Nasubiri Baraza Kuu-Hamad Rashid

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,322
33,126
Hamad Rashid 1(5).jpg
Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed

Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed, ambaye yeye na wenzake 14, wamo kwenye msuguano mkubwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, kuhusu uongozi, atakwenda kwenye kikao cha dharura cha Baraza Kuu la Uongozi wa chama hicho Taifa, akiamini ndicho chombo kisichokuwa na utata.
Hamad, ambaye pia ni mjumbe wa baraza hilo, alisema hayo alipozungumza na NIPASHE jana, ikiwa ni siku moja tangu Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Tanzania Bara, Julius Mtatiro, kutangaza kuitishwa kwa kikao hicho cha dharura kinachotarajiwa kufanyika mjini Zanzibar keshokutwa.
Mtatiro alisema hayo baada ya kumalizika kwa kikao cha siku mbili cha Kamati Tendaji ya CUF Taifa, iliyopokea na kujadili taarifa ya hali ya kisiasa ndani ya chama kutoka Kamati ya Ulinzi na Usalama ya chama hicho.
Hamad alisema tofauti na Kamati ya Nidhamu na Maadili ya CUF, ambayo aliipinga kwa vile haimo kikatiba, Baraza Kuu liko kikatiba ya chama.
“Tutakwenda kwenye Baraza Kuu. Hivyo, tunaamini litatupa tuhuma tunazotuhumiwa, kwani niliomba kwenye hiyo kamati ya nidhamu na maadili kwa maandishi, lakini sijapewa,” alisema Hamad.
Alisema akishakabidhiwa tuhuma hizo na Baraza Kuu, anatarajia litageuka kuwa kamati ya maadili na kumhoji.



CHANZO: NIPASHE
 
Huyu jamaa naona yuko sawa, CUF si chama cha upinzani sasa...ni bora yy na wenzake waanzishe chama cha upinzani zenj....japo naona anafanya hivyo baada ya kutopewa ulaji ulitokana na ndoa ya CCM na CUF.
 
Tatizo la huyu jamaa ni uroho au ulafi, yupo tayali kula hata bila kunawa!
 
Back
Top Bottom