Nashindwa kumuacha sijui ni dawa?

Nashindwa kumuacha sijui ni dawa?

Dah wakuu napitia kipindi kigumu kuna mwanamke nilianzisha mahusiano nae miaka kama mitatu nyuma

Sasa kipindi naanza nae mahusiano nilikuwa na kawaida ya kumpeleka gest tunafanya mambo yetu tunaishia
Geto umepanga na una kwako,Demu anakufanya uwe na hangover hata kama Limbwata sasa wasi was wako ni nini?Huyo ndo baby mama wako mpaka further notice.
 
Nimechelewa kuchangia vipi ushamuacha??

Mkuu mi pia naamini limbwata lipo ila ni mara chache sana hufanikiwa kumteka mwanaume!!

Wewe hapo hujatekwa na limbwata ila ni utumwa. Ndio wewe ni mtumwa kwa huyo mwanamke, na mtumwa huwa ni ngumu sana kujikomboa sababu ana unyonge ndani yake, anahisi hawezi ashalishwa sumu ya kutojikubali bila mkuu wake. Ushakua addicted na the way anakutreat na ndio maana unaweza kuta mwanamke anapigwa na mumewe lakini haondoki, kwanini, ni hivo ashakua addicted akienda mahali hapigwi lazma ataibua tabia tofauti coz hajayazoea maisha hayo.
 
Mi nimeamua hivyo nataka nimuache nipe hatua ya pili
Njia sahihi ya kumuacha mtu ni kujifanya masikini,mshindishe njaa akimaliza siku mbili ajaondoka njoo nikupe mbinu nyingine ya kumuacha
 
Sipendi umuache ila wacha nikushauri,

Siku moja rudi nyumbani ukiwa unalengwalengwa na machozi,

akikuuliza "kulikoni?"

Mjibu "nimefukuzwa kazi" (ikibidi jitengenezee na barua ya kufukuzwa kazi ili jibu liambatane huku unamkabidhi barua),


Kisha mwambie "nataka tuhamie kijijini tukalime hivyo anza kujiandaa maana mwezi huu nafanya maandalizi ikifika mwisho wa mwezi tunahamia kijijini",

kisha anza kuhamisha vile vitu muhimu kama Music system, TV na Fridge hamishia kwenye nyumba yako na vingine ambavyo unajua unapokua nyumbani huwa unavitumia au yeye anapenda kuvitumia na vyenyewe hamishia kwenye nyumba yako akikuuliza unapeleka wapi mjibu, "nauza nipate hela ya kuanzia maisha"

Uwe unaenda kazini kama kawaida ila ratiba zako za kurudi home zibadilike muda mwingine uwe unawahi sana muda mwingine uwe unachelewa, pia omba likizo ya ugonjwa kisha shinda nae home ili ajue kwamba kweli huna kazi, kama unaweza andaa timu yako mmoja wa rafiki zako wampigie simu wamwambie umewekwa ndani (hapa inatakiwa kama vipi uongee na polisi wakulaze ndani kweli)
Kifupi utumie mbinu za kimafia

Asipoondoka na akionyesha anakupa moyo kukabiliana na matatizo uliyonayo MUOE huyo mwanamke maana kwa sasa katika wanawake mia moja yupo mmoja

Au kama vipi muulize, "sijakuoa unanimwagia chai je nikikuoa?" Kisha msikilize atakujibu nini, kama anajijua kakosea atakuomba msamaha ila akikujibu jeuri piga chini

FILISIKA UJUE TABIA ZA MKEO
 
Nataka nikwambie mleta mada mapenzi yanamazoea na ndipo upendo huweza kuota mizizi, demu ukikutana naye mara moja au mbil hata tatu huwezi kumuwaza kivile lakini mtu umefikia kulala nae mwezi n.k mchana woote mpo wote mnakula wote anatandika kitanda na hana kasoro zozote papuchi unakula kama yoote hakika mazoea na serious love inaanzia hapo utajikuta unamhitaji kila wakati.

