Nassari wa Arumeru Mashariki kushtakiwa kwa uhaini? Anatafutwa na Polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nassari wa Arumeru Mashariki kushtakiwa kwa uhaini? Anatafutwa na Polisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kowakdengo, May 7, 2012.

 1. K

  Kowakdengo Member

  #1
  May 7, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau,

  Kuna tetesi kutoka vyanzo vya kuamini kutoka ndani ya jeshi la polisi Arusha kuwa huenda Mbunge kijana wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari aliyeibuka mshindi dhidi ya mgombea wa chama cha magamba (CCM), Sioi Sumari, akashtakiwa kwa kosa la uhaini kwa kudaiwa kuchochea Kanda ya Kaskazini kujitenga iwapo serikali itaendeleza manyanyaso na uonevu dhidi ya wadai haki, demokrasia na usawa kwa wote.

  Nassari anadaiwa kutoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya NMC, Unga Ltd Jijini Arusha ambapo hivi sasa anasakwa kwa udi na uvumba na jeshi la polisi kwa mahojiano.

  Pamoja na Nassari, polisi pia imetangaza kuwasaka Mwenyekiti wa vijana Chadema, John Heche na Ally Bananga aliyejiengua kutoka CCM na kujiunga Chadema hivi karibuni.

  Bananga na Heche inadaiwa ni chambo tu katika juhudi za kumshughulikia Nasaari ambaye ushindi wake unadaiwa kuwakera wakubwa serikalini ambao wameingiwa hofu kutokana na Chadema kuendelea kupata umaarufu sehemu mbalimbali nchini.
   
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Wanasakwa?

  Mbona jana kuna thread iliyopandishwa na ikisema wamekamatwa wote watatu na wanahojiwa?
  Leo tena wanasakwa. Hii serikali ya ccm inaonyesha dhahiri karibu sasa wanakata roho.
   
 3. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,085
  Trophy Points: 280
  kuna mambo ya msingi huwa yanafanyika na hakuna anayesema lakini yakisemwa na watu walio tofauti inakuwa issue.
  Ni mara ngapi wanasiasa wameongelea mambo ya maeneo na ukanda? ...cha msingi ni kuwa kila mtu anastahili kuelezea kilicho moyoni mwake kwa japo saa nyingine kinaweza kuudhi wengine.

  Mbona Mzee Mkapa aliposema vyama vya upinzani ni takataka na wapuuzi, wasipewe kura hakuchukuliwa hatua!? maana vipo kwa mujibu wa sheria.

  Ukianza kuona haya mambo yanaongelewa majukwaani basi ujue yameshaanza kuingia kwenye nyoyo za watu na badala ya serikali kumkamata aliyesema ni bora waende kwenye mizizi ili kuangalia ni kwa nini yasemwe katika utawala wa sasa na sio nyakati zilizotangulia za uongozi!?
   
 4. M

  MWIGOLA Senior Member

  #4
  May 7, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 172
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Mbowe si alirkebisha hili palepale jukwaani? au bado lipo
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  May 7, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Amesema kama serikali itaendelea kuwanyanyasa watajitenga wakajitangazie uhuru wao kama Darfur.
  Sasa wanasheria wanaweza kusaidia tafsiri ya neno kama likiwekwa hapo implication yake ikoje!
   
 6. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Mbona waliposema rais hatatoka kaskazini uvccm chairperson bagamoyo hawajamkamata,mbona aliyeandika bango la MBEYA NCHI RAIS SUGU hawajamkamata,sema wanataka kuendeleza agenda ya kuwapa kesi kama lema ili asipate kuonekana jimboni bt wanampa umaarufu.
   
 7. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Kisheria kuna maneno yakitamkwa ni uhaini inategemea kama kauli zake zinaangukia katika matamshi ya uhaini.

  Ni muhimu kuchunga maneno kabla ya kutamka.

  Hapo ndipo Polisi watakapomng'ang'ania na kumfikisha mahakamani kupata tafsiri ya kisheria.
   
