..nimewahi kufanya kwenye maduka kama mawili hivi ya nguo na viatu.

  Mwenye msaada tafadhali anipm.Nitashukuru.

  Natanguliza shukrani za dhati.

  Mbarikiwe
   
 2. L'AMOUR

  L'AMOUR Senior Member

  #2
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  FOOT STEPS, BATA SHOE NA BORA INDUSTRIES,MARIEDO ni baadhi tu ya makampuni yanayoweza kukufaa ukitafuta hapo. Pia achana na mawazo ya ku stick kwenye kazi uliyozoea cha msingi ni uwe flexible kwa kufanya kazi yoyote inayoweza kukuingizia kipato. hii yote itategemea na uko mkoa gani kwani hata mashirika yasiyo ya kiserikali kuna wakati huwa wanatafuta wafanyakazi kwa ajiri ya kusaidia shughuli za vijijini. Nadhani ukiweka mambo yote kwa kirefu wanaJF watakusaidia tu kwa mawazo
   
 3. n

  noella Senior Member

  #3
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Asante.

  Mimi ninaishi Dar.

  Nilitanguliza kusema kwenye hiyo industry kwa kuwa ndiyo nina uzoefu nayo ila sichagui kazi
  ili mradi mkono uende kinywani na nipate kuwahudumia wanangu pia.
  nitashukuru sana kwa mawazo yenu.Maana nina wiki ya tatu sasa sina kazi na sijui naanzaje.
  Shukrani.
   
 4. L'AMOUR

  L'AMOUR Senior Member

  #4
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Noella mwanzo huwa mara nyingi ni mgumu mimi nakushauri kwa kuanzia kamata vyeti vyako au barua zako za kazi na zile zinazoonyesha umeshawahi kufanya kazi sehemu kisha weka uwoga pembeni na kuanza kuonana na waajiri usijieleze shida yako mlangoni utaishia kwa walinzi na makatibu muhtasi ambao wanapenda kuchukua nafasi za wakubwa wao. Pale ppf tower kuna duka la nguo na viatu linaitwa mariedo nadhani maria sarungi anahusika nalo unaweza jaribu pia pale mlimani city kuna foot step wanauza viatu pia millenium business park kuna ofisi na duka la bata hapa ukipeleka CV inaweza kukupa mwanga kwani hawa bata wana maduka karibu mji mzima wa dar. So please act now vinginevyo watoto watakufa njaa na utapata vidonda vya tumbo. hii dunia sio njema na marafiki watakukimbia wakikuona ni mzigo kwao. All the best noella
   
 5. n

  noella Senior Member

  #5
  Apr 2, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Asante sana ushauri wako umenipa mwangaza.jana nilienda bata pale millenium business park nikaonana na manager
  akanambia wanahitaji cheti cha form four,ambacho mimi sina.kwahiyo ningepata ingekuwa si hicho.
  kuna mtu kanambia naweza kuchongesha ila pia kichwa changu hakinipi
  ningekuwa na uwezi ningesoma ile wanaita QT angalau na mimi niwe na cheti.
  sasa nimekwama hooo
   
Loading...