Nassari kutoka Machinga hadi kuwa Mbunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nassari kutoka Machinga hadi kuwa Mbunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, May 21, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  [​IMG]

  Naye Mbunge Nassari, aliwataka wananchi wa jimbo hilo ambao kwa sasa wako katika harakati za kupigania kurejeshewa ardhi, kuwa na maono (vision) juu ya matumizi yake ili kuepuka kuja kuiuza kwa watu wengine na tatizo la ardhi likabaki palepale.
  “Hata wananchi wa Arumeru Mashariki nimewaeleza kuwa, wanaelekeza juhudi kubwa kuhakikisha tunarejeshewa ardhi, lakini kama hatuna maono, tutajikuta ardhi hiyo imeuzwa yote, kwani tunaihitaji kwa ajili ya shule, zahanati, vyuo vya ufundi au maeneo ya watoto wetu kucheza,” alisema Nassari.


  Alisema kuwa aliamua kutoa sadaka ya kumshukuru Mungu kwa mambo makuu aliyomtendea kabla ya kuanza ziara kwa wapiga kura wake, ambao wamekuwa wakimuita kwenye vijiji 86 vya jimbo hilo, kwani Mungu alimlinda kipindi chote, hata wakati wa kampeni magari yao matatu yalipata ajali kwa kuanguka, lakini hakuna aliyeumia huku yeye akiibuka na ushindi kwenye uchaguzi.


  Mbunge huyo kijana alisema kuwa, alikuwa na maono ya kuongoza toka akiwa mdogo, na kwamba alichofanya ni kupigana kuhakikisha anafikia ndoto hizo, licha ya hali ngumu ya kiuchumi kwenye familia yao,
  kiasi cha kumlazimisha akiwa na miaka 9 kuuza machungwa soko kuu la Arusha kila alipokuwa akitoka shule na mifuko ya plastiki kwenye soko la Tengeru na Mbauda.
   
 2. Medical Dictionary

  Medical Dictionary JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 1,053
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  kwakweli meru hatujawahi kupata mbunge kama huyu...long live nassari
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wengi wetu tumetokea huko, kuvaa lubega na kuchunga ng'ombe au mbuzi, kuuza lambo barabarani, wakati wa likizo shule inapofungwa kufanya vibarua kujipatia pesa kidogo kwa ajili ya kununulia madaftari na kalamu, au kuuza machungwa. Mama zetu kupika pombe na kuuza vilabuni ili kutusomesha.

  Leo tupo tulipo, tusisahau kusema ukweli tulikotoka maana kwa njia hiyo tunawapa moyo vijana wenzetu wanaohangaika kutoka pale walipo na tuwape moyo wasikate tamaa kwani yataka tu moyo.

  Watu waliotokea mazingira kama hayo wana uwezo wa kupenya kila hali ya maisha hata yawe magumu namna gani kwani wameshazoea taabu.
   
 4. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Asante! maneno mazuri sana...... lazima watanzania waelimishwe umuhimu wa kumiliki ardhi na athari za kuuza kwa wageni
   
 5. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ukimuona maskini anashabikia Ccm nenda kampime akili!
   
Loading...