Natafuta fuso (tani 10) ya kukodi kwa mkataba

MUST

Senior Member
Mar 11, 2012
107
63
Wakuu amani iwe nanyi. Kama tittle invyoonoesha. Nahitaji kukodi fuso ya tani 10 kwa ajili ya kubebea bidhaa ya unga wa mahindi mkoa wa marogoro na Iringa. Nikikabidhiwa gari hiyo nitalipa hesabu ya mwezi ya Tsh 1,800,000/-. Ifahamike kuwa mimi ndio mwenye biashara hiyo ya unga na sio dalali wala dereva. Makabidhiano yanafanyika kati ya mwenye gari na mimi. Majukumu ya mwenye gari na mimi ninayekodi ni kama ifuatavyo.

1. MIMI NINAYEKODI
Nitalipa hesabu hiyo ya 1,800,000/- kwa mwezi
Nitahusika kulipia gharama ya mafuta
Nitahusika na posho ya driver
Nitahusika na Matengenezo madodo madogo pamoja na kumwaga oil

2. MWENYE gARI
Atahusika na kubadili matairi yanapoisha
Atahusika na service kubwa ya engine pale itakapojitokeza

Kwa yeyote atakayekuwa interested na biashara hii anipigie au kuacha ujumbe kwa 0654000253
Asanteni
 
Yaani nikupe Fusso kwa Hesabu ya Tsh. 60,000 kwa siku?

Kama uko tayari kwa hesabu ya 250,000 kwa siku sema tuongee biashara..
 
Umepiga mahesabu vibaya na hiyo biashara yako!! Hesabu ya fuso yenye uwezo wa kubeba tani kumi kwa mwezi ni milion tatu had tano kutegemea na aina ya biashara inayofanyika,!!! Mkoa wa Arusha na manyara matajiri wengi wanawapa madereva haya magari na wanachukua milion tatu had nne kwa mwezi, !! Jaribu kujiuliza mtu anayebeba nyanya kutoka ilula kwa laki nane iyo ni safari ya usiku mmoja then kesho anarudi Iringa akiwa na tani tisa za bati au Nondo au square pipe na juu anaweka kret tupu za nyanya kesho yake jion anapakia tena! Anapata pesa nyingi sanaaaaa kuliko unavyoweza kudhani na hizi ndio gar zinazopendwa sana na wafanyabiashara hasa wa mazao fresh maana ni nyepesi na zina speed nzuri na zinauwezo mzuri kwenye njia mbaya wakati wa kupakia mzigo.
 
sijahtaji uchambuzi nimehtaji mwenye fuso...tatizo watanzania mnapenda kuchambua sana bila kuja na way fowrd. wati 3 wote hawana huduma nnayohtaji ila wanachambua tu...siasa nlukuki nahtaji mwenye huduma kama hana pita mbele
 
Ww umeambiwa ukwel una mashart kama mganga wa kienyej unadhan fuso ya tani 10 garama yake shi ngapi? Kama vipi nunua yako
 
sijahtaji uchambuzi nimehtaji mwenye fuso...tatizo watanzania mnapenda kuchambua sana bila kuja na way fowrd. wati 3 wote hawana huduma nnayohtaji ila wanachambua tu...siasa nlukuki nahtaji mwenye huduma kama hana pita mbele

Kaulizie bei Ya Fuso complite ikiwa imeshawekwa body hapa bongo alafu ndio urudi na hizi hoja zako hapa. Ingekuwa rahisi namna hiyo mimi ningekodi kumi alafu baada ya mwaka ningenunua zangu mbili na ningemnunulia mke wangu Rav 4 Kill Time!!
 
Hii ndo kitu inaturudisha nyuma...nimepata reply 7 lakini katika hizo hakuna hata mmoja mwenye gari wote wanachambua tu. Bahati mbaya wako ananymous so they have nothing to loose wao ni kuongea tu. nipe way foward sema fulani ana gari au nani anagari namba zake hizi hapa ongea nae mfanye biashara. au mimi nina gari kwa bei hiyo tunfanye hivi na hivi. Sasa hapa iko tofauti wewe huna gari unacomment nini. Nani kasema anahitaji gari mpya hadi unipigie hesabu za fuso mpya. Mini ninatoa offer ya 21.6m per year, assured earning. kuna mtu itamfaa ntafanya nae biashara. asa unavyocomment humsaidii mwenye gari wala hunisaidii mimi, wala hamna umuhimu wa hii forums sasa. Zaidi zaid unamprempty mtu mwenye nia ya biashara. kama huna gari wala huna njia ya kuniunganisha na mwenye gari kaa kimya au pita sio unaleta ujuaji. Am waiting to talk to serious people and not some little crap who spend their useless time to comment.
 
Wakuu amani iwe nanyi. Kama tittle invyoonoesha. Nahitaji kukodi fuso ya tani 10 kwa ajili ya kubebea bidhaa ya unga wa mahindi mkoa wa marogoro na Iringa. Nikikabidhiwa gari hiyo nitalipa hesabu ya mwezi ya Tsh 1,800,000/-. Ifahamike kuwa mimi ndio mwenye biashara hiyo ya unga na sio dalali wala dereva. Makabidhiano yanafanyika kati ya mwenye gari na mimi. Majukumu ya mwenye gari na mimi ninayekodi ni kama ifuatavyo.

1. MIMI NINAYEKODI
Nitalipa hesabu hiyo ya 1,800,000/- kwa mwezi
Nitahusika kulipia gharama ya mafuta
Nitahusika na posho ya driver
Nitahusika na Matengenezo madodo madogo pamoja na kumwaga oil

2. MWENYE gARI
Atahusika na kubadili matairi yanapoisha
Atahusika na service kubwa ya engine pale itakapojitokeza

Kwa yeyote atakayekuwa interested na biashara hii anipigie au kuacha ujumbe kwa 0654000253
Asanteni
atleast laki kwa siku na gharama zote za juu ni zako
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom