Nashindwa kumuacha sijui ni dawa?

Ndenji five

JF-Expert Member
Nov 1, 2021
1,985
3,083
Dah wakuu napitia kipindi kigumu kuna mwanamke nilianzisha mahusiano nae miaka kama mitatu nyuma

Sasa kipindi naanza nae mahusiano nilikuwa na kawaida ya kumpeleka gest tunafanya mambo yetu tunaishia

Mwisho wa siku nikaona huko gest pesa inakata pasipo sababu wakati gheto lipo na kakibanda ninako yaani nimepanga afu nimejenga nimepanga kutokana huwa napenda kubadili mazingira ya kuishi huwa sipendi kukaa sehem moja kwa mwaka mzima

Basi nilivyoona gharama zinateketea nikamfanyia saplaizi ya kumleta gheto mwanzo nilikuwa nasema gheto nimepewa kulinda la jamaa mimi na kaa kwa wazazi

Basi akawa anakuja kuja atafanya usafi nikilud toka kazini nakuta gheto limeng'aa nakuta tu ujumbe nilikuja mimi

Tumeenda miez ikapita mara akaja akawa ana tabia ya kujakukaa wiki mara mwezi

Mi hapo sina mchongo wowote kama naoa au vipi najua tu ndio hivyo amenisogezea huduma karibu

Nakuja kustuka mwaka ukapita nisikumbuke nilimwambia gheto la jamaa

Hadi kufikia hapo dem akawa kama kaota mizizi kama mimi ndio mumewake nakuta tu natembelewa na mashemeji

Nikaamua kumwambia nasafiri kikazi kumbe nakuja kwenye nyumba yangu naishi hata mwenzi narud tena gheto mara moja sasa kuanzia mwaka jana najikuta siwezi kukaa hom kwangu kwa siku mbili bila kumuwaza yeye hata kama nikisafiri siwezi kukaa wiki mbili bila kutamani kurudi

Licha ya mambo mengi ya ajabu aliyonifanyia kama kumwagiwa chai na kunisema kama mtoto mbele za watu lakini bado namkubali japo kuwa kazini wananijua nikichukia nakua vipi
Nishawahi nasa makofi mkurugenzi wangu na kuwekwa ndani ila kwa huyu mazi nakuwa bwege nikiwa nje ya ulingo mpaka najiona mpuuzi basi nakuwa na hasira nikifika pale napoa mwenyewe

kila nikijalibu kumtimua dem anakuwa king'ang'anizi ila sijawahi kumwambia kama nimejenga na nina wapangaji

wakuu hivi
Hili sio limbwata kweli na si kupanga kuoa mpaka niweke mambo yangu sawa ila nyege zimenisaliti nioe kabla ya muda
Wakuu
Nifanyeje kutoka hapa nilipo?


1642488040470.png

 
Back
Top Bottom