 8. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Hawa polisi wetu sijui wataelimika lini,nawashauri wasome hukumu ya kesi ya Mtikila aliyoshitakiwa kwa kuiita CCM majambazi,manguruwe etc, pia wasome hukumu ya kesi ya Kasanga Tumbo aliyeshitakiwa kwa kuhamasisha watu wajichuklie hatua mikononi na kuwaua wezi wanapowakamata, ndipo watajua kutofautisha kauli za wanasiasa na misemo waitumiayo kwenye jamii,otherwise mnawapa wapinzani chati kwa kuwafungulia kesi ambazo msiho wake wnashinda na kuonekana heroes kwenye society.

  Wakoloni walipotaka kumtawaza Kenyata kama mrithi wao waliona itakuwa ngumu kwani hakuwa shujaa kwenye jamii yake na hakushriki kwenye MAUMAU kama walivyoshiriki mashujaa wa Kenya kama Dedan Kimathi,njia waliyotumia wakoloni wali negotiate na Kenyata wajifanye wamemfunga na kufungwa kwake kutangazwe kwa nguvu kisha wamueachie na tayari watakuwa wamemfanya shujaa wa Kenya sawa na walio piganna MAUMAU.

  Ndicho wakoloni walichofanya na hatimae kumpa uraisi bila wanachi kujua mchezo wenyewe. Ukimfunga au kumkamata mtu unampa popularity; refer to Mandela. Be of your age, msiwape watu popularity bila wao ku struggle.
   
 9. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Polisi wanachokitafuta kwa Nassary na Wameru watakipata soon..wewe subiria tu.. nawashauri waachane na mbinu yeyote maana Polisi wakicheza faulo wanaweza jikuta wanasababisha alichokitamka Nassary
   
 10. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Mh hili nalo tatizo tungoje tuone watawafanya nini ,ilia wanatakiwa kuwa makini maana maneno hayo yangetamkwa na gamba hamna shida ila kwao inakuwa nongwa.
   
 11. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #11
  May 7, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  There might be a point here...................
   
 12. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #12
  May 7, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Nasari naye anaonekana akili haijakomaa bado. Ana kauli ambazo hazina mantiki kabisa.
   
 13. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #13
  May 7, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Nassari nitakwenda kumtetea...
   
 14. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #14
  May 7, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  "Kanda ya Kaskazini kujitenga iwapo serikali itaendeleza manyanyaso na uonevu dhidi ya wadai haki, demokrasia na usawa kwa wote".

  Kwani hata mwanamke akitelekezwa anafanya nini? Zingatia neno iwapo, Hata Tanu ndivyo ilivyofanya kwa muingereza, alipowanyima haki watanganyika.Na sudani kusini waliponyimwa haki na kaskasini. Issue ya vurugu, vita NK haipo hapa. Wanaweza kwenda UN na Kuthibitisha ukandamizaji kama upo.

  Statement nyingine ni za kutoa angalizo tu. Msitafute wahaini, wakati kule migodini tunapata asilimia 4, na wananchi wetu kule ni choka mbaya.
   
 15. a

  andrews JF-Expert Member

  #15
  May 7, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  POLE SANA KADA WA CCM KWA NINI USIENDE KUFANYA KAZI TBS1?AU GAZETI LA UHURU HUMU UNAPOTEZA MUDA:israel:MHHHH UNALO HILO
   
 16. agatony8l

  agatony8l JF-Expert Member

  #16
  May 7, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  nAUNGA MKONO HOJA
   
 17. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #17
  May 7, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Hapa umechangia jambo la maana. wakati mwingine kichaa kinapandaeee!!!
   
 18. Quanta

  Quanta Member

  #18
  May 7, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 55
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 15
  Tatizo serikal ni ya kihuni! Policcm wao hawana akli nzuri,mbona magamba yanaropoka 2. Ccm die 4reva & ever
   
 19. Suzie

  Suzie JF-Expert Member

  #19
  May 7, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 1,264
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Huna lingine kichwani kwako ukalifungulia uzi?? Unatafuta mtu alipopaliwa ndo umkalie kooni2mbu tupishe tunasonga nyie mmekalia majungu tu
   
 20. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #20
  May 7, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,272
  Trophy Points: 280
  Sugu Rais wa Mbeya!!
   
Loading...