Nashindwa kustahimili hizi tabia, Ushauri wako ni muhimu sana

king suleman

JF-Expert Member
Jun 28, 2014
1,749
1,148
Habari wanajamvi.

Mimi nina matatizo kama mawili yananitatiza nashindwa kuacha.

Tatizo la kwanza, nina usingizi kupita kiasi yaani nawahi kulala ila nachelewa kuamka na hata nikienda darasani bado nasinzia. Kwenye discussion simalizi dakika 5 nasinzia na toka nipo o level nilikuwa hivi.

Tatizo langu la pili, nina tabia ya kuropoka yaani hadi najiona nakera ila nashindwa niacheje kwasababu najistukia. Nimesharopoka kila nikisema naacha muda huo huo mtu akiongea kitu mimi tayari nishajibu.

HIVYO BASI KWA MWENYE USHAURI USIPITE KIMYA TU.

Asanteni.

Nawasilisha.
 
Ha ha ha....unajua umenichekesha wapi??? pale kwenye uropokaji.. coz nimevuta picha unavyoropoka. kiukweli ni tatizo kwani inaweza kukupelekea kudharaulika.. jitahidi kufirikiri kwa kina kabla hujasema chochote.. kuhusu tatizo la usingizi hebu jitahidi kuamka mapema fanya mazoezi, pia kumbuka usingizi ukiuendekeza ni unaendekeza umasikini..
 
Habari wanajamvi,

Mimi nina matatizo kama mawili yananitatiza nashindwa kuacha,

Tatizo la kwanza, nina usingizi kupita kiasi yaani nawahi kulala ila nachelewa kuamka na hata nikienda darasani bado nasinzia. Kwenye discussion simalizi dakika 5 nasinzia na toka nipo o level nilikuwa hivi.

Tatizo langu la pili, nina tabia ya kuropoka yaani hadi najiona nakera ila nashindwa niacheje kwasababu najistukia. Nimesharopoka kila nikisema naacha muda huo huo mtu akiongea kitu mimi tayari nishajibu.

HIVYO BASI KWA MWENYE USHAURI USIPITE KIMYA TU.

Asanteni.

Nawasilisha.

aisee kuna jamaa tulikuwa naye darasani Olevel tulikuwa tunamuita Imma mropokaji..na alikuwa anaropoka kweli kweli..hiyo ni tabia mkuu huwezi kuiacha!!

ila usingizi jaribu kuweka ratiba yako vizuri!!
 
Ha ha ha....unajua umenichekesha wapi??? pale kwenye uropokaji.. coz nimevuta picha unavyoropoka. kiukweli ni tatizo kwani inaweza kukupelekea kudharaulika.. jitahidi kufirikiri kwa kina kabla hujasema chochote.. kuhusu tatizo la usingizi hebu jitahidi kuamka mapema fanya mazoezi, pia kumbuka usingizi ukiuendekeza ni unaendekeza umasikini..

Nice one , mdau fuata hii .itakusaidia .
 
usingizi hauna dawa mkuu ,....wewe pono tuu.

ila uropokaji sio fresh mtoto wa kiume

jitambue uache hiyo tabia cos mnakera sana
 
Umenikumbusha mbaali... Skul a'level,kuna kijana alikua anaropoka yaani hovyo tu, hujamaliza kuongea kashadakia... Pole
Jaribu kujicontrol

Usiendekeze usingizi utakuumbua...wah kuamka fanya mazoez, ukiuzoesha mwili hiyo hali itaisha
 
kuropoka ni vizuri ila uwe unaropoka point sio pumba

nimepata adhabu sana shule kwa ajili ya kuropoka
ila nimepunguza siku hizi
hii tabia haiachiki
 
kwenye usingizi, inaweza ukawa unachoka sana, (kiakili) hivo kupelekea ubongo unaopelka mawasiliano ya wewe kuwa active kushindwa kufanya kazi yake coz unakuwa over loaded! cha kufanya, punguza mawazo na jaribu kufanya k2 kinachokufanya uwe active ukiwa unasikia hali hyo, (your interest thing!) itakusaidia

kuhusu kuropoka aisee hyo ni tabia mbaya, na inategemea na mazingira yanayokuzungka! umejizoesha hvyo, acha!!
 
Jifunze kuacha kuropoka, usingizi wako unasababishwa na kutumia nguvu nyingi kwenye uropokaji, talking to much, mwanaume huongea maneno kati ya 15000-25000 kwa siku kwa tabia yako ya uropokaji we utakua unabonga up to 40000-50000 ambayo ni idadi ya maneno per day kwa wanawake. Jitahidi kuwa msikilizaji, zip it….
 
unapiga msuli mpaka saa ngapi? maana usije kuwa unalala saa tisa usiku halafu unataka uamke saa kumi na moja alfajiri??? anyway sie wengine na elimu zetu za mkoloni hizi discussion tulikuwatunahudhuria kipindi cha pepa tu kwa masaa machache, siku nyingine saa 4-5 tupo vitandani, kusoma sio vita

hiyo ya kuropoka mradi umegundua tatizo anza kujicontrol, maana hauwezi kuacha mara moja itachukua muda
 
Ubora wa maneno ni machache na yanayoeleweka. Na uzuri wa maneno ni mpangilio wake.Ukizingatia hili unaweza punguza kuropoka.

Kuhusu kulala sana, unaweza punguza kwa kupanga ratiba yako vyema
 
Mweeee mbona namie kuna mchizi tulisoma nae alikua anaitwa imma mropokaji hahahah na alikua anaropoka balaa na alikua ana misifa kweli, au ndo huyo nini?
aisee kuna jamaa tulikuwa naye darasani Olevel tulikuwa tunamuita Imma mropokaji..na alikuwa anaropoka kweli kweli..hiyo ni tabia mkuu huwezi kuiacha!!

ila usingizi jaribu kuweka ratiba yako vizuri!!
 
Back
Top Bottom