natafuta asali mbich ambayo haijachakachuliwa

Ninayo asali mbichi ambayo ni ya Dodoma,sifa yake ni kuwa inatokana na mchanganyiko wa maua ya alizeti,mibuyu n.k,tofauti na ya kutoka baadhi ya sehemu za tabora ambayo ina mchanganyiko wa maua ya tumbaku na kama inavyojulikana tumbaku inapigwa dawa nyingi kwa hiyo asali yake itakuwa na slight difference katika formula ukilinganisha na ya Dodoma.

Nitumie contacts zako halafu nitakutumia kwa njia ya basi kama lita 1 hivi ili ujaribu na tumia njia zozote kuipima ikiwemo TFDA.Sitakutoza fedha kwa hiyo lita 1,ila gharama ya usafiri wake ambayo haitozidi 3000.
 
Mmh mimi nimenunua asali ambayo iko katika pakeji inayoridhisha na inayo mawasiliano ya msambazaji zikiwemo namba za simu na box. NIKIITAZAMA SASA INAONYESHA ROBO YA CHUPA KUANZIA CHINI IMEGANDA NA IKIPATA JOTO INAYEYUKA NA KURUDI KAWAIDA. Sasa inamaana hii asali niliyoinunua nayo itakuwa FEKI ? Na huyu msambazaji amewezaje kuhalalisha kitu feki kwa kujitangaza kibiashara.

Asali huyeyuka pia lakini inaweza kuganda,wakati mwingine warinaji huchanganya asali ya mzinga 1 na mwingine kwa sababu inaweza wakati mwingine kuna tofauti ya wepesi wa asali kwenye mizinga tofauti,hebu jaribu kuchukua kiberiti halafu pakaa njiti asali halafu washa kwenye ganda.mara nyingi iliyochakachuliwa huwa haiwaki! Kuna mbinu nyingine nitarudi nikipata wasaa
 
Kama unakaa Dar njoo Sinza madukani ule mtaa unaenda Namnaan hotel upande wa kushoto kuna duka linauza asali origino kuanzia nyuki wadogo mpaka wakubwa asali original haitakiwi kuganda...thanks

Napingana na wewe.Asali ni cristal..ikiganda inatengeneza mgando wenye chembechembe kama sukari.Unadhani dhana ya asali mbichi imetokana na nini? kwamba mtu anachukua asali pure ambayo ni nzito halafu anayeyusha na kuchanganya na vitu vingine kama maji yenye sukari guru au hata unga wa ngano..na mara nyingi inatakuwa nyepesi na hiyo haimaanishi asali zote nyepesi zimechakachuliwa lakini probability ni kubwa.

Duka hilo nilishawahi kuliona ila sijachunguza asali kwa hiyo siwezi kuhukumu.
 
Ivi asali huwa inaharibika? ( ina muda wa kutumia?)

labda nimenunua asali leo (original) haijachakachuliwa naweza nikaitumia kwa muda gani?

Itunze asali katika sehemu isiyo na joto wala baridi kali halafu inaweza kukuchukua muda wa miaka zaidi ya 3 ikiwa poa kabisa.Ila muhimu kukumbuka ni kuwa lazima formula yake itabadilika kidogo.Namaanisha inapungua ubora na si kuharibika kabisa.
 
BAADA YA ASALI KUONEKANA NI MSAADA KWA MATATIZO MENGI YA KIAFYA WATU WASIO WAAMINIFU WAMETAKE ADVANTAGE YA KICHAKACHUA ILI WAFAIDIKE, MIMINIMENUNUA JUZI HUKU KWETU TANGA NIMEITEST IKO POA KWANI YALIPUKA HIYO YAHE. (CHUPA YA ORANGE TSH. 5000 TU.:yawn:
 
Ivi asali huwa inaharibika? ( ina muda wa kutumia?)

labda nimenunua asali leo (original) haijachakachuliwa naweza nikaitumia kwa muda gani?
Asali huwa haiharibiki hata kidogo nani wewe kakwambia asali inaharibika? Asali waweza kutumia wakati wowote hata kama ikikaa mwaka mzima Asali haiwezi kuharibika hata kidogo

hebu ngoja mzizi mkavu atupe utaalamu
Asali ni dawa ya kila maradhi kwa mfano Asali umpake maiti hawezi kuoza hata akae miaka 100, Asali inatibu maradhi mengi tu. Asali ina faida nyingi tu,
 
Na mimi ninakusaidia kwa kuhakikisha kuwa hiyo ni Asali mbichi ni ya kweli Siyo feki itabidi uiweke kwenye friji ikiwa haijaganda itakuwa ni ya kweli hiyo Asali mbichi Orignal lakini ikiganda hiyo ni Asali ni Feki iliyochakachuliwa ni hivyo Mkuu, Kupata Asali mbichi mijini ni kama kupata Almasi Sokoni tena unakuwa hiyo Almasi umeikota hapo Sokoni si rahisi nyingi za Asali zilizopo Masokoni ni feki zimechakachuliwa.

...Asali mbichi imekuwa adimu sana kuipata siku hizi na bei yake imepanda sana. Hili limesababishwa na Mkuu mmoja hapa jamvini ambaye anaitwa Nyama Yao :):) ambaye aliandika kuhusiana na asali mbichi na kuipandisha sana chati na hivyo kuifanya demand ya asali mbichi iongezeke kupita kiasi.

 
Asali orignal unazipata taboro tu hapo dar nimarogi tu.

Ngoja siku naenda tabora takupitia ukachukue mwenye kutoka kwenye mzinga :biggrin:
 
Asali halisi haina expiry date. Haihalibiki. Ikikaa muda mrefu bila kutikiswa huganda juu lakini ndani inakuwa na Hali ileile. Haishambuliwi na bacteria au virus.
endapo bado hujapata nipm
 
wadau naombeni msaada asali nyingi za hapa bongo zimechakachuliwa, i am real inthe need of natural honey, tena asali mbichi, anybody who can help please PM me uniambie bei, na ntakupataje,naamini jf ndo mambo yote

Nipe namba yako ya sim na niambie upo wapi nitakutumia bure udugu kusaidiana
 
Mi nahitaji asali mbichi ya nyuki wadogo, mwenye nayo tafadhali tuwasiliane
 
Mi nahitaji asali mbichi ya nyuki wadogo, mwenye nayo tafadhali tuwasiliane

Faida za asali wa nyuki wadogo na wakubwa karibia zinalingana,tofauti ni ufanyaji kazi.Ya nyuki wadogo inawahi kufanya kazi mwilini kuliko nyuki wakubwa.Hiyo ya wakubwa ninayo...kwa sasa nipo Dom
 
Itunze asali katika sehemu isiyo na joto wala baridi kali halafu inaweza kukuchukua muda wa miaka zaidi ya 3 ikiwa poa kabisa.Ila muhimu kukumbuka ni kuwa lazima formula yake itabadilika kidogo.Namaanisha inapungua ubora na si kuharibika kabisa.

shukrani plato
 
Asali huwa haiharibiki hata kidogo nani wewe kakwambia asali inaharibika? Asali waweza kutumia wakati wowote hata kama ikikaa mwaka mzima Asali haiwezi kuharibika hata kidogo

Asali ni dawa ya kila maradhi kwa mfano Asali umpake maiti hawezi kuoza hata akae miaka 100, Asali inatibu maradhi mengi tu. Asali ina faida nyingi tu,

Hakuna alieniambia ni swali tu niliuliza mkuu!

hata ivyo shukrani kwa kunijibu.
 
Back
Top Bottom