Natabiri Bashiru kuwa Waziri Mkuu

Tanzania ni nchi inayoamini katika Uhuru wa kutoa maoni.
 
Wewe utakuwa bashiru bila Shaka maana hata hujui sifa kuu za mtu anayeweza kuwa PM kwa mjibu wa Katiba. Hivi nikuulize wewe bashiru umechaguliwa kuwakilisha Jimbo gani? Viti maalum siyo jimbo
 
Mtu kaonyesha umbumbu wake yaani hata hajui pm anatakiwa awe mbunge wa namna gani
 
Kwa hiyo unataka kutwambia mojawapo ya sifa ya waziri Mkuu Tanzania ni uongo? Maana huyu aliyepo ni mwongo na aliwadanganya watanzania mchana kweupe wakati Jiwe akiwa hatunaye yeye akasema anachapa kazi. tena alidanganya akiwa msikitini. Na huyu unayempigia debe aliapa kwamba hatakubali uteuzi mwingine lakini sote ni mashahidi kwamba amekubali teuzi nyingi ikiwemo ya ubunge alionao. Kabla aliteuliwa kuwa balozi na pili kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.
 
Ila ninyi wanaCCM angalau muwe mnahudhuria tuition ili mjue katiba na nchi yetu kwa ujumla. Akili zenu finyu mno! Hamjui kwamba PM sharti awe ni mbunge wa kuchaguliwa?
 
mimi kinacho nishangaza mbona watu wamefurahi sana jamaa kushuka nafasi ....
 
Kuna mambo kadha nayaona kwa Bashiru

Mama kama kamtoa Bashiru kwenye hiyo nafasi kwa sabbu ya kutompenda...basi ataangukia pua...hana lake.


Lakini kama ametolewa kimkakati. ..basi atapewa wizara then kwa baadae atakuja kupewa nafasi kubwa ya kiserikali.

Muda ni Mwalimu.

Maisha yanabadilika
 
Waziri Mkuu huwa mbunge wa kuchaguliwa toka jimboni, si wa kuteuliwa. Subiri aje agombee jimbo litakalokuwa wazi na kuchaguliwa au asubiri uchaguzi mkuu 2025 ndipo utabiri
 
Wa manyani huko mbuga ya Mwl Nyerere zamani selous
 
Waziri mkuu BILA JIMBO?
Waziri Mkuu hatokani na wabunge wa kuteuliwa
 
Pitia Katiba kwanza ndipo uandike hicho unachofikiria kuandika.PM ni lazima atokane na mbunge wa Jimbo
 
Hahhaha....bashiru anajipigia ngoma ndogo, asijisifie vyeo vya mbeleko bali ajijenge mwenyewe tuweze kutambua uwezo wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…