Nashukuru valentine day kuwa alhamis

Nashukuru valentine day kuwa alhamis

Gefu

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2010
Posts
6,929
Reaction score
2,567
Wadau wa jf,
Naweza nisieleweke kirahisi lakini kwa upande wangu namshukuru Mungu sana hii siku (ambayo bado sijui maudhui yake ni nini zaidi ya kuleta matatizo)kuwa katikati ya wiki. kwa hakika sehemu nyingi za fujo (ambazo wengine mnaita za starehe) zilikuwa na watu wachache na pengine hakukuwa na watu kabisa. Hili limesaidia sana kupunguza kelele na fujo ktk maeneo ninayoishi.

Sinahakika sana suala la tarehe,lakini nahisi nalo limechangia sana kupunguza hizi fujo. Pengine wadau wa jf ni moja ya waamini wa siku hii ya upendo(si mapenzi) ya msimu au upendo wa maua. Sijui msimu wa maua ukipita upendo kama utaendelea kuwepo. Anyway hebu ngoja nipate mtazamo topfauti,lakini kwangu siku hii sioni maana yake hasa nikilinganisha na uhalisia wa mambo,vitoto vidogo vinafanyiwa mambo ya ajabu, kisa valentine. Vibinti vinajirahisi kisa valentine. Oooh ! Mungu asante kwa kutuepusha na hili balaaa !
 
watu wengi wanaoponda siku ya valentine ni wale tulio single au tuliokua kwenye mahusiano lakini hatufurahii mahusiano hayo au wale tulowahi kutendwa siku ya valentine,:A S 100: ila kwa wale walio kua happy na watu wao jana ilikua shangwe na vigelegele!
 
Sijawahi kutendwa,na sijawahi kusherehekea hii siku simply because sijui maudhui yake, mimi na mpenzi wangu tunapendana kwa dhati tangu tulipokutana siku ya kwanza. Shida yangu ni hapo kwenye shangwe na vigelele,hata kanisani vinapigwa,lakini je,maudhui halisi ninini ? au kuishia kutenda uovu kwa jina la shangwe na vigelegele. Nisaidie dada Purple
 
Kwa kifupi ni kwamba tumeiga kwa walioanzisha kwa ajili ya kumuenzi jamaa yao. Tumezidi kuiga na tutaiga hadi ndoa za jinsia moja kuzibariki kwenye misikiti na makanisani siku moja. Ila Valentine day ina histori yake na ni kumbukumbu nzuri ila wengi wanaitumia vibaya kwa kufanya ukahaba.
Angalizo: Kufanya mapenzi kabla ya ndoa na au nje ya ndoa hayakubaliki na ni chukizo na dhambi mbele za Mungu.
 
ni siku ya kuonyesha upendo kwa njia ya kipekee zaidi, kila siku watu wanaonyeshana upendo but valentine ni siku special zaidi kama vile watu wanavyoweza kusheherekea birthdays, anivesaries, eid, christmass n.k, lakini pia hakuna aliyelazimishwa unaweza kuiacha kama ilivyo au unaweza kuichukulia kama ilivyo, all is well!
 
watu wengi wanaoponda siku ya valentine ni wale tulio single au tuliokua kwenye mahusiano lakini hatufurahii mahusiano hayo au wale tulowahi kutendwa siku ya valentine,:A S 100: ila kwa wale walio kua happy na watu wao jana ilikua shangwe na vigelegele!

heri ya wewe ulikuwa miongoni ya wale waliokuwa na bahati hiyo ya kujua hilo..
 
Back
Top Bottom