Wakuu kwanza nitangulize Salamu kwenu .Wakuu kuna wazo limenijia nikalitafakari nakuona ni-share na nyie ,kama mnavyojua kuwa ajira saiv zimekuwa ngumu sana cha msingi ni kuangalia namna ya kujiajiri wenyewe kwa sababu hata kama ajira hakuna lakini bado mahitaji muhimu ya kibinadamu yapo pale pale .Sasa wazo lenyewe ni hivi wakuu kuna kigari nilinunua huko nyuma lakini saiv nimeipack uwani coz sina kazi na pia ina break down kidogo hivyo nikapata wazo la kuifufua na kuifanya uber ,ambopo hadi isimame vizuri na kuweza kukaa kibiashara inahitaji kama 600,000 tsh .Sasa kutokana na hali yangu ya kiuchumi saiv sio nzuri naalika mtu ambae anaweza kutoa hiyo amount kwa makubaliano kama yafuatayo .Gari ikishakaa sawa nitaifanya uber na dereva nitakuwa Mimi mwenyewe hivyo katika hela yake atakayotoa nitwaweza kumlipa 35,000 kwa wiki na kwa mda wa miezi 6 amboyo ni sawa na 840,000 na plus nusu ya hela aliyoweka 300k ambayo italipwa baada ya hiyo miezi sita .nitangulize shukrani na maoni pia wakuu.Ambae atakuwa tayari tutasaini makubaliano kwa mwanasheria kabisa kwa kulinda pande zote mbili.