Nasubiri Heshima ya Bunge Kwa General Kyaro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nasubiri Heshima ya Bunge Kwa General Kyaro

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Megawatt B, Apr 11, 2012.

 1. M

  Megawatt B JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2012
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  ....Ninasubiri, na nitafurahi na kuona kwamba Bunge letu limefanya haki kama litasimama dakika moja tu, kutoa heshima kwa mpendwa wetu, kamanda, aliyekwenda vitani akakoswa risasi na majeshi ya idd Amini kwa niaba yetu, aliyekuwa mkuu wa majeshi ya Tanzania (1988-1994) marehemu General Mwita Kyaro... sitaki mlundikano wa watu, sitaki wabunge watoke bungeni... nataka wabunge wasimame dakika moja tu basi!
   
 2. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Taarifa rasmi ikifika bungeni watafanya hivyo kama kanuni za bunge zinatoa ruhusa hiyo.

  Inawezekana kanuni inasema watasimama kwa wabunge waliokufa na viongozi wa kitaifa wa kisiasa tu.
   
 3. K

  KAFWIMBI Member

  #3
  Apr 11, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi ni nani alipeleka taarifa ya kifo cha Kanumba Bungeni? Je Kanuni za Bunge zinaruhusu kuwafanya Wabunge kusimama kwa dakika moja kwa ajili ya heshima ya kumbukumbu ya marehemu Kanumba? Aliyekuwa Inspekta Jenerali wa Polisi Haruni Mahundi aliyefariki muda mfupi kabla ya Kanumba na kuzikwa muda mfupi kabla ya Kanumba mbona hakupewa heshima aliyopewa Kanumba na Mheshimiwa Spika wa Bunge letu. Nilidhani kwa kuwa alikuwa mtumishi wa umma na aliyestaafu kwa heshima zote za jeshi la Polisi naye pia alistahili basi kutajwa sambamba na Kanumba ili naye apewe heshima inayostahili.Wanaofahamu vema kanuni za Bunge tupeni elimu ya uraia kuhusu jambo hili. Vinginevyo kesho anaweza kufa mtu wa bongo fleva akapewa heshima na Bunge letu kama Kanumba. Hivi hawa wa Bongo fleva na Bongo Muvi ndo watu sana katika nchi hii kuliko wengine au Mama alizidiwa na mahaba kwa kijana akajikuta maneno yanamtoka tu?
   
 4. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #4
  Apr 11, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  CCM na bunge la wasanii tu,
   
 5. H

  Huihui2 JF-Expert Member

  #5
  Apr 11, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Wonders will never end in this country, jana kwenye TBC1 kipindi cha Habari ya saa 2 jioni nilitamani kupasua TV ya nyumbani kwangu nilipoona item ya kwanza ya news ni mazishi ya Kanumba, then Mpiganaji aliyetetea taifa lake kwenye vita dhidi ya Nduli Iddi Amin Dada mwaka 1978-79 na hatimaye kuwa CDF kipindi cha awamu ya Rais Alj H Mwinyi, marehemu Ernest Mwitta Kiaro anakuwa item number 2
   
 6. Mr.Professional

  Mr.Professional JF-Expert Member

  #6
  Apr 11, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,602
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  itatolewa kesho kwa maelekezo yaliyotolewa na Naibu wa speaker
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Apr 11, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Zitto wa CDM kawakumbusha!
   
 8. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #8
  Apr 11, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Mawazo yangu yapo kwenye pesa. Je na serikali nayo itatoa Ubani wa Milioni 10?
  Yangu Macho!

  I wish Serikali itatoa Milioni 20 kutokana na mchango wa huyu Comrade!
  Kama serikali imetoa Sh. 10 mil. kwa Kanumba aliyepeperusha bendera kupitia sanaa ya filamu, sembuse mtu aliyeipigania nchi hii kutokana na uvamizi wa Nduli Idd Amin Dada!
   
 9. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #9
  Apr 11, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,787
  Likes Received: 36,792
  Trophy Points: 280

  kanumba anaingia ktk kundi lipi kati ya haya uliyoorodhesha hapa?
   