Unajua mwanzoni waweza mhitaji mtu 7bu ya kukata kiu lakini muda unavyozidi kwenda inakwenda zaidi ya kiu kwamba unataka mke
 
Watu kama wewe mleta mada usipokuwa makini utakuja kujuta na kuteseka ktk suala zima la mapenzi kwa wazoefu wa maisha hakuna njia sahihi na inayoeleweka ya kumpata mke mwema kwani hata wale walofuata inayosemwa kuwa ni misingi ya kuoa wamekula za uso inawezekana huyo ndo mkeo na ukijifanya mjanja sana utakuja kuoa malaya wa ajabu na utamkumbuka huyu wa sasa na haitokusaidia kwani atakuwa kaolewa na anaejali,

Kama sifa anazo za kuwa mke weka ndani jitambulishe taratibu zifatwe uanze kuitwa baba huyo mwanamke unaemfikiria kwamba ndiye anaefaa kuwa mkeo yaweza kuwa ni illusion na hata kama yupo yawezakuwa naye huko aliko anakula mhogo wa jang'ombe kama wewe unavyomlisha mtoto wa watu.
Jambo jingine unajitafutia hatari kuishi na mtu mwaka mzima halafu unamuacha kisha unaoa mwingine acha huo upuuz anaweza kuondoka na shahawa zako na kuzipeleka mahala ukateseka ktk hii dunia hasa kama ataamua kufanye ile irreversible reaction
 
Dah wakuu napitia kipindi kigumu kuna mwanamke nilianzisha mahusiano nae miaka kama mitatu nyuma

Sasa kipindi naanza nae mahusiano nilikuwa na kawaida ya kumpeleka gest tunafanya mambo yetu tunaishia

Mwisho wa siku nikaona huko gest pesa inakata pasipo sababu wakati gheto lipo na kakibanda ninako yaani nimepanga afu nimejenga nimepanga kutokana huwa napenda kubadili mazingira ya kuishi huwa sipendi kukaa sehem moja kwa mwaka mzima

Basi nilivyoona gharama zinateketea nikamfanyia saplaizi ya kumleta gheto mwanzo nilikuwa nasema gheto nimepewa kulinda la jamaa mimi na kaa kwa wazazi

Basi akawa anakuja kuja atafanya usafi nikilud toka kazini nakuta gheto limeng'aa nakuta tu ujumbe nilikuja mimi

Tumeenda miez ikapita mara akaja akawa ana tabia ya kujakukaa wiki mara mwezi

Mi hapo sina mchongo wowote kama naoa au vipi najua tu ndio hivyo amenisogezea huduma karibu

Nakuja kustuka mwaka ukapita nisikumbuke nilimwambia gheto la jamaa

Hadi kufikia hapo dem akawa kama kaota mizizi kama mimi ndio mumewake nakuta tu natembelewa na mashemeji

Nikaamua kumwambia nasafiri kikazi kumbe nakuja kwenye nyumba yangu naishi hata mwenzi narud tena gheto mara moja sasa kuanzia mwaka jana najikuta siwezi kukaa hom kwangu kwa siku mbili bila kumuwaza yeye hata kama nikisafiri siwezi kukaa wiki mbili bila kutamani kurudi

Licha ya mambo mengi ya ajabu aliyonifanyia kama kumwagiwa chai na kunisema kama mtoto mbele za watu lakini bado namkubali japo kuwa kazini wananijua nikichukia nakua vipi
Nishawahi nasa makofi mkurugenzi wangu na kuwekwa ndani ila kwa huyu mazi nakuwa bwege nikiwa nje ya ulingo mpaka najiona mpuuzi basi nakuwa na hasira nikifika pale napoa mwenyewe

kila nikijalibu kumtimua dem anakuwa king'ang'anizi ila sijawahi kumwambia kama nimejenga na nina wapangaji

wakuu hivi
Hili sio limbwata kweli na si kupanga kuoa mpaka niweke mambo yangu sawa ila nyege zimenisaliti nioe kabla ya muda
Wakuu
Nifanyeje kutoka hapa nilipo?


Sio limbwata Wala nn.....muoe tu huyohuyo

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom