Nashindwa kujielewa ni mimi tu 'nisiyependa kujichanganya na watu' au kuna wenzangu wapo hivi? Msaada tafadhali

jerryempire

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
5,128
8,646
Habarini,
Kuna jambo linanipa wakati mgumu sana hivyo ningeomba ushauri au kama kuna mwenzangu analipitia hili anisaidie kimawazo alilikabili na kulishinda vipi.

Maisha yangu ni kwamba nililelewa na mama yangu mkubwa,sababu mzee sikuwahi kumuona na bimkubwa alifariki nikiwa na umri mdogo sana,Hivyo familia ya dada wa mama yangu ndo amenilea mpka nimefikia hapa.

Kwa elimu nimesaidiwa kusoma mpka level ya diploma kwa kozi ya HRM.

Tatizo ambalo nimekabiliana nalo na ambalo nimeshindwa mpka sasa kuliepuka ni hali ya kutopenda kujichanganya na watu na kutokupenda kabisa kuongea na watu, nadhani kwa wenzangu wengi wana marafiki wa primary,secondary na hata wale walosoma nao chuo pamoja,Lakini kiupande wangu hali haipo hivyo kwani toka nimeanza darasa la kwanza mpka leo nimemaliza chuo sijawahi kuwa na rafiki wa kiume wala wa kike japo utaniongelesha ntakujibu ulichoniuliza tu baada ya hapo naondoka.

Kwa maisha ya shuleni ilikuwa ukifika mda wa kurudi nyumbani au mwalimu akimaliza kufundisha tu basi naweka madaftari kwenye begi njia moja kwa moja nyumbani popote utaponiona popote ntapotembea ntakuwa peke yangu,japo ni watu wengi sana walifosi kuwa karibu nami wakati nasoma but ukiwa unaniongelesha tu mara kwa mara naweza kukukimbia au kuanza kukukwepa.

Katika ngazi ya familia na hata ndugu,mfano naweza kupigiwa simu na mtu nnayemfahamu nikaiangalia simu mpka ikakata au nikapigiwa simu nimaizima na kutoa kabisa betri,alafu baadae nikamtafuta tu kwa mesage na ntapenda unijibu kwa mesage pia yani usinipigie.

Nyumba zote nlizowahi kupanga na hata hii nlopanga mpka mda huu kuna madada wapo tu nje wanasubiria ntoke waniongeleshe inshort wanataka tuzoeane but nna mwezi wa saba naishi nao hakuna tuongeacho zaidi ya salamu tu hata jina langu halisi hawalijui wala nashughulika na nn hawajui zaidi ya kuhisi,hisi tu

Upande wa mahusiano nna mpenzi wangu,yeye ni muongeaji kweli kweli lakini toka niwe nae naona na yeye ameshaanza kubadilika maana alishafanya vitu vingi mno vya kukorofishana but mwisho wa siku anajirudi baada ya kukutana na reaction tofauti kiasi cha kuniambia wakati mwengine japo nimpige ili aamini kuwa yameisha.

Nimeyaandika haya baada ya kukosa kazi zaidi ya 5,ningependa kuelezea hii ya mwisho.

Niliitwa na mtu baada ya kuweka tangazo la kutafuta kazi humu jf,basi kuna mtu akanipigia simu niende kuna kazi fulani,basi baada ya kwenda nafika pale nilichelewa kama dakika 5,mzee akawaka mpka basi kwanini nimechelewa na matusi juu mzee sema sana but reaction ambayo nilionyesha yule mzee baadae alinipa elf 50 ya nauli na kuniomba radhi then akanambia atanitafuta baada ya mahojiano baada ya kufika nyumbani akanipigia simu na kunambia kijana wangu samahani kwa yaliyotokea pia niombe radhi kuwa sitaweza kukuajiri kwani watu kama wewe wakimya na tabia zangu naogopa unaweza kunifanya kitu cha ajabu,basi kazi ikaishia hapo

Je, kuna mwenzangu anaepitia hali hii na je ulifanya vipi kukabiliana nayo?najiona tofauti mwenzenu msaada wenu wa ushauri unajitajika
 
Hiyo tabia ni kama ulemavu fulani. Honestly inakukosesha baadhi ya vitu ambavyo ungevipata kirahisi.
Pambana dhidi ya huo ulemavu for your own sake.
Nenda mahala watu wanakunywa kahawa, wanacheza pool table, wanashabikia mpira n.k nawe utoe hoja...taratibu utaanza kuzoea kisha utajichanganya na watu wa level unayoipendelea zaidi.
 
Hiyo tabia ni kama ulemavu fulani. Honestly inakukosesha baadhi ya vitu ambavyo ungevipata kirahisi.
Pambana dhidi ya huo ulemavu for your own sake.
Nenda mahala watu wanakunywa kahawa, wanacheza pool table, wanashabikia mpira n.k nawe utoe hoja...taratibu utaanza kuzoea kisha utajichanganya na watu wa level unayoipendelea zaidi.
mpira haupo kabisa,kwenye damu pool ndo sijawahi kulicheza wala kufkiria kucheza toka nizaliwe kwenye vijiwe vya kahawa nilishawahi pita mara 2 but habari zote wanazodanganyanaga huwa najua ukweli,unakuta mtu anadanganya wenzake yuko serious kabisa na mm ukinidanganya au ukiwa muongo tu huwez kuniona kamwe
 
Mimi si muongeaji sana,sipend kujichanganya na watu na si mkimya sana ila sipend mtu anaeongea sana
Huwa nahis kama inzi ama mbu wanavyopiga kelele ukiwa umelala ila sijafkia hatua yako,
Kwa mtazamo wangu sion kama ni tatizo,nshamwona mtu kama huyo na alitamani kuwa kawaida ila hiyo hali ni zaidi ya tabia,haikuwah kupungua na ukimuudh inakua mara dufu
 
Back
Top Bottom