 10. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #10
  Apr 11, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hii nichi huwa haina vipaumbele, haiujui inataka nini haswa na nini maslahi ya taifa?
  Kulikuwa na sababu gani ya kugharamia mazishi ya kanumba? tutagharamia ya wasani wooteee?
   
 11. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #11
  Apr 11, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  kanumba 10+15m
  mahundi...?
  Kyaro...?
  Maana hawa wote walikuwa wakuu wa majeshi...jeshi ka wasanii..la polisi na JWTZ
   
 12. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #12
  Apr 11, 2012
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  amesahau kuweka kundi la frimasoni na supastaa wa bongo muvi :heh::heh::heh:
   
 13. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #13
  Apr 11, 2012
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160

  kwani generali yeye ni frimasoni hadi apewe 10m??
   
 14. K

  KAFWIMBI Member

  #14
  Apr 11, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Labda sum huwa inatajwa tu kunogesha sherehe then mshiko hatolewi kwa kuwa wanajua hawa Bongo muvi na ndugu zao wa Bongo fleva hata wasipopewa mshiko watakwenda kudai wapi? Mfano mzuri ni pale yule mnyapara wa shughuli za serikali Bungeni a.k.a mtoto wa mkulima alipotoa ahadi ya kuwapa 10M wanandinga wa T stars si mnakumbuka alivyowayeyusha mpaka jamaa walipotanganza mgomo wa kimya kimya ndo tunasikia zimetolewa lakini matumizi yamebadilika. Hawa ndo viongozi wa Bongo
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  Apr 11, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,564
  Likes Received: 18,298
  Trophy Points: 280
  Zitto kakumbushia, pamoja na dakika moja ya Mahundi.

  Naibu spika kichwa kizito sana!. Eti anasubiri taarifa ndipo kesho wataanza kwa one minute silence!.

  Kikao cha kesho asubuhi kitakuwa moto sana
  1. Kitaanza kwa one minute silence ya Kiaro na Mahundi.
  2. Hati za kuwasilishwa mezani ni taarifa ya CAG!.
  3. Nasari na mwenzake kuapishwa.
  4. Waziri Mkuu kikaangoni katika maswali ya papo kwa papo.
  5. CAG press confetence!.
   
 16. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #16
  Apr 11, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Naibu Speaker kaniacha hoi, a minute of silence needs to wait for what??
  Hawa CCM hata wakikumbushwa jambo badala ya kushukuru wanakuwa vichwa ngumu
   
 17. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #17
  Apr 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Acheni wabunge wafanye kazi tulizowatuma sio kuomboleza vifo vya kila mtu tafadhari!

  Ila naamini ni sahihi pale anapotokea mtu maarufu na mwenye mchango mkubwa katika taifa apewe heshima yake.

  Angalia umati uliomzika kanumba zaidi ya watu 600 wamepoteza fahamu, jamaa maarufu anadeserve heshima ya bunge.
   
 18. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #18
  Apr 11, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Nchi hii hufanya mambo bila kuyapangilia na ndio maana kila kitu ni kwa mtindo wa dharula kwasababu katika dharula hizi hawa wezi ndio wanakiuka taratibu na kupata mwanya wa kufisadi. Nakumbuka mara nyingi akifa kiongozi wa juu nchini wazo la kuwa na mahala maalum pa kuwazika hawa viongozi huzuka lakini mara tu baada ya mazishi hoja hiyo hupotea mpaka atakapokufa mwingine!! Kuna umuhimu wa kuwa na HERO'S acre mahala ambapo watu waliolitumikia Taifa kwa uadilifu watahifadhiwa pamoja na hata kuwa rahisi kuwakumbuka tunaposhehrekea siku ya mashujaa. Serikali haina budi kutekeleza ahadi inazotoa kwa wananchi badala ya kutegemeai kuwa wasipozitekeleza wadanganyika watasahau!
   
 19. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #19
  Apr 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Pasco umekuwa kipofu!
  Ina maana wewe hujui kanuni za bunge?
  Bunge lina taratibu zake kupokea taarifa rasmi FULL STOP.
  sijaona tatizo kwa naibu spika
   
 20. N

  Ningu Member

  #20
  Apr 11, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Taarifa rasmi maana yake nini? huyo ni General bwana rtd & R.I.P kwa hiyo kuna haja, tena haja kubwa ya kusimama!!!
   
Loading...