Nasikitika kusema, baada ya miaka 13 kwenye ndoa leo mimi na mke wangu tumetalakiana

Ni kama hamna ndugu. Maana kila mmoja amelikinai hilo tendo kwa mwenzie. Lipo kwa mbali kama kubakana tu ili kutimiza wajibu.

Nilichokifanya ili kujiokoa na kuuweka sawa moyo usipitie majeraha makubwa,ikanibidi nifungue duka wilaya nyingine na tulipo mkoani.

Kwa hiyo muda mwingi namalizia huko shop. Naweza nikawa huko wiki na home siku 3,au 4 sababu ya watoto.
mkuu pole sana, maisha yanakuwa magumu sana...yaani kukaa nyumbani inakuwa kama jehanamu vile.
 
Ukiona nyumbani kwako kwa familia yako mwenyewe huna hamu ya kumaliza kazi zako uende kwako badala yake unatamani jioni isifike ili uendelee kuwa mbali na nyumbani kwako kwasababu ya KERO za mke / mume, moja kwa moja ndoa inakuwa mashakani
 
Ni kama hamna ndugu. Maana kila mmoja amelikinai hilo tendo kwa mwenzie. Lipo kwa mbali kama kubakana tu ili kutimiza wajibu.

Nilichokifanya ili kujiokoa na kuuweka sawa moyo usipitie majeraha makubwa,ikanibidi nifungue duka wilaya nyingine na tulipo mkoani.

Kwa hiyo muda mwingi namalizia huko shop. Naweza nikawa huko wiki na home siku 3,au 4 sababu ya watoto.
Daah pole sana kamanda, wahenga tunaelewa hiyo hali
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wewe ndio mafala duniani. Kama unampenda bado mpaka kukuliza kwa nini unamuacha?. Mimi nilijua unaweka sherehe kabisa kufanikisha kufikia kitu kigumu Talaka??.

Mimi natamani hata kufikia leo Talaka,lakini mwanamke huyu ni king'ang'anizi hatari. Nimetumia kila njia nifikie hatua uliyofikia wewe.

Mpaka siku nikabeba vitu vyote ndani na loli nilimwambia ndio nakupeleka kwenu na vitu vyote vya humu ndani. Aliita watu wote ninaofahamiana nao mpaka wachungaji sio kwamba anaomba samahani ili tu wasuruhishe abaki. Nimesema kwamba kuomba samahani mke ni jeuri,kiburi. Tunaweza tukakaa hata miezi mi3 amenuna tu. Tunaishi kama jehanum karibia mwaka wa 15. Kuachana ndio hataki kabisa.

Mimi nikifikia hatua uliyofikia wewe ni sherehe. Sitarudi nyuma kumfikiria hata nusu,. Halafu sitaoa tena maisha yangu yote yaliyobakia.

Kuoa ndoa za kikristo ni shida sana...ndoa ya kiislam ndio sahihi
 
Ukiona nyumbani kwako kwa familia yako mwenyewe huna hamu ya kumaliza kazi zako uende kwako badala yake unatamani jioni isifike ili uendelee kuwa mbali na nyumbani kwako kwasababu ya KERO za mke / mume, moja kwa moja ndoa inakuwa mashakani
Absolutely
 
Ni mtu ambaye niliishi naye miaka kumi na tatu na tulibahatika kupata watoto wanne. Ila leo mama Agness nimempa talaka mahakamani bila kupenda. Imeniuma sana nilimzoea sana mke wangu.

Mama Agness ameniliza sana. Daaah talaka inauma sana kwa mtu uliyemzoea. Nimemuuzi mtu niliyempenda. Ndiyo hivyo tena hatimaye mimi na mke wangu leo mwendo tumeumaliza.

Huwa nawaza sana watoto kwenye hii hatua.
Mungu asimamame kurejesha amani kwenye ndoa aisee.
 
Ni yule uliyemhonga 7800, ooh! Nimecoment kabla sijasoma.
Ni mtu ambaye niliishi naye miaka kumi na tatu na tulibahatika kupata watoto wanne. Ila leo mama Agness nimempa talaka mahakamani bila kupenda. Imeniuma sana nilimzoea sana mke wangu.

Mama Agness ameniliza sana. Daaah talaka inauma sana kwa mtu uliyemzoea. Nimemuuzi mtu niliyempenda. Ndiyo hivyo tena hatimaye mimi na mke wangu leo mwendo tumeumaliza.

Katika kipengele ninachokipenda katika dini ya Ukristo ni kile cha katazo la kutalikiana, Kama umewahi kupitia pito analopita mleta mada utadhibitisha hiki nisemacho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni mtu ambaye niliishi naye miaka kumi na tatu na tulibahatika kupata watoto wanne. Ila leo mama Agness nimempa talaka mahakamani bila kupenda. Imeniuma sana nilimzoea sana mke wangu.

Mama Agness ameniliza sana. Daaah talaka inauma sana kwa mtu uliyemzoea. Nimemuuzi mtu niliyempenda. Ndiyo hivyo tena hatimaye mimi na mke wangu leo mwendo tumeumaliza.

Nimepigia mstari "nimemuuzi mtu niliyempenda"--- Mara nyingi sisi wababa ni chanzo-- Pole sana mkuu! Tupo wengi tunaohangaika kutafuta suluhisho, kuachana na mtu uliyeishi naye zaidi ya miaka 7 inauma sana hata pale unapojiaminisha kuwa haumpendi tena!
Pole kwa mara nyingine
 
Back
Top Bottom