Natabiri haya baada ya tume ya Nape kuhusu mkuu wa mkoa Dar

CK Allan

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
2,781
6,065
Pengine nikawa tofauti na wengi lakini nadhani wapo wengi ambao pia wanahisi kama mimi kuhusu tume hii kumaliza kazi yao... swali la wengi ni "what next?" mimi natabiri haya yafuatayo...

1. RC hatawajibishwa kama wengi tunavyodhani, maana tayari ameshakingiwa kifua, kuwa apige kazi asisikilize mengine...

2. Itatafutwa sababu ya kumfanya RC kuingia clouds usiku (kumbuka tayari kuna nadharia mbali mbali mfano alipeleka kipindi chake, au alienda kutafuta madawa ya kulevya au vyovyote vile) endapo italazimika kufanyika hivyo..

3. Kwakuwa RC hakuhojiwa hii itafanya ripoti hii kukosa uhalali na itaonekana ni lengo la kumchafua jamaa tu, na pengine hata ripoti nzima kuwekwa kapuni..

4. Ripoti ikifika "panapohusika" huyo anayehusika na utumbuaji atasema yupo bize na mambo mengine asidraiviwe.....

5. na pengine kwa mshangao wa wengi badala ya RC kutumbuliwa anaweza kupewa cheo kikubwa zaidi...
6. hatimaye shoka imeungua mpini umebaki.. News Alert: - Magufuli afanya mabadiliko madogo kwenye Baraza la Mawaziri.
Tuendelee kuwemo...
 
Na sie wengine tunataka asimtumbue sasa ili ajianike mwenyewe na kuuthibitishia umma kwamba yeye ni mtu wa aina gani!!

Baada ya hapo, ni jamii ya Kibashite pekee ndiyo itaweza kuamini kwamba JPM hapendi ujinga!!!

Kadri siku zitakavyoenda huku akimbeba Bashite; ndipo watu wengi zaidi watakavyopata fursa ya kuiona sura halisi ya Baba ake Bashite ambayo wengine hadi leo hawajaigundua!!!
 
Hamna jinsi, Matendo ya makonda yamechafua taswira za mamlaka za uteuzi na heshima yake, naamini kwa kuwa uraisi ni taasisi, hata kama Rais anampenda kijana wake, ataambiwa kuwa kuendelea na huyu kijana kunaifanya taasisi hii ikose imani ya umma na hivyo muweke pembeni tu!
 
Pengine nikawa tofauti na wengi lakini nadhani wapo wengi ambao pia wanahisi kama mimi kuhusu tume hii kumaliza kazi yao... swali la wengi ni "what next?" mimi natabiri haya yafuatayo...

1. RC hatawajibishwa kama wengi tunavyodhani, maana tayari ameshakingiwa kifua, kuwa apige kazi asisikilize mengine...

2. Itatafutwa sababu ya kumfanya RC kuingia clouds usiku (kumbuka tayari kuna nadharia mbali mbali mfano alipeleka kipindi chake, au alienda kutafuta madawa ya kulevya au vyovyote vile) endapo italazimika kufanyika hivyo..

3. Kwakuwa RC hakuhojiwa hii itafanya ripoti hii kukosa uhalali na itaonekana ni lengo la kumchafua jamaa tu, na pengine hata ripoti nzima kuwekwa kapuni..

4. Ripoti ikifika "panapohusika" huyo anayehusika na utumbuaji atasema yupo bize na mambo mengine asidraiviwe.....

5. Mwisho kwa mshangao wa wengi badala ya RC kutumbuliwa anaweza kupewa cheo kikubwa zaidi...

Tuendelee kuwemo...
Hata akipewa cheo kikubwa imani iko wapi tena,kama majina siyo halisi??
 
Wao waendelee tu na Madaraka yao. Hakuna lenye Mwanzo likakosa Mwisho.

Kadri wanavyozidi kulindana ndivyo kadri mambo yao yatazidi kufunuliwa.

Mungu hua Haendi Likizo.
 
Back
Top Bottom