Yaani hii ya kukomaa mwenyew naitamani sana ila muda sasa kuugawa ndo shida....me nataka ninunue mawili afu mwezi wa 5 nikamate madogo wawili nikakae nao chaka flan hivi tukabebe mpunga,mihangaiko yangu mikubwa ipo mjini na mjini si mbali sana na hilo chaka,so nimeoanga yaan nakaa nao wiki,wiki narud mjini....nakaa nao tena wiki then wiki narud mjini na madude nayafunga GPS kabisa.
Kwenye hela niwaambie madogo kwamba nitawalipa 350 kila mmoja kwa mwezi na posho ndogo ndogo niwe nawatoa kila siku ila kila guta lilaze 60 kwa siku.
Natafuta wale madogo ambao hawana majukumu home.
Vipi hii idea unaionaje mkuu?