Natafuta chuo cha ualim wa secondary dar es salaam

Diploma in secondary Education haipo tena.
Unatakiwa kusoma Diploma in primary Education ili uwe mwalimu wa msingi au Bachelor degree ili uwe mwalimu wa sekondari
 
Haijalishi una DivI ila Diploma in secondary education haipo tena...Tangu mfumo wa diploma in primary Education uje mambo yakapinduka...Pole sana mkuu
 
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu wote walioomba kudahiliwa katika kozi za Astashahada (Cheti) na Stashahada (Diploma) na Umma kwa ujumla kuwa dirisha la maombi lilifungwa mnamo tarehe 15 Septemba 2016 ili kuruhusu uteuzi wa awamu ya pili kwa waombaji wa kozi hizo.

Uteuzi wa awamu ya tatu kwa waombaji wa Astashahada na Stashahada unatarajiwa kutangazwa mnamo tarehe 5 Oktoba 2016, hivyo basi waombaji wanaombwa kuwa na subira ili kutoa muda kwa Baraza kukamilisha taratibu za uteuzi huo.

Maombi mapya ya Udahili
Baraza linapenda kutoa taarifa kuwa Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS) utafunguliwa tena tarehe 5 Oktoba 2016 hadi tarehe 15 Oktoba 2016 ili kujaza nafasi za udahili zilizobaki wazi baada ya uchaguzi wa awamu ya pili. Hatua hii itawezesha kuruhusu machaguo mapya kwa wale ambao hawakuchaguliwa katika kozi walizoomba pamoja na kuruhusu waombaji wapya ambao kwa njia moja au nyingine hawakuweza kuomba hapo awali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom