Nashindwa kujielewa ni mimi tu 'nisiyependa kujichanganya na watu' au kuna wenzangu wapo hivi? Msaada tafadhali

Acha punyeto,
Huwezi amini punyeto humfanya mtu awe mbinafsi na mpenda faragha binafsi, hata akitembelewa na rafiki atatamani rafiki aondoke ili apate nafasi ya kujiburudisha.
If other factors remain constant, masterbation segregates a victim from socialization!
Sure kabisa
 
Huko atafukuzwa wiki hiyohiyo akifika. Hakuna malezi magumu kama ya upadre. Ukiwa mkimya sana utadhaniwa unaficha tabia ama jambo fulani. Na zaidi huo wito ni wa kutumikia watu je kama hata kuongea na watu ni shida je utume utafanyikaje?
Katika utume kuna kufinyangwa wito ukiwa sahihi atafanikiwa tu.

Paroko wetu kabla Kigango chetu hakijapewa hadhi ya kuwa Parokia teule na hatimaye sasa kuwa Parokia ,aliwahi kuwaelezea waamini kuwa. Yy katika maisha yake kabla hajawa Padre, alikuwa anapenda kukaa sehemu zenye Utulivu.

Daima maeneo ya kujichanganya hakupendelea, baada ya kumaliza Form Six alijishughulisha shughuli binafsi lkn ile khali ya kupenda utulivu.

Aliamua kwenda kusomea Upadre sehemu ambayo anajisikia Amani sana.

Maisha yao yenyekuhitaji ibada, mafungo na sala naamini atafurahia na kujisikia mwenye AMANI.
Kwa kuongezea kazi za kitume ziko nyingi kwa Mapadre.
 
Njia rahisi zaidi kuliko zote za kujichanganya na watu ni kununua njumu au Snickers za kuchezea basket then unaingia uwanjani. hakuna mwanaume atakaekufukuza uwanjani au kukukataza usiguse mpira. hapo utapata marafiki wengi, sometimes mnakua mnaamshana weekend mkafanye mazoezi, wengine wanakuadd hadi kwenye groups za whatsapp.
mkiwa na communication nzuri mnapanga hadi skukuu mkatembee wapi. Mnatengeneza Real brotherhood!
 
Aiseee mbona kama unanisema mimi kabisaa
Zipo NNE mkuu umesahau pragmatic personality hii ndio inamuhusu huyo dogo hii personality ndio ile hata ukitukanwa we huna habari hata hujibu

Hawajali na wala hawashituki hata ukitokea msiba wenyewe wanachukulia poa tu hata likipigwa Bomu pale watageuka then wanaendelea na ratiba zao

Pia wanahasira za karibu ila wanawahi kujirudi

Pia hawapendi zile kazi nzito na ngumu wao wanafanya kufukia mashimo

Pia kwenye mahusiAno hawatabiriki in Short they don't fail in love but sometime they fail only for sex
Hawa ndio wakisalitiwa solution wanakunywa sumu ya panya
 
Mimi ni introvert. Sikutumia dawa hata kidogo. Baada ya kuona nitakosa fursa nikajitahidi kusoma vitabu vya kujipa moyo na kujenga uwezo. Nikajiwekea utaratibu wa kujikwamua kwa kutumia mbinu mbalimbali.

Nakushauri soma vitabu vya kukusaidia. Usinywe dawa kabisa Jiwekee malengo ya kuondokana na hali yako. Amka kila siku na kutekeleza mbinu ulizojiwekea.

Waweza kumwona mtaalamu wa saikolojia ukiona umeshindwa kujisadia mwenyewe.
 
Mimi pia nipo ivoo tangu utoto.

Ni mtu wa kukaa pekeyangu sipend kabisa kukaa na watu kujichanganya.
Nimelelewa na wazazi wote wawili
Wamejitahid sana sana lkn bado.
Sipend kuongea adi inibidi
Ata mtu akinikosea siwez kumwambia
Sipendi kujichanganya ata ikitokea nkajichanganya for 2hr nahis naloose enegy

Iyo tabia imenipelekea kutokuattend kwenye vipind class kipindi nasoma
Ata discussion sikuwai fanya
Church nlikua sipendi kwenda

Mpaka sasa nnarafiki mmoja tu.

Napoishi sasa ni miaka 4 lakin sina ata jirani naeongea nae
Sina aibu ila sipendi watu
Mtu wa karibu sana kwangu ni gf basi

Ata familia yangu naongea nayo mara chache sana
Sijali sana watu na hiki ndo kinachoniumiza zaid.
Bt i think mzee wangu nae yupo ivi kama mim
 
Sometimes unasemwa kwamba unajiskia..
I don't care..maisha ya kumplease kila mtu siyawezi..
Mara ooh hajichangaanyi...sitoki nyumbani bila sababu za maana..ukitaka kuongea na mm njoo nyumbani.
Hadi umri huu nmefika nipo hivyohivyo,sidhani Kama nitabadilika.
And I'm just comfortable na haya maisha.
Hii ya kusema watu wa aina hii wanajisikia ninakumbana nayo sana katika maisha isipokuwa kwa wale wanaonijua vizuri tu.
Najikubali jinsi nilivyo. Kama hakuna cha maana sana huko nje basi ni bora nitulie nifatilie vitu ninavyopenda mtandaoni au vitabuni au kama uwepo wangu unahitajika katika kazi fulani basi nitahakikisha naisimamia kazi hiyo vilivyo bila kutoka hadi imalizike.
Nina hulka ya kujichanganya na kuzungumza vizuri pia hasa kwenye shughuli zenye masilahi ingawa kama hatujazoeana sana kutakua na mazungumzo mafupi tu na ya moja kwa moja na watu ninaofanya nao kazi
 
Kuna video za YouTube zimetumwa hapo juu na wadau, zicheki au ingia YouTube andika INTROVERT VS EXTROVERT, UTAPATA MASOMO YA KUTOSHA.
Yap! video nimeziona na hasa ile ya sign of introverts kama sijakosea dalili zote ninazo hivyo kwa uhakika kabisa mimi ni miongoni mwa introverts sasa basi ningependa kuendelea kujifunza zaidi je?kuwa introverts kuna faida na hasara gani kijamii,kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni?😚 nahitaji utajitambua wajuzi endeleeni kunifungua macho
 
Huyo Ni Mimi mkuu sema Nina wazazi wote sema Mzee alikuwa mkali siyo mchezo, ilikuwa Ni bakora Tu.
Kipindi nipo home wageni wakija Ni mbio chumbani, Unasikia mzee anasema huyo kuongea yake huwa Ni tabasamu Tu.

Leo anasema naamini mawazo yangu Tu kuwa ndiyo sahii Tu.

Kwakweli hii hali naona siyo nzuri sababu inaleta msongo WA mawazo japo Ni Fan WA mpira, lakini Kuna kipindi naongeleshwa nichangie wapi Ni kimya Na tabasamu Tu.

Nimeanza remedies hapa, kwa kuchangia mada za dini, sometimes naachana Na simu Na PC Na kufuata watu physically tuongee japo kidogo coz nilikuwa naongea Mwenyewe ndani kwa ndani Na nikikosa solution naumia Sana kimya kimya.

Pitia www.youthAliveportal.com utapata resources za kufanya remedies za kiasili hata hiyo ya kumeza sawa ili kusolve msongo siyo nzuri.

Mkuu "Honk up"
Wewe ni mimi ndani ya wewe!!!!!
 
Njia rahisi zaidi kuliko zote za kujichanganya na watu ni kununua njumu au Snickers za kuchezea basket then unaingia uwanjani. hakuna mwanaume atakaekufukuza uwanjani au kukukataza usiguse mpira. hapo utapata marafiki wengi, sometimes mnakua mnaamshana weekend mkafanye mazoezi, wengine wanakuadd hadi kwenye groups za whatsapp.
mkiwa na communication nzuri mnapanga hadi skukuu mkatembee wapi. Mnatengeneza Real brotherhood!
Duu!
 
Mimi pia nipo ivoo tangu utoto.

Ni mtu wa kukaa pekeyangu sipend kabisa kukaa na watu kujichanganya.
Nimelelewa na wazazi wote wawili
Wamejitahid sana sana lkn bado.
Sipend kuongea adi inibidi
Ata mtu akinikosea siwez kumwambia
Sipendi kujichanganya ata ikitokea nkajichanganya for 2hr nahis naloose enegy

Iyo tabia imenipelekea kutokuattend kwenye vipind class kipindi nasoma
Ata discussion sikuwai fanya
Church nlikua sipendi kwenda

Mpaka sasa nnarafiki mmoja tu.

Napoishi sasa ni miaka 4 lakin sina ata jirani naeongea nae
Sina aibu ila sipendi watu
Mtu wa karibu sana kwangu ni gf basi

Ata familia yangu naongea nayo mara chache sana
Sijali sana watu na hiki ndo kinachoniumiza zaid.
Bt i think mzee wangu nae yupo ivi kama mim
Ipo kama mimi ila tilofauti ni kwamba mzee wangu mm hana sifa kama za mzee wako
 
Hii ya kusema watu wa aina hii wanajisikia ninakumbana nayo sana katika maisha isipokuwa kwa wale wanaonijua vizuri tu.
Najikubali jinsi nilivyo. Kama hakuna cha maana sana huko nje basi ni bora nitulie nifatilie vitu ninavyopenda mtandaoni au vitabuni au kama uwepo wangu unahitajika katika kazi fulani basi nitahakikisha naisimamia kazi hiyo vilivyo bila kutoka hadi imalizike.
Nina hulka ya kujichanganya na kuzungumza vizuri pia hasa kwenye shughuli zenye masilahi ingawa kama hatujazoeana sana kutakua na mazungumzo mafupi tu na ya moja kwa moja na watu ninaofanya nao kazi
Like me
 
Namuonaga jamaa unamuona ana stress mbaya haongei..unamkuta anaongea alone...! speak speak speak! mie magonjwa ya stress nilishapishana nayo msamvu round about aisee..siyapi nafasi...na sitak jitesa kwakweli..!polen
Hongera zako maana ungejifanya kuyafuata kuvuka hiyo round about ya msamvu tu saiz tungekuwa tumekujumlisha kwa wale waliofanywa mishikaki kwa muuni kuchomoa betri
 
Habarini,
Kuna jambo linanipa wakati mgumu sana hivyo ningeomba ushauri au kama kuna mwenzangu analipitia hili anisaidie kimawazo alilikabili na kulishinda vipi.

Maisha yangu ni kwamba nililelewa na mama yangu mkubwa,sababu mzee sikuwahi kumuona na bimkubwa alifariki nikiwa na umri mdogo sana,Hivyo familia ya dada wa mama yangu ndo amenilea mpka nimefikia hapa.

Kwa elimu nimesaidiwa kusoma mpka level ya diploma kwa kozi ya HRM.

Tatizo ambalo nimekabiliana nalo na ambalo nimeshindwa mpka sasa kuliepuka ni hali ya kutopenda kujichanganya na watu na kutokupenda kabisa kuongea na watu, nadhani kwa wenzangu wengi wana marafiki wa primary,secondary na hata wale walosoma nao chuo pamoja,Lakini kiupande wangu hali haipo hivyo kwani toka nimeanza darasa la kwanza mpka leo nimemaliza chuo sijawahi kuwa na rafiki wa kiume wala wa kike japo utaniongelesha ntakujibu ulichoniuliza tu baada ya hapo naondoka.

Kwa maisha ya shuleni ilikuwa ukifika mda wa kurudi nyumbani au mwalimu akimaliza kufundisha tu basi naweka madaftari kwenye begi njia moja kwa moja nyumbani popote utaponiona popote ntapotembea ntakuwa peke yangu,japo ni watu wengi sana walifosi kuwa karibu nami wakati nasoma but ukiwa unaniongelesha tu mara kwa mara naweza kukukimbia au kuanza kukukwepa.

Katika ngazi ya familia na hata ndugu,mfano naweza kupigiwa simu na mtu nnayemfahamu nikaiangalia simu mpka ikakata au nikapigiwa simu nimaizima na kutoa kabisa betri,alafu baadae nikamtafuta tu kwa mesage na ntapenda unijibu kwa mesage pia yani usinipigie.

Nyumba zote nlizowahi kupanga na hata hii nlopanga mpka mda huu kuna madada wapo tu nje wanasubiria ntoke waniongeleshe inshort wanataka tuzoeane but nna mwezi wa saba naishi nao hakuna tuongeacho zaidi ya salamu tu hata jina langu halisi hawalijui wala nashughulika na nn hawajui zaidi ya kuhisi,hisi tu

Upande wa mahusiano nna mpenzi wangu,yeye ni muongeaji kweli kweli lakini toka niwe nae naona na yeye ameshaanza kubadilika maana alishafanya vitu vingi mno vya kukorofishana but mwisho wa siku anajirudi baada ya kukutana na reaction tofauti kiasi cha kuniambia wakati mwengine japo nimpige ili aamini kuwa yameisha.

Nimeyaandika haya baada ya kukosa kazi zaidi ya 5,ningependa kuelezea hii ya mwisho.

Niliitwa na mtu baada ya kuweka tangazo la kutafuta kazi humu jf,basi kuna mtu akanipigia simu niende kuna kazi fulani,basi baada ya kwenda nafika pale nilichelewa kama dakika 5,mzee akawaka mpka basi kwanini nimechelewa na matusi juu mzee sema sana but reaction ambayo nilionyesha yule mzee baadae alinipa elf 50 ya nauli na kuniomba radhi then akanambia atanitafuta baada ya mahojiano baada ya kufika nyumbani akanipigia simu na kunambia kijana wangu samahani kwa yaliyotokea pia niombe radhi kuwa sitaweza kukuajiri kwani watu kama wewe wakimya na tabia zangu naogopa unaweza kunifanya kitu cha ajabu,basi kazi ikaishia hapo

Je, kuna mwenzangu anaepitia hali hii na je ulifanya vipi kukabiliana nayo?najiona tofauti mwenzenu msaada wenu wa ushauri unajitajika
Ndio wapo ila ni wachache sana rafiki.kwa njinsi navyojua watu wenye tabia hii sanasana ni wale wenye element za ujiniaz.intellent people(genius) mara nyingi uwa kivyao na kujikuta hata wakiongea wenyewe kwa sauti na hii inasababishwa na wao kufikiri tofauti sana na wengine kupelekea kuwakwepa watu kwa7bu ya small talk.genius wanachukia sana small talk,negative mind hata watu wakiwa wanaongea kichinichini (kunongozena) huwa wanachukia sana kwani wanapenda sehemu zenye utulivu kama library.hata kama wakiwa kwenye group assgment mtu huyu hanaweza kwanza hasionekane kabisa au akiwepo basi hatoongea neno hata moja na kama akiongea basi wazo lake uwa tofauti kabisa hvyo anaofia kuofiwa.Yote hii inasababishwa na brain kufikiri fasta na kusolve mambo makubwa na kupelekea kuchukia maongezi madogo.
Dalili za huyu mtu.
1. kuchelewa kulala
2.kusahausahau vitu vidogo
3.kujitenga na watu (kama ulivyosema)
4.kuwa na mawazo makubwa
5.mezani kwa chumba chake uwa lafu(lakini hapa kukiwa na nondo mbalimbali kama vitabu na picha za hamasa ukutani)
6.kufikiri chanya zaidi
7.kupenda kujifunza
8.kujua hisia/tatiza la mtu kwa kumuona tu hata kama hajaambiwa
9.kupenda kupumzika mara kwa mara
10.kuwa na uwezo wa kukopi mazingira fasta (mfano kazini hata akiwa mgeni wiki moja anauwezo wa kuwakopy na kuendana nao sawa kama mtu aliyekuwa miaka kadhaa iliyopita.ila mbaya kama hakuna jambo mawazo na changamoto mpya za kazi.basi anaboweka haraka sana,labda anaweza acha kazi.
Sasa ndugu kaza unazo moja ya tabia hizi basi unaweza ukawa upande huo.kwa maelezo zaidi ingia youtube google characteristic of genius.
 
Back
Top Bottom