Ndio hivyo tangu nimwagane na wife niliempenda sana,3year ago.Nashindwa kupenda tena kila ninaekutana nae naona ndio yuleyule tu.
Advice me please.
Kadri unavyozidi kumpenda mtu sana basi na ndivyo unavyozidi kuchelewa kumsahau.ukimpenda sana mtu alafu mkatengana ghafla baasi itachukua muda sana kukaa sawa na kumsahau kwa sababu alikaa hasa hasa moyoni.
Kinyume chake sasa..
Kama hukumpenda sana mtu basi kumsahau ni rahisi sana mkuu, kama mtu hukumpenda sana ghafla mkatengana basi inachukua muda mchache kumsahau.
Katika hali ya kwanza ile ya kumpenda mtu sana na kuchelewa kumsahau.hali hii ya kuchelewa kumsahau mtu ni ya kawaida sana kwa yule ambaye ghafla ametengana na ampendaye.
Usijaribu kupingana na hiyo hali mkuu, utakuwa umefanya maamuzi mabaya, huo ni upepo tu, hapo moyo wako unajirestoree upyaa.
Na kadri maumivu yako yanavyozidi pale unapomkumbuka basi ndivyo kuna asilimia fulani za kumbukumbu zinaondoka moyoni mwako juu yake. Acha uumie kwa ajili ya kuusafisha moyo wako asiwepo kabisa kwako.
Lakini jambo zuri ni kuwa, itakapotokea umekuja kumpata unayempenda zaidi ya huyo mliotengana, basi utakuja kumsahau mara moja,lakini kwa sasa ni nadra sana kumpata huyo ila ingetokea sasa hivi basi amini kwamba moyo ungeshamfuta yule na kumuweka huyu wa sasa hivi.
Relax mkuu, usijione kama haupo kawaida, hiyo ni kawaida katika maisha.
Muhimu usilazimishe kumpenda mtu kwa sasa, Acha itokee automatically umpende mtu pasi na kulazimisha na kutafuta tafuta yupi mzuri wa kumpenda.
Tulia, relax, fanya mambo yako, kila unapoumia jiambie kwamba haya maumivu ni kwa sababu moyo unafuta taswira yake ndani yangu....
Enjoy the life....