Natafuta chuo cha ualimu ngazi ya cheti karibu na Dar

ESPIRIT

JF-Expert Member
Jul 3, 2014
665
524
Husika na kichwa cha habari. Ni mdogo wangu namtafutia Chuo cha ualimu kwa ngazi ya cheti, kilichopo angalao karibu na mji wa Dar es Salaam
 
Husika na kichwa cha habari. Ni mdogo wangu namtafutia Chuo cha ualimu kwa ngazi ya cheti, kilichopo angalao karibu na mji wa Dar es Salaam
Je, ana vigezo tajwa vya kudahiliwa katika kozi husika?

Kama ndiyo, Ualimu wa aina ipi? Ualimu wa Shule za Kingereza (English medium) au Shule za Serikali?

Kama jibu ni shule za serikali, basi tembelea tovuti ya NACTE www.nacte.go.tz akasome maelezo na kuomba udahili. Udahili huo unafanywa kwa mfumo wa udahili wa pamoja (CAS) kwa kozi za Ualimu na afya, chini ya Wizara ya Elimu na Wizara ya afya pamoja na Chuo husika.

Kama ni Mwl wa shule zinazotumia Kingereza kama lugha ya mawasiliano, basi wasubirie wengine watakuja kukupa Mwanga uende kuomba udahili chuo gani.

NB: Hata hivyo sidhani kama kuna vyuo vinatoa mafunzo ngazi ya Cheti, kwa walimu wa Shule za Serikali. Naona ni kuanzia Diploma, miaka mitatu.
 
Ooh, Yaani JF siiachi hata siku moja, nashukuru kwa ushauri wenu, wa haraka hivo
 
Kibamba /vikindu ni government au private wakuu. Na ada zao vipi
 
Kibamba /vikindu ni government au private wakuu. Na ada zao vipi
ACHANA na VYUO vya PRIVATE,
Nenda VIKINDU chuo cha serikali,
ADA 600,000/=
pia kwa maisha haya private gharama kubwa wakati mshahara watalipwa sawa.

Serikalini ukilipa 600,000=
hakuna tena kulipia hostel wala chakula

huko private hawaivi vizuri na ajira ya sasa tunaanza kuomba hatapata kipaumbele
 
Kweli kabisa mkuu, akisoma serikali inakuwa fresh zaidi maana kaichangia serikali
 
Back
Top Bottom