Ndoto zinaweza kukupata kutokana na mazingira uliyo nayo/ unayo lala
Hiyo sehemu unayolala inaweza ikawa mi nyumba ya mapepo/ majini hivyo yana kuingilia.
Kingine ukute zamani ulikua unapiga punyeto( punyeto maana yake unafanya mapenzi ma majini mahaba hivyo unayapa uhalali wa kukutesa
Kingine inaweza kuwa umefungishwa ndoa za majin mahaba / wanawake wa kipepo ktk ulimwengu wa roho bila ww kujua
Hivyo yana uhalali kabisa ya kukuigilia ktk mwil wako sababu ww ni mke wao halalii.
Kingine hao wanaume walio pita kwako wana maroho machafu ndio maana yanakutesa( spirits).
Sababu kama wew ni bint ukifanya kile kitendo unapokea na mwanaume anatoa
Na Biblia yangu inaniambia ajiunganishae na kahaba wamekua mwil mmoja
Hivyo zile roho zotee alizo kuwa nazo huyo mwenza naww unakua nazo
Mpka hapo umenielewa?
Huna haja ya kupanda ndege uende kwa nabii gani sijui
Mm ninachojua Mungu wangu/ Yesu wangu ni wa wote juhud yako tu ya kuomba itakutoa kwenye shida yako
Mungu hayupo kuwa special kwa grp fulan tu la watu.
Hapana . Mungu hana upendeleo na wala hapokei rushwa.
Umenielewa had hapo?
Yes ndoto ni lango la kiroho ndani ya mtu. Mungu anaweza kupitishia maonyo, maelekezo na kukukumbusha kupitia ndoto, likewise na shetani anaweza kutumia lango la ndoto kupitishia mambo yake mabaya
Kuota unafanya mapenzi, simply inaonesha kuwa kwenye ulimwengu wa roho una mahusiano ya kingono na ulimwengu wa giza. Kinachokuja kuleta shida sio tu kufanya mapenzi, bali ni ule muunganiko na maagano yanayoletwa na ngono (union and covenants) . Kwa ufupi tu ni kwamba spiritually wewe ni mke wa mtu, upo ndoani hapo na spiritual husband wako.
Yeremia 1:5
kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni nalikutakasa, nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.
Kwa hiyo ulizaliwa ukiwa msafi, hukuwa na tatizo lolote, mwili wako ulitumika Kwa ajili ya Mungu. Lango la ibilisi kuingilia na kukutumia wewe lilikuwa limefungwa. Mwili wako ulikuwa ni hekalu takatifu la Mungu, Mwili wako ulitumika kama dhabihu kwa Mungu.
Mathayo 13:25
Lakini watu walipolala akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.
Kwa hiyo wewe ulikuwa kama ngano iliyo safi. Lakini uliposinzia (sio tu kusinzia kimwili), but ulipoanza kuenenda kimwili, imani yako ilipokuwa haba, shetani akapata lango, akaingia na kupanda uharibifu juu yako (magugu)
Mwanzo 4:7
Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo yakutamani wewe, walakini yapasa uishinde
Kwa hiyo kwa dhambi zetu na kutokusimama sawasawa na Mungu, tunafungua milango ya dhambi kuingia maishani mwetu na Kupanda uharibifu
I Wakorintho 6: 19
Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu?.....
Kwa hiyo kwa kupitia uzinzi na huyo spiritual husband Au wife unachafua hekalu la Roho Mtakatifu, je Roho Mtakatifu anakaa mahali pachafu? ? Hapana....
SPIRITUAL WIFE/ HUSBAND ANAINGIA KUPITIA
1. Kujichua/ kupiga punyeto
2. Kuangalia porn
3. Nguo za ndani, damu ya hedhi na manii. Vinatumika sana kutuletea majini
4. Kuchanjwa Chale au kuchora tattoo (2Walawi 19: 28)
5. Mvuto wako (sexual appeal); kama ambavyo binadamu tunakutana na kutamaniana, vivyo hivyo hata jini mahaba anaweza kukuona na kutamani uwe mkewe
6. Maagano: kuna wamama wanaopata watoto kupitia waganga na mizimu. Baba wa mtoto ni nani, unamjua? Na wakati mwingine mganga anakuingizia dawa kwa kutumia uume wake
7. Kuvaa Pete za urembo. Pete ni ishara ya mamlaka Au muunganiko wa watu/ agano (Ndoa), haya wewe si unavaa Pete huku Huna hata mume, basi mume jini mahaba atakutafuta mfunge Ndoa vizuri
8. Kuna wanaorithi kabisa majini mahaba. Inakuwa kama ni tatizo la ukoo/familia nzima. Mtu mmoja alifungua lango, jini mahaba akaingia kwa familia nzima
9. Kuvaliana/ kuazimana Nguo , bangili, Pete etc.
DALILI ZA KUWA NA SPIRITUAL HUSBAND/WIFE
1. Kuota unafanya mapenzi na watu usiowafahamu na wakati mwingine hata na ndugu zako unaowafahamu. Wengine inakuwa too much hata mchana ofisini akipitiwa tu na usingizi anapata ndoto hizi. Na wengine akiamka anakuta amechafuka kweli
2. Kuota unafunga Ndoa na watu usiowafahamu
3. Kuota una familia, au unakuwa unaona ndotoni kuwa unalala na partner wako
4. Kuota unanyonyesha, unamuogesha mtoto
5. Kuota una mimba. Na kuna wengine huwa wanapata mabadiliko yote kama anayopata mama mjamzito wa kawaida. Kuna wengine wanaota kabisa wanajifungua Au kupata miscarriage
6. Kutokuwa na uwezo wa kutungisha mimba Au kuzaa. Huyo spiritual wife/husband kwanza hatokuruhusu ukutane kimwili na mtu mwingine apart from yeye, hawapendi kushare mapenzi na binadamu. Na yanaweza kukufunga kabisa usizae na binadamu ili uwazalie wao tu
7. Kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa. Jini mahaba Anakusatisfy ukilala, ukiamka hamu yote haipo
8. Kutotaka Ndoa kabisa, kuchelewa kuolewa/kuoa na kutodumu katika ndoa. Tayari katika ulimwengu wa roho una ndoa, ndoa ya pili ya kazi tena? Wewe ni mke/mume wa mtu, hawawezi kukuruhusu ufunge ndoa tena na binadamu. Kuna watu wanafikia hadi hatua ya kuwa-engaged, kesho tu akiamka hamtaki tena mchumba wake. Mkijikongoja mkaoana basi mtapata vita haswa na mafarakano, hadi muachane. Utakuwa na spirit ya "Marry and Remarry
9. Kufunga hedhi bila mimba, kutokwa na damu nyingi sana randomly na wakati mwingine kupata damu chache sana.
10. Mikosi na mabalaa mbalimbali