Nashindwa kumsaidia

Nashindwa kumsaidia

uongope uharibu ndoa kwa mtu wa nje tu..tena hana msaada kwenye ndoa yenu...acha uzoba..yena ilistahili umle kimya kimya tu ..sema basi....na acha u=kutetea uozo kisa kazi hayo hayakuhusu ya kazini kwao waachie wao we kuwa mkweli kwa mkeo....mke ni mke ni wa thamani sio hao wanaotaka kumkomoa wife kisa anaringa ...
 
Wana jamvi nina mke wangu ambaye ni HR katika kampuni fulani hapa Dar na mimi ni mfanyabiashara japo mambo yangu yameyumba sana kwa sasa hivyo wife ambaye ndio amepata ajira mwaka huu anaboost sana mambo ya familia na next week alipanga tuvute usafiri ili kurahisisha shughuli zetu na pia kumuwahisha kazini asubuhi

Juzi nilipokea ujumbe messenger kutoka kwa dada mmoja ambaye sikumfaham ila aliniomba namba ya simu akidai ana maongezi na mimi basi nikampatia namba nakupotezea

Asubuhi alinitafuta akiniuliza nipo wapi huku akitaka tuonane mida ya mchana kwa maongezi nae nilimwambia inabid nikufahamu kwanza vizuri before ya kukutana nawe lakini akanisihi nisiwe na shaka

Basi nilikutana nae maeneo aliyinielekeza na nilipofika niligundua hata yeye alikuwa hanijui kwani alinikaribisha kwa kusita kama hana uhakika na mimi, niliongea nae na akaweka wazi ya kuwa alikuwa amevutiwa na mimi kimapenzi akidai aliwahi niona nilipompelekea bidhaa moja ya wateja wangu ambaye ni rafiki ake.

Kwakwel sikukubaliana nae kwa pale nikamweleza wazi kuwa nina mke na ninampenda sana hivyo ni bora angetafuta mtu mwengne wa kuwa nae tuliachana japo hakuridhika na aliendeleza mawasiliano

Juzi alipiga simu na bahati mbaya simu ilikuwa kwa wife na namna nilivyosave ile namba ilimpa wasiwasi wife akaniletea simu nikaongea nae kawaida kama story sikutaka kumkazia ili wife asielewe chochote

Kumbe wife aliingiwa mashaka sana na aliichukua ile namba bila mimi kujua na alivyojaribu kuipiga akagundua ni ya mdada ambaye anamjua ni secretary wa ofisi yao na walikuwa close toka anaanza ajira pale ila hawakuwa na maelewano mazuri siku za hivi karibuni

Hivyo wife wangu akahoji imekuaje kuanza kuwasiliana nae na ni mahusiano gani yanayotuunganisha basi nikamwelezea wife ilivyokuwa akawa amechukia sana akasema atafanya kila namna huyu binti kumtimua kazini kwani ni wazi alifanya makusudi kwa kujua kwani walikuwa marafiki sana hapo awali

Nikamtafuta yule binti nikajaribu kumbana na kumweleza kuwa wife amechukua namba yake alishtuka sana na kusema nimsamehe kwan ni kweli alikuwa akijuana na mke wangu na ni boss wake lakini alitaka kumkomoa eti wife amekuwa mtu wa kuringa sana hapo ofisini akakiri na namba yangu alikuwa nayo before hajaniomba ila alizuga tu kupitia messenger ili isiwe rahisi kwangu kuelewa

Wife leo hakwenda kazini na alimpigia simu huyu dada zaidi ya mara 5 lakini hakupokea na hapa alipo kila nikijaribu kumshauri apotezee hili suala asimuharibie mtoto wa watu kazi ananiwakia anadai basi lengo letu ni moja

Huyu bint katuma meseji anajilaumu na ameingiwa na hofu na mimi nimeshndwa kumsaidia eti ananiomba nimwambie wife kuwa ni mimi niliemtafuta ili niokoe ajira yake mimi hapa nilipo sielewi wife toka jana hayupo sawa na amechukia hashauriki tena. Naomba mawazo yenu jamani namna ya kulimaliza hili soo bila huyu manzi kupoteza kazi na mimi ndoa yangu ibaki salama
Hii chai
Yeye huyo mwanamke kama aliamua kumkomoa bosi wake kwa kuringa maana yake alishajizatiti kwa chochote kitakacho toezea mbeleni.
 
Back
Top Bottom