Nassari wa Arumeru Mashariki kushtakiwa kwa uhaini? Anatafutwa na Polisi

Kisheria kuna maneno yakitamkwa ni uhaini inategemea kama kauli zake zinaangukia katika matamshi ya uhaini.

Ni muhimu kuchunga maneno kabla ya kutamka.

Hapo ndipo Polisi watakapomng'ang'ania na kumfikisha mahakamani kupata tafsiri ya kisheria.

Nape mbona walimuacha aliposema hii nchi ina wenyewe na wenyewe ni CCM?au ndio kusema tunatumia kale kamsemo ka kunya anye kuku akinya bata kaharisha?
 
kusema tahamasisha wajitenge kama serikali haitatekeleza madai sidhani kama ni uhaini
tafsiri halisi ya uhaini.
ni njia ya kuitaka serikali ifanye hivo sidhani kama inahusika kwa njia yoyote ktk kumgoa rais au kumuua
 
Amesema kama serikali itaendelea kuwanyanyasa watajitenga wakajitangazie uhuru wao kama Darfur.
Sasa wanasheria wanaweza kusaidia tafsiri ya neno kama likiwekwa hapo implication yake ikoje!

kwani Darfur imejitenga!
 
I think Nassari alichemka kusema maneno kama yale

Hata kama tunakua na mzuka, kuna vitu hatuwezi kusema

Ila bado sidhani kuna haja ya kusema afunguliwe kesi ya uhaini, ushabiki huo upo

WAWAFUNGE WAZANZIBARI WOTE BASI KWA KUKATAA MUUNGANO KAMA WANAWEZA
 
kuna mambo ya msingi huwa yanafanyika na hakuna anayesema lakini yakisemwa na watu walio tofauti inakuwa issue.
Ni mara ngapi wanasiasa wameongelea mambo ya maeneo na ukanda? ...cha msingi ni kuwa kila mtu anastahili kuelezea kilicho moyoni mwake kwa japo saa nyingine kinaweza kuudhi wengine.

Mbona Mzee Mkapa aliposema vyama vya upinzani ni takataka na wapuuzi, wasipewe kura hakuchukuliwa hatua!? maana vipo kwa mujibu wa sheria.

Ukianza kuona haya mambo yanaongelewa majukwaani basi ujue yameshaanza kuingia kwenye nyoyo za watu na badala ya serikali kumkamata aliyesema ni bora waende kwenye mizizi ili kuangalia ni kwa nini yasemwe katika utawala wa sasa na sio nyakati zilizotangulia za uongozi!?
Mkuu nashangaa sana. Mbona wale UVCCM wa pwani walitamka mambo ya ukanda lakini hawajakamatwa? Au kwa kuwa Nasari amegusa palepale?
 
"Kanda ya Kaskazini kujitenga iwapo serikali itaendeleza manyanyaso na uonevu dhidi ya wadai haki, demokrasia na usawa kwa wote".

Kwani hata mwanamke akitelekezwa anafanya nini? Zingatia neno iwapo, Hata Tanu ndivyo ilivyofanya kwa muingereza, alipowanyima haki watanganyika.Na sudani kusini waliponyimwa haki na kaskasini. Issue ya vurugu, vita NK haipo hapa. Wanaweza kwenda UN na Kuthibitisha ukandamizaji kama upo.

Statement nyingine ni za kutoa angalizo tu. Msitafute wahaini, wakati kule migodini tunapata asilimia 4, na wananchi wetu kule ni choka mbaya.
I like this.....!
 
Wanasakwa?

Mbona jana kuna thread iliyopandishwa na ikisema wamekamatwa wote watatu na wanahojiwa?
Leo tena wanasakwa. Hii serikali ya ccm inaonyesha dhahiri karibu sasa wanakata roho.
huwa taarifa za hapa JF sio za kuaminika tena pameshakuwa kijiwe cha porojo huyo anasema wanahojiwa huyu anasema wanatafutwa MODS wanalala hawafanyi kazi yao ndio maana kila upuuzi unawekwa hapa!!!
 
Wadau,

Kuna tetesi kutoka vyanzo vya kuamini kutoka ndani ya jeshi la polisi Arusha kuwa huenda Mbunge kijana wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari aliyeibuka mshindi dhidi ya mgombea wa chama cha magamba (CCM), Sioi Sumari, akashtakiwa kwa kosa la uhaini kwa kudaiwa kuchochea Kanda ya Kaskazini kujitenga iwapo serikali itaendeleza manyanyaso na uonevu dhidi ya wadai haki, demokrasia na usawa kwa wote.

Nassari anadaiwa kutoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya NMC, Unga Ltd Jijini Arusha ambapo hivi sasa anasakwa kwa udi na uvumba na jeshi la polisi kwa mahojiano.

Pamoja na Nassari, polisi pia imetangaza kuwasaka Mwenyekiti wa vijana Chadema, John Heche na Ally Bananga aliyejiengua kutoka CCM na kujiunga Chadema hivi karibuni.

Bananga na Heche inadaiwa ni chambo tu katika juhudi za kumshughulikia Nasaari ambaye ushindi wake unadaiwa kuwakera wakubwa serikalini ambao wameingiwa hofu kutokana na Chadema kuendelea kupata umaarufu sehemu mbalimbali nchini.
mbona anaedelea na shughuli zake kama kawaida,unakuza mambo usiyoyafahamu!!
 
Nasari naye anaonekana akili haijakomaa bado. Ana kauli ambazo hazina mantiki kabisa.

kauli kama hizo ziliwahi kutolewa mara kadhaa early seventies au late sixties na wabunge wa mikoa ya kusini lakini hakuna aliyefunguliwa kesi ya uhaini.
 
POLE SANA KADA WA CCM KWA NINI USIENDE KUFANYA KAZI TBS1?AU GAZETI LA UHURU HUMU UNAPOTEZA MUDA:israel:MHHHH UNALO HILO
Du!
Hatukujua kuwa JF ni kijiwe cha CDM, lakini mjue hapa mnapata ushauri wa bure.
Kwa sasa hivi msaidieni mawazo kijana wenu asije ishia lupango kwa kutamka maneno yasiyotamkika.
Tulisema sana na kushauri juu ya Lema, soo alilolipata mnalalamika.
Tatizo lenu mnafikiri CDM ina gia ya kwenda mbele tu.
Ngoma ikilia sana.......malizia!
 
mbona zanzibar kila siku wanasema wanataka wajitoe wawe nchi yao wenyewe lakini hawakamatwi?? zanzibar na arusha tofauti yao nini?? yote ni mikoa ya tanzania??:doh:
 
kuna mambo ya msingi huwa yanafanyika na hakuna anayesema lakini yakisemwa na watu walio tofauti inakuwa issue.
Ni mara ngapi wanasiasa wameongelea mambo ya maeneo na ukanda? ...cha msingi ni kuwa kila mtu anastahili kuelezea kilicho moyoni mwake kwa japo saa nyingine kinaweza kuudhi wengine.

Mbona Mzee Mkapa aliposema vyama vya upinzani ni takataka na wapuuzi, wasipewe kura hakuchukuliwa hatua!? maana vipo kwa mujibu wa sheria.

Ukianza kuona haya mambo yanaongelewa majukwaani basi ujue yameshaanza kuingia kwenye nyoyo za watu na badala ya serikali kumkamata aliyesema ni bora waende kwenye mizizi ili kuangalia ni kwa nini yasemwe katika utawala wa sasa na sio nyakati zilizotangulia za uongozi!?

Naunga mkono hoja!
 
Back
Top Bottom